Kifo cha "KAKA" chaacha pengo katika soka Mkoani Mbeya , hasa TUKUYU STARS , Mamlaka za michezo zapuuza kifo chake .

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Ama kwa hakika kwenye nchi hii we jitendee wema ujiondokee !

kifo cha Ramnik Patel maarufu kama KAKA , aliyewezesha timu ya Tukuyu Stars ya mjini Tukuyu , Wilaya ya Rungwe , mkoani Mbeya kutikisa soka la Tanzania na kutwaa ubingwa wa ligi kuu mwaka 1986 , kimenikumbusha kwamba , nchi hii ni miongoni mwa nchi chache duniani zisizo na shukrani , nguli huyu wa soka la Tanzania ni kama alishatupwa na kutelekezwa hata kabla hajakata roho , wema wote aliolitendea soka la nchi hii imeonekana ni kazi bure !

Kwa vijana wa sasa huyu ndiye mfadhili na mdhamini wa mwanzo kabisa wa soka la Tanzania , alijitolea pesa zake binafsi kuinua soka mkoani Mbeya , huyu ndio amesababisha nchi hii kuwa na wachezaji mahiri kama Godwin Aswile , Justine Mtekere , Mh Suleiman Methew , Sekilojo Chambua , Jimmy Mored , Mbwana Makata , Steven Musa na wengine kibao , lakini pamoja na wema wake katika soka la Tanzania bado " amekufa peke yake " , yaani pamoja na kifo chake bado hakuna hata kiongozi aliyestuka au japo kupata majonzi !

Nakulilia Tanzania .
 
Nilimuona siku moja akihojiwa na AZAM TV, Dah ndo napata taarifa hapa kuwa
amefariki, ilitakiwa hata dakika moja tusimame kabla ya mechi kama maombolezo.
Yeye, Gulamali, Azim Dewji n.k ni watu wanastahili heshima kubwa katika soka letu.
 
Dah umenikumbusha Abbas Gulamali Rais wa kwanza Yanga Wakimataifa. R.I.P.
 
Nilimuona siku moja akihojiwa na AZAM TV, Dah ndo napata taarifa hapa kuwa
amefariki, ilitakiwa hata dakika moja tusimame kabla ya mechi kama maombolezo.
Yeye, Gulamali, Azim Dewji n.k ni watu wanastahili heshima kubwa katika soka letu.
Kabisa
 
Ama kwa hakika kwenye nchi hii we jitendee wema ujiondokee !

kifo cha Ramnik Patel maarufu kama KAKA , aliyewezesha timu ya Tukuyu Stars ya mjini Tukuyu , Wilaya ya Rungwe , mkoani Mbeya kutikisa soka la Tanzania na kutwaa ubingwa wa ligi kuu mwaka 1986 , kimenikumbusha kwamba , nchi hii ni miongoni mwa nchi chache duniani zisizo na shukrani , nguli huyu wa soka la Tanzania ni kama alishatupwa na kutelekezwa hata kabla hajakata roho , wema wote aliolitendea soka la nchi hii imeonekana ni kazi bure !

Kwa vijana wa sasa huyu ndiye mfadhili na mdhamini wa mwanzo kabisa wa soka la Tanzania , alijitolea pesa zake binafsi kuinua soka mkoani Mbeya , huyu ndio amesababisha nchi hii kuwa na wachezaji mahiri kama Godwin Aswile , Justine Mtekere , Mh Suleiman Methew , Sekilojo Chambua , Jimmy Mored , Mbwana Makata , Steven Musa na wengine kibao , lakini pamoja na wema wake katika soka la Tanzania bado " amekufa peke yake " , yaani pamoja na kifo chake bado hakuna hata kiongozi aliyestuka au japo kupata majonzi !

Nakulilia Tanzania .

Hii ndio Tanzania mkubwa. Umenikumbusha kifo cha Kocha (alikuja baadae kuwa Mchungaji na Makamu Mwenyeketi wa Kanisa la Moravian) Mzee Elijah Kategile. Huyu ndie aliekuwa kocha wa Taifa Stars iliyofuzu kwa mara ya kwanza (na pekee hadi sasa) Fainali ya Mataifa ya Afrika Lagos 1980. Kuna watu waliamua kumpa hiyo sifa Joel Bendera - ambae katika uhai wake sikuwahi kumsikia akikanusha ili kuweka kumbukumbu sahihi.

RIP KAKA! Wewe ulikuwa mzalendo wa kweli wa nchi na mpenda michezo kwa vitendo.
 
Vijana wa siku hizi wanasema kuwa mzalendo kwa Taifa lako ni sawa na kujitwisha mzigo wa miba.Tafakari na chukua hatua
 
kaka ndiye miongoni wa wafadhili wa kwanza kufadhili timu za mikoani tofauti na wengine waliokuwa wanakimbilia simba na yanga kupata umaarufu
 
Hiyo timu ilikuwa imekamilika. Hapo ongeza David Mwakalebela, Selemani Said Sanga na Salum Kabunda. Sifa moja ya wachezaji wengi wa timu hii walikuwa hawaonekani kama wachezaji mpira ukiwaona mtaani(kama walivyokuwa wachezaji wa Cameroon kina Geremy Njitap) lakini muziki wao uwanjani ulikuwa hatari.
Any wise, RIP Mzee Ramnik Kaka
 
Asante mkuu
 
Mwakalebela mtoe hapo kumbukumbu zinaonyesha hakupitia tukuyu stars wengine wote sahihi
 
Back
Top Bottom