Kifo cha kampuni ya mabasi SCANDINAVIA EXPRESS

Kifo cha kampuni ya mabasi SCANDINAVIA EXPRESS

Chuma

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2006
Posts
1,324
Reaction score
43
Naomba kuuliza kwa wale wenye data za usahihi Kufeli au kufilisika kwa mabasi ya scandinavia ktk muda mfupi tu...Jamaa alijitahidi mno, na kila ukifika ofisi zake unaona bora kuliko kwenda Ubungo...Mabasi mapya, leo mabasi yamechoka kama unakwenda Mtwara au Lindi? wenye data niwekeni sawa...
 
alikuwa akija so fast hadi compete na POSTA ktk kusafirisha vifurushi..leo ukifika hapa kamata hata AC hakuna, Joto kwenda Mbele...Magari hayakosi ubovu kila kilometer xy
 
kuna kipindia CRDB walitaka kupiga mnada mabasi yake, lakini alitetewa sana!
mimi nasikitika sana kwa hali iliyomfika, kwani sisi wa mtwara tulisema barabara ikiisha tu na sisi tutapanda scandinivia, naona hilo haitawezekana kwa hivi karibuni,
lakini naamini akifanya juhudi za makusudi atainuka tena, hiyo ni hali ya kwaida katika biashara, matsushita iliingia hadi kwenye -ve sell!
Hata scandinavia anaweza kujinasua hapo alipo na kuchipua tena!
 
"Sina Uhakika", msije mkasema Idimi alisema, ila inasemekana kwamba yale mabasi yalikuwa ni syndicate ya kampuni kadhaa ambazo zilikuwa zinatumia jina moja hilo kufanya biashara. Inasemekana walifarakana na kila mmoja akafa na chake, na sasa kampuni inatapatapa.
Ni kweli kwamba kwa sasa mabasi yale hayaaminiki tena, ni mabovu mno! Kuna siku nimepanda kutoka Dar Kwenda Zambia, likafia pale Ifunda, lilihitajika kushusha injini kabisa. Fikiria mtu ambaye unawahi deadline na kadhia kama hiyo!
 
Issue ya Scandinavia Express, iko wazi sana, kampuni ilikuwa inadaiwa na wadai mbalimbali.

1. Mabenki (mawili hadi matatu)

2. Makampuni ya Mafuta ya Petrol.

Ikafika wakati walitaka kufilisi... hivyo creditors wote wakajitokeza... wote creditors wakagundua asset za Scandinavia Express haziwezi kulipia madeni yote... Nadhani walikubaliana bora kampuni iendelee ili iweze kulipa madeni kidogo kidogo...

Search google utapata mengi... "Scandinavia Express Kufilisiwa" au text zingine lakini ziwe na neno kufilisi/wa

Mfano http://216.69.164.44/dar/Biashara/2005/11/09/12065.html
 
Hili la Wadeni na kesi zao lilikuwa wazi kabisa na nafikiri suala la Mahakama ikatoa uamuzi kuwa hilo ni jambo la kawaida ktk business kubwa.

Kwangu mie Mikopo ya RIBA lengo lake si kumsaidia mkopaji, bali mtoaji. Na ndo maana wengi wa watu n makampuni yao wameona njia nyepesi ya ku-WIN si tu kukopa bali kuibia Bank au Asasi za Serikali.Business as business lazima iwe na profit n Loss, wakati wewe unapata LOSS bado deni lako la Bank lipo pale.

Hivi kuna hisia zozote za kuwa amehujumiwa na Big tycoon yoyote?..mwenye data anaweza tusaidia...najua jamaa alisaidia mno kuwapeleka wajumbe CHIMWAGA...sijui alikuwa ktk base ya ZERO au EL or whatever...Kipindi kile bado kibiashara alikuwa bado yupo FIT, soon after election biashara zikaanza Kuyumba kwa 100%
 
ikiwa nyie ni watanzania nadhani inapasa tuwe wazalendo wa kweli na musiiponde kampuni ya kizalendo ilioyofanya mashirika ya umma yaliyokuwa yakipewa ruzuku yalishindwa kufanya.

Scandinavia ilihujumiwa na ma tycoon wachafu wasioitakia mema TZ. Hao ndio walioipania kwa sababu za uroho wao na kwa sababuimeondoa dhana ya TZ kuwa ina shida ya usafiri, kwani hilo ndilo kigezo waliokuwa wakiiibia taifa letu. Hao ni maadui ambao hata passport zao sio za kitanzania na waliungana kutengeneza njama za kujaribu kuiuwa.

Scandinavia iko mbioni kuweka huduma zake bora kuliko mwanzo kwa sababu inaleta mabasi mapya. Na kusema ukienda kamata hakuna hata ac sio kweli, kwa sababu nilituma vifurushi zangu wiki ya jana na kutuma fedha pia na terminal yao inayo ac na huduma yao ni safi. tuweni wazalendo na tusikubali kutiwa sumu na maadui wasiotakia mema taifa letu. Hao hao walioitilia fitina Scandinavia kwa kutumia rushwa na uhusiana wao na baadhi ya wafanya kazi mabenki waliorubumiwa ni bila shaka wamo katika watu walioibia BOT. Yupi bora, Scandinavia ambayo deni lake au madeni yake ambayo alikuwa akilipa vizuri kabla ya kupigwa vita na kuhujumiwa, hata kwa ujumla wake haifikii hata asilimia kumi ya fedha zilizoibiwa na kampuni moja kati makampuni 22 ambazo nyingi na fake na za wa asia, au hao walioiba ?

Scandinavia biashara yake ni halali na wala hakuwa na tatizo. Tusipoamka na kuwa macho na badala yake tukawa tunaungana na wabaya wa taifa letu kupakaza matope watanzania wenzetu walio wana uchungu wa maendeleo ya nchi yetu, tutaburuzwa siku zote. Tusidanganyike na choko choko zisizo za msingi. ingekuwa Scandinavia ameiba kama walivoiba BOT musingethubutu kusema uzushi kama vile hakuna ac kwenye termino yao.

Jama tuamkeni tusiendeshwe na wafanya biashara za haramu wachache wakajenga sumu za kuchukia kampuni iliotowa muhanga kwa ajili ya uchu wa kutrupa mawendeleo
 
Scandinavia OYEEEEEEEEEEEE, jamani tusitumike na watu kumpiga vita Skandi, skandi amejitahidi na amepambana na Mungu atamjaalia mshindi. Nadhani hapa tulie na wanaotuibia fedha zetu na kutuuzia chakula kibovu na wanaokimbiza mali zetru nje ya taifa lertu
 
CRDB alitumiwa na mfanya biashara mmoja aliozoea kudhulumu taifa hili na hakuna lolote kingine.

Njama zilipikwa kwa kutumia mwanasheria fulani aliwahi kuwa hakimu na akafukuzwa kwa rushwa na akafanya uwakili na akafungiwa na Serikali kwa ajili ya rushwa na game zake ndio tenda za kuhujumu watu wema. Suala la mafuta likikuwa feki pia, ni katika kutaka kutengeneza majungu ya kummchapia nayo skandi. kwani skandi ameonekana kuwa na misimamo ya kutetea maslahi ya watanzania na taiofa zima katika shughuli zaske ambayo ni kinyume cha matakwa cha hao wafisadi waliotaka kumuingiza katika kundi lao la ubaguzi warangi na ukabila. Wanadhani na kuamibni wenye uwezo na haki ya kluwa na kitu ni wao tu na si watu wengine.

Mengi wa IPP alishahujumiwa na anahujumiwa mpaka leo kwa kuwa ni mzalendo pia na wengi kama hao. Mbona wanayoibia serikali yetu na wanaotuuzia chakula kibovu na wanaotuuzia pembejeo mbovu ambayo hata ruzuku yake waliopewa bna swerikali ili mbolea iwe nafuu lakini hao huiba hatuwazungumzii ? au tunawaogopa kwa kuwa ni watu wa aina fulani ?

Crdb ni ya kuangalia sana kwani pamoja na kijifanya benki kubwa lakini ni one man show na hakuna lolote bali ni wasanii tu ambae kiongozi wake yuko bize kufanya fitina apate kuwa gavana jambo ambalo ni hatari kwa taifa letu izingumzwe kuwa crdb ichunguzwe kama ilivochunguzwa BOT ndio tutafahjamu ukweli wa mambo haya
 
Duuuh!!

Simba, watu hawajaikandia scandinavia, bali wana uliza tu, swala la kukosa AC kutajwa lisikukondeshe ndugu... ni kitu kidogo hicho. Ila tuna shukuru kwa data zako. Endelea kutumwagia pls!

SteveD.
 
"Sina Uhakika", msije mkasema Idimi alisema, ila inasemekana kwamba yale mabasi yalikuwa ni syndicate ya kampuni kadhaa ambazo zilikuwa zinatumia jina moja hilo kufanya biashara.

Ni kweli kwamba kwa sasa mabasi yale hayaaminiki tena, ni mabovu mno! !

Kuwa katika 'syndicate' ni jambo la kawaida katika biashara, mfano chain stores/supermarkets (sina uhakika kwa TZ) zipo katika mtindo huo.Mradi wamiliki wote wanajua lengo, dhumuni na kanuni yao ni moja.

Mabasi ya sacandinavia ni kweli ni mabovu,ukipanda huna uhakika kama utafika on time, pamoja na hayo wanajitahidi sana kumaintain huduma zao, hiki ndicho kinanifurahisha, angalau 'wana ka customer care'.
 
Asante kaka steve, nakushukuru, na nimekuelewa na najuwa hawakuwa wakikandia ila hali ya sasa inatisha kwani kuna watu wafisadi wanatumia njama tofauti ya kuchafuwa watu na kwa kuwa forum hii ndio ya kuamsha na kudhirisha ufisadi huo wao wakajaribu kutaka kutuondoa na kutuipeleke katika kuitumia watakavyo wao. tuko pamoja

simba
 
All in all and regardless of what happened ile kampuni haikustahili kabisa kufika hapo ilipo kwa sasa. Ilikuwa ndio kampuni yenye huduma za kipekee East Africa. Mabasi mazuri, decent services, reliable na mengine mazuri mengi tu. Tungekuwa na serikali makini ilipaswa kuingilia kati hata kama ni kwa kuikopesha, and the kuajiri independent company kusimamia taratibu. Lakini kama tunavyojua kwa bongo hiyo ni ngumuu mno!
 
SteveD

Anachoongea Simba ni dhahiri.....kuanguka kwa Scandinavia ni result ya mchezo mchafu baina ya wafanyabiashara wakubwa na ndugu zao waliomo ktk hiyo biashara ya transportation..........

Unajua Watanzania tuko mahali pabaya sana kwamba fate yetu huamuliwa na wafanyabiashara matapeli na ndio hao wanaosumbua wafanyabiashara wengine, tuliowagusa kule BoT....ni %ge ndogo sana....kazi tunayo

angalia maneno ya Simba ni mazito sana.........kuanzia kwa waleta pembejeo mpaka wanaoleta vyakula vibovu..........unakumbuka viwanda vyetu vingi vya maana kama vya kutengenza viatu, kubanjua korosho na vya nguo vilikufaje.........unakumbuka Tea Blenders na umaarufu wake, UDA et al...........watu wanahujumu kwa kisingizio cha ushindani wa kibiashara.........
 
All in all and regardless of what happened ile kampuni haikustahili kabisa kufika hapo ilipo kwa sasa. Ilikuwa ndio kampuni yenye huduma za kipekee East Africa. Mabasi mazuri, decent services, reliable na mengine mazuri mengi tu. Tungekuwa na serikali makini ilipaswa kuingilia kati hata kama ni kwa kuikopesha, and the kuajiri independent company kusimamia taratibu. Lakini kama tunavyojua kwa bongo hiyo ni ngumuu mno!

Unachosema ni kweli kabisa ndungu Nyambala.
Huwa baadhi ya serikali duniani huwa na sera za "kulinda" makampuni hata ya watu binafsi pale mambo yanapoonekana kwenda kombo! Huwezi kujua kuwa kampuni kama hii inaajiri watu wangapi kwa Afrika mashariki yote, achilia mbali hapa Tanzania! Sasa kama inafilisika, je ni watu wangapi watakosa ajira? Ni familia ngapi zitakosa kipato? Wenzetu walioendelea, mahali popote ambapo watu hupata shibe yao halali basi serikali hupalinda sana pasichafuke, ili kulinda ajira na kodi!
Kwetu je?
 
Simba na Wengine lengo la kuuliza ni kupata data za uhakika. sote tuna uchungu na nchi.Hao mafisadi wataje Waziwazi. Kama kuna wafanya biashara wanaofanya hujuma dhidi ya wengine wataje.
 
Naomba nitofautiane kidogo.

Tatizo la makampuni mengi nyumbani ni management. Hatujaweza bado kuendesha biashara kitaalam. Overhead zetu ni kubwa mno kwa sababu kila mmoja anayehusika na hiyo biashara anataka kutambilika kama tajiri. Bado tunaendesha biashara kijamii. Hatutilii maanani kuwa mikopo inabidi irejeshwe, na irejeshwe na riba. Wengi bado tunaamini kuwa ukiwaweka watu sawa mikopo itapotea. Hio ilikuwa kweli wakati serikali ilishika utamu lakini siyo sasa.

Mabenki na makampuni ya mafuta yanaendeshwa kwa misingi ya biashara. Umekopa, unalipa. Usipolipa wanachukua hatua zinazostaili bila kuangalia uzalendo. Naamini kabisa ukiangalia kwa ndani, hii kampuni ilikuwa inafuja pesa.

Nani anajua management structure ya Scandinavia? walikuwa wanalipanaje? Gharama zao za kujiendesha? Kote huko kuna matatizo. Yale ya mbele yalikuwa sho tuu, ndani lazima uozo uliishaaanza. Wakiweza na kukubali kujifunza kutokana na hili,na si kuendelea kutafuta mchawi,watarudi na kupata mafanikio kuliko awali. Asset kubwa waliokuwa nayo ni kuwa wateja wao wengi bado wana imani nao. Wajenge kwenye hili. Na baadaye pengine badala ya kupingilia benki, watafute njia mbadala za kuraise funds kama kwenda public.
 
Nimekubaliana na wewe hapa...who knows what kinda management they had in there!!!...Wanatanzania kunalalamika hatupewi mikopo wakina tuna business plans kibao..na tunaposhindwa kulipa ile mikopo tunaanza kutafuta nani mchawi...kampuni zote kinazoweka maslahi ya kampuni mbele ya maslahi ya wamiliki huwa zinasonga mbele na wamiliki hula matunda miaka nenda rudi...
 
CRDB alitumiwa na mfanya biashara mmoja aliozoea kudhulumu taifa hili na hakuna lolote kingine. Njama zilipikwa kwa kutumia mwanasheria fulani aliwahi kuwa hakimu na akafukuzwa kwa rushwa na akafanya uwakili na akafungiwa na Serikali kwa ajili ya rushwa na game zake ndio tenda za kuhujumu watu wema.

Mzee Simba,

Tunaamini wewe ni shupavu kama Simba na sii mwoga! Hapa JF we dare to talk openly! JK, EL, BoT, Maliasili n.k. Hebu shusha nondos na data za CRDB ili kumkoma Nyani kungali kweupe!!!! Inaenlekea unajua mengi ya CRDB over Scandnavia!

Heshima mbele Mkuu!
 
Scandinavia Yaishinda Shell katika Kesi

KAMPUNI ya Scandinavian Express Services Limited, imeshinda kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Kampuni ya mafuta ya Shell Limited.

Shell ilifungua kesi ikitaka Scandinavian ifilisiwe ili iweze kulipwa deni lake la sh zaidi ya bilioni moja inazoidai kampuni hiyo ya usafirishaji.

Hukumu ya kesi hiyo yenye kurasa 36, ilitolewa juzi na Jaji wa Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara, Nathalia Kimaro.

Jaji Kimaro alisema baada ya kupitia hoja za upande wa mashitaka na upande wa utetezi, amebaini kuwa kuifilisi Kampuni ya Scandinavian si jambo la busara.

Alisema anakubaliana na hoja za mawakili wa upande wa utetezi kuwa kampuni hiyo ina mchango mkubwa kwa uchumi wa taifa.

Alisema inasafirisha abiria zaidi ya 2,000 kila siku kwa kutumia mabasi zaidi ya 80.

Mabasi hayo yanafanya shughuli zake katika eneo lote la Afrika Mashariki hadi katika nchi za Malawi na Zambia.

Kampuni imeajiri wafanyakazi zaidi ya 600; ambao Jaji Kimaro alisema kwa hali ya sasa ya ukosefu wa ajira na ongezeko la uhalifu nchini, kuifilisi ni kuleta matatizo zaidi.

Alisema kampuni inatumia sh 69,343,500 kila mwezi kuwalipa wafanyakazi mishahara.

Jaji Kimaro alikubaliana na hoja za utetezi kuwa Scandinavian inao uwezo wa kulipa deni inalodaiwa, na uwezo huo umethibitishwa kwa malipo iliyofanya kwa benki za Euro African, na NBC Limited.

Alikubaliana na hoja kuwa kuyumba kwa Scandinavian kifedha kulisababishwa na mambo kadhaa, yakiwamo ya ajali zilizosababishwa na ubovu wa matairi ya mabasi, na kupanda kwa bei ya mafuta.

“Haya ni mambo yanayochukuliwa kuwa ni ya kawaida katika biashara,” alisema Jaji Kimaro.

Jaji pia alisema kampuni hiyo, licha ya matatizo ya mtiririko wa fedha yaliyojitokeza siku zilizopita, bado inaendelea na shughuli zake kama kawaida, jambo ambalo linathibitisha kuwa inaweza kulipa madeni yake.

“Uamuzi wa kuifilisi utaiua kampuni ambayo ni msafirishaji mkuu wa abiria, mizigo na vifurushi si kwa Afrika Mashariki pekee, bali hadi Zambia na Malawi.

“Inasafirisha abiria 2,000 kila siku na imeajiri wafanyakazi 600; pia ni moja ya walipa kodi. Mahakama inajua matatizo ya ajira yanayoikabili nchi yetu ambayo yameongeza vitendo vya uhalifu,” alisema Jaji Kimaro.

Alisema hoja zilizotolewa na upande wa utetezi ni za msingi na zinazopaswa kuzingatiwa.

“Zilionyesha ni kwa namna gani pande zote mbili zisivyoweza kunufaika kama Scandinavian ikifilisiwa.

“Uamuzi wa kuifilisi utaiua, tatizo la ajira litaongezeka, na pia uhalifu. Uamuzi wa aina hiyo hautakuwa na manufaa kwa jamii,” alisema Jaji Kimaro.

Katika hukumu hiyo, Jaji Kimaro alitoa miezi tisa kwa Scandinavian na kampuni zinazoidai, kuketi pamoja na kutafuta njia sahihi za kulipa madeni hayo.

Katika kesi hiyo, jopo la mawakili wa Scandinavian liliongozwa na wakili wa kujitegemea ambaye sasa ni Jaji mstaafu, Lameck Mfalila.

Kampuni hiyo ilikuwa ikiungwa mkono na benki za NBC Limited, Standard Chartered, Euro Africa na Kampuni ya Scania Tanzania.

Shell ilikuwa ikiungwa mkono na kampuni za Diamond Motors, Sameer Tanzania Limited na Benki ya CRDB. Mawakili wake waliongozwa na Kennedy Fungamtama.


Tuendelee na mjadala
 
Back
Top Bottom