Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Ama kwa hakika kwenye nchi hii we jitendee wema ujiondokee !
kifo cha Ramnik Patel maarufu kama KAKA , aliyewezesha timu ya Tukuyu Stars ya mjini Tukuyu , Wilaya ya Rungwe , mkoani Mbeya kutikisa soka la Tanzania na kutwaa ubingwa wa ligi kuu mwaka 1986 , kimenikumbusha kwamba , nchi hii ni miongoni mwa nchi chache duniani zisizo na shukrani , nguli huyu wa soka la Tanzania ni kama alishatupwa na kutelekezwa hata kabla hajakata roho , wema wote aliolitendea soka la nchi hii imeonekana ni kazi bure !
Kwa vijana wa sasa huyu ndiye mfadhili na mdhamini wa mwanzo kabisa wa soka la Tanzania , alijitolea pesa zake binafsi kuinua soka mkoani Mbeya , huyu ndio amesababisha nchi hii kuwa na wachezaji mahiri kama Godwin Aswile , Justine Mtekere , Mh Suleiman Methew , Sekilojo Chambua , Jimmy Mored , Mbwana Makata , Steven Musa na wengine kibao , lakini pamoja na wema wake katika soka la Tanzania bado " amekufa peke yake " , yaani pamoja na kifo chake bado hakuna hata kiongozi aliyestuka au japo kupata majonzi !
Nakulilia Tanzania .