Kifo cha Kanumba kimekupa fundisho gani?.

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Posts
1,002
Reaction score
277
Tupeane pole kwa msiba huu wa mpendwa mwenzetu aliyetutoka,wakati huo sisi kama vijana tukiwa na maswali vichwani mwetu ambayo yanapaswa kujibiwa na sisi wenyewe mojawapo likiwa je mwenendo huu una staha na hatima ya maisha yangu? Nakumbuka kauli ya marehemu babu yangu aliwahi kuniambia,MJUKUU WANGU UNAPOONA UMEFIKIA WAKATI ULIO NA MAFANIKIO SANA KTK MAMBO YAKO KUWA MWANGALIFU SANA JUA KUWA MATATIZO MAKUBWA YANAKUNYEMELEA.Samahanini kama nitakuwa nimewakera ila kauli hii ya babu ya imebeba ujumbe juu ya kifo cha Kanumba na maisha ya wasanii wetu waliobakia.
 
Ukipata mafanikio ktk umri mdogo inabidi uwe makini sana na pia nimejifunza ufreemanson sio mzuri.
 
nimejifunza kunyamaza kimya katika mazingira kama ya kifo cha huyu dogo na pia kifo is nature hakiepukiki, no matter how!
 
Nimejifunza kuwa Kanumba alikuwa hajaelevuka ndiyo maana hakutaka mpenzi wake awe huru kutumia simu yake.
 

Hapa funzo ni kuacha uzinzi hasa wale msiotaka kuoa na kufanya uchumba wa kudanganyana muda mrefu uaminifu hauwezi kuwepo km huna ndoa na mtu na isitoshe huna madaraka ya kumzuia asitembee na mtu mwingine kwakuwa bado anatafuta mzuri
 
Hapa funzo ni kuacha uzinzi hasa wale msiotaka kuoa na kufanya uchumba wa kudanganyana muda mrefu uaminifu hauwezi kuwepo km huna ndoa na mtu na isitoshe huna madaraka ya kumzuia asitembee na mtu mwingine kwakuwa bado anatafuta mzuri

Safi sana nitakapofika nyumbani kwenye desktop nitakupa like yako.
 
Vijana acheni kuishi maisha ya anasa kama wasanii wengi wanavyoishi. Hivi marehemu angekuwa amelala (hiyo saa sita ya usiku) yote hayo yangempata? Binafsi kifo hiki kimenisikitisha sana kwa vile bado alikuwa mdogo sana 28 yrs ndiyo maisha yanaanza halafu anakatika ghafla!! Ila ukweli ni kuwa maisha ya starehe aliyokuwa anaishi ni hatarishi sana. Saa sita za usiku ni muda wa mtu kuwa kitandani anapumzisha hekalu la Mungu sio kutoka kama tulivyomsikia seki akisema kwenye luninga. Poor Kanumba. He did not deserve to die at that tender age. Fundisho ni:- "Vijana mchunge style zenu za maisha, na mchague marafiki wazuri kwa tabia sio sura". Lulu angekuwa na tabia nzuri asingeenda nyumbani kwa mvulana saa sita za usiku na wasingegombana. Tunaambiwa chanzo cha mauti ya Kanumba ni ugomvi. Kijana chunga sana. Kanumba keshamaliza yake ila waliobaki wachukue somo kwenye msiba huu.
 
Ndio maana ukikosa dili kubwa la fedha usilalamike sana uwezi jua kama ungelipata ndio lingekupa ticket kupata mafanikio kwenye umri mdogo ni hatari sana hasa kwa nchi zetu za ki-afrika ambapo hatujazoea! Hivi angekua 50 kweli angewaza atoke outing saa 6 usiku? Angekua 50 si mke wake angekua amelala mda huo? Age 17-35 hapa ukipata hela
inabidi uwe makini sana!
 
Hapa Mungu katoa somo, huyu jamaa mnasema ni kioo cha jamii, tena ni mkombozi wa sanaa, lakini upande mwingine alikuwa ndivyo sivyo, usanii kwa ujumla ni mafunzo ya kijamii ya kuelewesha watu na kuwafundisha, sasa kama huyu anatufundisha starehe, Ubishoo wa Mgari, Ushindani wa Kuchukua wanawake au? ni sawa tulimpenda, lakini labda Mungu alimwona anazidi kupotea kwani aliwahi kuwa karibu na DINI sana na MWIMBAJI wa kwaya sasa kafa kwenye maravidava.
R.I.P. Kanumba Mungu akutangulie, akunusuru jehanamu.Amina
 
Hapa funzo ni kuacha uzinzi hasa wale msiotaka kuoa na kufanya uchumba wa kudanganyana muda mrefu uaminifu hauwezi kuwepo km huna ndoa na mtu na isitoshe huna madaraka ya kumzuia asitembee na mtu mwingine kwakuwa bado anatafuta mzuri

mkuu maneno yako yamenigusa.
 
mie nimejifunza kutomwogopa mwanaume yeyote yule.ukinigeuza punchin bag nakupa dozi yako inayokustahili.utaamua mwenyewe kubak dunian au kwenda akhera.
 
Ukipata hela ya mawazo epuka ulevi, wenye hekima walisema pombe ni mama wa maasi..jama alikunywa hamu ya kugonga ngozi ikamjia kamuita mwenzie, wivu ukafuata na kwa sbb ya pombe alikosa reasoning na ugomvi kufuata. Mwisho MAUTI yakamkuta..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…