Kifo cha kweli cha Adolph Hitler: Hebu tuachane kwanza na ile ya kujiua kwa tindikali au kukimbilia kwake Argentina

Matendo yake yanashahabiana na unachowaza.
 
Hii itikadi kali sana haifai duniani
 
Jama alikua katili sana si kawaida
 

Hongera sana DA' VINCI XV kwa kufanya utafiti kuhusu taarifa za huyu Mwendawazimu wa karne ya Ishirini Adolf Hitler.

Kutokana na taarifa hizi za karibuni hii inathibitisha utafiti wa Prof. Hugh Trevor Roper Mwanahistoria aliyezuru Ujerumani mapema baada ya vita vya pili vya dunia na kukusanya ndondoo kuhusu siku za mwisho za maisha ya hitler! jamaa alilalamika sana kwamba Mwisho wa Siku za Uhai wa Hitler ziligubikwa na mafumbo na uzushi mwingi sana .

Sababu kuu aliyoitoa ni kwa sababu walio ikomboa berlin hawakuwa Waingereza,Wafaransa wala Wamarekani bali walikuwa Warusi - hawa ndio waliotengeneza mazingira magumu ya ukweli wa Hitler alikufa pale pale ngomeni au alitoroka na kukimbilia Amerika ya Kusini.

Trevor Roper anadai kwamba Mara General George Zukhov aliyeyaongoza majeshi ya Wajamaa (Red Army),kuivamia na kuikomboa Berlin aliruhusu Uhuru uliopitiliza wa utoaji taarifa kumhusu Hitler ( George alitaka watu wajue hitler hakuwa jambo la maana sana na amekufa kama watu wengine tu).

Rias Stalin alipoendelea kusoma kwenye Gazeti maarufu la Urusi kuhusu habari za Mstari wa Mbele Vitani "Pravda" na kupewa taarifa za Siri kutoka kwa Maafisa wake Ghafla aliagiza George Zukhov arudi Moscow haraka, anakapelekwa Kamanda mwingine ambaye aliminya utoaji wa Taarifa kwa makusudi,kutokana na maagizo aliyopewa na Stalin.

Hii ilifanywa makusudi na Stalin kwa sababu zake binafsi - alishaingia hofu kubwa kuwa aliyewaunganisha wajamaa na Mabeberu ameshakufa - Uhasama unaweza kurudi kwa kasi ya Vifurushi vipya vya TCRA,ilikupata muda wa kujipanga aliamua kuendeleza uzushi wa kuwa hitler yupo hai.

Lakini tayari Hugh Tervor roper alishakusanya taarifa za kutosha na kuhitimisha kuwa ADOLF HITLER Alijipa risasi na kufa papo hapo na Mkewe EVA BRAUN alijiuwa kwa kunywa sumu aina ya Cyanide kwa hiyari yake.

Ni maagizo ya Hitler Mwenyewe kuwa miili yao ichomwe iwe jivu,Inasemekana kuwa Red Army wangechelewa kidogo labda wangekuta jivu tupu.

Asante.
 
Pia kuna taarifa alikuwa na Korodani moja huyu mwamba ni kweli??
 
Shukraani mkuu
Tumeongeza kitu
 
Pia kuna taarifa alikuwa na Korodani moja huyu mwamba ni kweli??
Sina uhakika mkuu ila niseme tu kama korodani moja inaweza athiri mtu asiweze Kuzaa basi inawezekana huenda ikawa kweli huyu mwamba alikuwa na kende moja maana Hitler mpaka umri wa miaka 56 hakuwahi kuwa na mtoto.sijajua pengine nini kilisababisha awe na kende moja ila huyu bwana aliwahi kuwa mwanajeshi na alipigana vita ya kwanza ya dunia na inasemekana aliwahi kujeruhiwa huko vitani ikiwa pamoja na kupofushwa na gesi ya sumu maana vita ya kwanza ya dunia ilikuwa ni vita ya kwenye mahandaki na yenye kutumia gas za sumu hivyo huyu bwana aliwahi athiriwa na hiyo gesi ya sumu.
 
Huwa sielewi kabisa. Mtu anayeua mpaka watoto anakuinspire vipi? Imagine katoto kako ka kike na ww na mkeo mmepanga mstari mkiwa watupu mnasubiri risasi kwa amri ya anayekuinspire. He was a fool with military powers.
he was a poor boy who claim greater power,ananiispire kama kijana mpambanaji na siyo muuwaji
 
Unamkubali sababu ya uuaji wake??[emoji44][emoji44][emoji44]
Nje na kuua kimsingi jamaa ukisikiliza hotuba zake alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuhamasisha (Convincing power) mpaka watu wanapata morali ya kufanya jambo kitu ambacho si rahisi.

Nilimtazama akiwa anahutubia katika kiwanda cha krupp hotuba iliyopewa jina la Reoccupation of the Rhineland kimsingi hata Mimi nilimkubali mbali na kumtazama kama muuaji.
 
Speech zake wajerumani walikuwa wanazielewa sana alipendwa sana na wajerumani wakati anaomba kuchaguliwa kuwa chansela wanasema alikuwa na charisma.Ila alipokamata tu dola ndio wakamjua ni adolf hitler ni nani
 
Aisee shukraani mkuu

watu
kama kina Hugh Tervor wamepambana kutufunulia kuja tusiyoyajua
 
sawa sawa mkuu shukraani
 
sawa sawa mkuu shukranii uwepo wako umekuwa muhimu sana hapa🙏
 
Jamaa alikuwa mtalaamu wa kuongea sana
Speech zake wajerumani walikuwa wanazielewa sana alipendwa sana na wajerumani wakati anaomba kuchaguliwa kuwa chansela wanasema alikuwa na charisma.Ila alipokamata tu dola ndio wakamjua ni adolf hitler ni nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…