Wanabodi,
Kwanza tuendelee kupeana pole kwa msiba wa mpendwa wetu Stephen Kanumba.
Leo nimeisikia taarifa ya awali ya polisi ikielezea mwili wa marehemu umekutwa na jeraha kichwani na kushikiliwa kwa binti Lulu mwenye umri wa miaka 18 kuisaidia polisi katika uchunguzi huo!. Taarifa ya daktari kuhusu kilichosababisha kifo bado haijatolewa!.
Hili ni jukwaa la jamii inteligence likijikita zaidi kwenye facts na sio hisia na hoja hapa sio kupeana pole za msiba wala kumtetea huyu binti Lulu ambaye anataka kibebeshwa msalaba wa kifo cha Kanumba kama mhusika mkuu wakati ukweli halisi kuna kila dalili zinazoonyesha Kifo cha Kanumba japo kimesababishwa na ajali ya kuanguka na kujigonga, kinaweza kuwa kimesababishwa na uzembe wa watu fulani na sio huyu binti Lulu!.(kwanza nilipost kule jamii inteligence ikagoma)
Hoja hii inafuatia maswali mengi bila majibu ya ni nini haswa kilichotokea hiyo jana!.
Wewe kama uu mmoja wa mashabiki wa Kanumba na mpaka sasa una uchungu mkubwa na kifo hiki, nakishauri usichangie uzi huu maana utakosa objectivity na impartiatility kutokana na huzuni.
Hoja za msingi ni hizi.
1. Ugomvi ulitokea saa 6 usiku na mpaka majirani walisikia kelele. Mwili umefikishwa hospitali ya Muhimbili saa 11 Alfajiri, nini kilitokea hapo kati?.
2. Mdogo wa marehemu aliyekuwa nyumbani wakati huo ameongea kwenye TV kuwa aliposikia ugomvi akaenda kutoka kuingilia mlango ukafungwa kwa ndani, akaendelea kusikia vishindo ambavyo na majirani walivisikia, what did he do?, au mlango ukishafungwa basi ni kujiachia tuu liwalo na liwe, hapa sio kuna uzembe fulani?!.
3. Baadae Lulu akaufungua mlango na kutoka kama alivyozaliwa na kumweleza huyo kijana Kanumba ameanguka hiyo ilikuwa ni around saa 6 usiku, huyo kijana ulikwenda chumbani na kumkuta Kanumba kama alivyozaliwa anagalagala chini huku povu likimtoka mdomoni, what did he do first?.
4. Anasema alimpigia simu daktari wake!. Hivi kweli unaitwa chumbani na kumuona mtu ameanguka anavuja damu anatapatapa, wewe utamtafuta kwanza daktari wake au kazi ya kwanza ni kumkimbiza mgonjwa hospitali ya karibu?. Pale kwa Kanumba mpaka hospitali ya Sinza Palestina ambayo ni 24/7 ni only 5 minites away!. Tukio limetokea saa 6 usiku mwili wapelekwa Muhimbili 11 alfajiri!. Kulitokea nini hapo?!. Hapo sio uzembe fulani huu?!.
5. Hivi ni kweli Kanumba alikuwa na daktari wake?. Jee alikuwa ana suffering something kiasi kwamba kuna daktari maalum ndio huwa anamhudumia hali iliyolazimisha lazima atafutwe huko aliko ndipo Kanumba apate huduma ya kwanza!. Kama tukio ni saa 6, daktari alipigiwa simu saa ngapi?, na alifika saa ngapi?, kumbukeni muda wote huo Kanumba anagalagala na kuvuja damu nyingi kumsubiria daktari wake afike?!. Huu sio uzembe fulani?.
6. Tunaelezwa daktari alipofika ndipo juhudi za kumkimbiza Muhimbili zikafuatia, huku kukipatikana tarifa za baadhi ya wasanii kufika hapo kwa Kanumba within minutes na wengine kukiri walimkuta mwili umeshaanza kuwa baridi, muda gani ulishapita toka tukio mpaka hao wasanii/majirani waliofika mwanzo and what did they do?!. Hapa kweli hakuna uzembe fulani?.
7. Tumeonyeshwa picha na TBC zikionyesha umati mkubwa wa wasanii ukiandamana kuupeleka mwili Muhimbili, ikumbukwe wakati tukio alikuwa kama alivyozaliwa ila mwili ulionekana umevishwa, hivyo emergence ya aina ile mgonjwa huwa anafunikwa tuu shuka na kuwahishwa hospitali, kupatikana muda mpaka kumvisha huu sio uzembe fulani?!.
8. Kama tukio ni la dharura tulitegemea watu wa kwanza ni majirani iweje wasanii wajazane kivile usiku huo mpaka na waandishi wa TBC?. Haiwezekani baada ya kutokea ajali hiyo ya kuanguka, badala ya kumpatia mgonjwa huduma ya kwanza ya kujaribu kuokoa maisha ya Kanumba, watu walikuwa bize kuwatafuta masuper star na waandishi wawahi tukio lile huku wengine wakiendelea kuhangaikia kuupiga picha mwili wa Kanumba licha ya kujua tayari ni dead body?!.
9. Kama hao waliofika wakanshika na kuona mwili umeanza baridi, ni muda gani daktari alifika?. Ni muda gani walijua Kanumba ameshafariki?, kama alifia nyumbani hawakujua hiyo sasa at that poit ni police case badala ya kuitana makundi ya wasanii na kuidramatise scene ya kifo cha Kanumba?!.
10. Mwisho kwa sababu ripoti ya daktari kutaja chanzo cha kifo haijatoka, naombeni tusimbebeshe mtoto Lulu msalaba wa kifo cha Kanumba!. Inawezekana ni Kanumba mwenyewe aliteleza, na hata kama ni kweli alimsukuma, kama alimsukuma in self defence, Lulu hana hatia yoyote kwa sababu kifo kitakuwa kimetokea kwa bahati mbaya bila kusudio la kutenda jinai ya mauaji!.
RIP SK The Great
Pasco.