Hata mimi sishangai kusikia Business Times ina hali mbaya. Nina muda mrefu tangu nilipojiondoa katika kampuni hiyo. Lakini nasikia sasa mambo hayaendeshwi kitaalamu. Ukishakuwa mtoto wa mwenye kampuni inatosha kupata nafasi ya kazi. Ukiacha GM ambaye baadhi tu ya wafanyakazi wanasema ana busara na msikivu, kuna mwingine ambaye wafanyakazi wenzake wanadai hawamwelewi kwa sababu haeleweki. Nasikia ingawa huyo mwingine wanayemwita Immma hana taaluma yoyote ya uandishi na wala hajawahi kuandika makala au habari yoyote, yeye sasa ni mhariri mkuu wa gazeti la Darleo. Mtu mmoja akaniambia anahudhuria pia vikao vya jukwaa la wahariri. na sijui kama wahariri wanaokutana wanaulizana taaluma zao. kama yote hayo ni ya kweli, kwanini nishangae ninaposikia BTL iko taabani wakati inaendeshwa na watu wasiojua wanachokifanya? kama ninayosikia ni ya kweli, kuna siku mhariri mkuu wa majira atakuwa mtoto wa mwenye kampuni, na kisha magazeti mengine kama spoti starehe na business times lenyewe. sasa wameanza na darleo, mengine yatafuata. sishangai kila nikisoma majira nakuta halina mhariri bali lina kaimu wake. anayekaimu nafasi hiyo ni John Mapinduzi. Yeye asubiri mhariri mkuu wa Majira atakapokuja kutoka familia ya mwenye kampuni. Nikifikiria hayo hata nikiambiwa nirudi business times nitakataa. Na tangu nilipoondoka 2006 sijajuta. Hiyo ni kazi ya familia. Kama bado kampuni itakuwepo mabadiliko yake yatakuwa hivi: Mkurugenzi wa Business Times Ltd, Baba Mbuguni. Meneja Mkuu, Mtoto Mbuguni, Mhariri Mkuu Majira, Family3 Mbuguni. Mhariri Mkuu Darleo, Family4 Mbuguni, Mhariri Spotistarehe, Family5 Mbuguni, Mhariri Mkuu Business Times, Family6 Mbuguni. Meneja Mkuukiwanda cha uchapaji, Mr1 Mbuguni, nk, nk. Vikao vyote vya utawala vitafanyika nyumbani na maamuzi kufanyika huko huko. Halafu mnashangaa kampuni isife!!!!!!!!!!!!!!!!????????????