Kifo cha kweli cha Adolph Hitler: Hebu tuachane kwanza na ile ya kujiua kwa tindikali au kukimbilia kwake Argentina

Kifo cha kweli cha Adolph Hitler: Hebu tuachane kwanza na ile ya kujiua kwa tindikali au kukimbilia kwake Argentina

Nakazia hapo "he was a fool with military powers" halafu inawezekana alikuwa na matatizo ya kisaikolojia imagine Hitler alikufa na 56 years hakuwa haya na mtoto.Kuna fununu kuwa inawezekana jogoo lilikuwa halipandi mtungi.Ujue watu wa namba hii huwa wanakuwa na inferiority complex
Matendo yake yanashahabiana na unachowaza.
 
Hitler naamini alijiua kwenye fuhrer bunker.Hii ni sehemu ambayo ilikuwa chini ya ardhi.Wakati anakaribia kupoteza kwenye vita ya pili ya dunia alikuwa anajificha kwenye hii sehemu yeye na wasaidizi wake kama kina herman goring na yule aliyekuwa waziri wake wa propaganda za kiNazi joseph gobbles.

Katika kitabu chake kinachoitwa Mein Kempf hitler anatueleza alivyokuwa anafikiria kujiua baada ya mapinduzi yake ya kuchukua nchi kufeli mwaka 1923 na alifungwa jela,alipokuwa jela alikuwa na mawazo ya kujiua,mapinduzi haya yalikuwa yanaitwa beer hall pusch.

Kwa kutaka kule kujiua alipokuwa jela kunaonesha kabisa ni mtu ambaye kujiua kwake ni jambo la suluhu pale mambo yanapo muendea mrama.Hivyo kuna uwezekano alipoona ujerumani inapoteza vita ya pili ya dunia akaona ajitoe roho.

Miongoni mwa wasaidizi wake ambao pia walijiua ni Heinrich Himmler(Mkuu wa jeshi la schutzstaffel),Herman Goring(Reich marshal) na joseph goebbels(waziri wa propaganda)

Kuna siku nitakuja na mada inayowaelezea hawa waliokuwa wanaitwa schutzstaffel kwa kifupi SS ambao kofia zao zilikuwa zina alama ya fuvu la kichwa kuashiria ni watu wa kifo.Hakujawahi kutokea wauaji hapa duniani kama hawa jamaa.Ile idadi ya wayahudi milioni 6 waliouwawa wakati wa Hitler hawa jamaa wanaoitwa ss ndio walikuwa wanahusika.
View attachment 1735324
Huyu pichani anaitwa Himmler ndio alikuwa mkuu wa vikosi vya schutzstaffel nchi nzima.Huyu ndio alikuwa mtekelezaji mkuu wa mauaji ya wayahudi

Nadhani wayahudi walipokuwa wanaona mtu mwenye nguo kama za huyu hapa chini wakati ule wa utawala wa Hitler basi wayahudi walikuwa wanakiona kifo kipo karibu yao
View attachment 1735633
Hii itikadi kali sana haifai duniani
 
Sobibor yenyewe ilikuwa Poland,kulikuwa Luna kambi za aina hii
Concentration camp(Dachau,Buchenwald)
Death camp(Sobibor,Belzec,Auschwitz)
Labour camp(Mauthausen,flossenburg)
POW(Prisoner of War Camp) nimezisahau

Ingawa walizicategorised kwa namna hii lakini kwenye kila aina ya kambi hizi kulikuwa na mateso,ukatili,vifo na kazi ngumu.Hizi death camp zilikuwa zinaitwa death camp kwa kuwa kulikuwa na vyumba maalumu kwa ajili ya kuuwa watu wengi kwa wakati mmoja kwa kutumia gas sumu mfano Zyklon B imetumika sana Auschwitz kuua watu na inasemekana ni death camp iliyoua watu wengi zaidi kuliko nyingine
Jama alikua katili sana si kawaida
 
Wasalaam,

Kumekuwa na Hadithi nyingi sana Kumuhusu diktekta maarufu , mwamba wa Ujerumani Adolph Hitler, katika hatma yake Wengine wakidai alichomoka kwenda kwa wafadhili wake wa Argentina kustirika Aibu ya kushindwa Vita, wengine Wakadai alijitumbukiza kwenye Tindikali Eti baadala ya Mabaki ya nguo zake kukutwa pembeni ya Tindikali nadharia hiyo hata mimi miaka ile nakua ilikaa kwenye Ubongo wangu, wengine wakasema Diktekta huyo alikufa kwa kushambuliwa na Mbu yule mdudu wa Malaria ,habari zipo nyingi nyingi.

View attachment 1735002

Katika utafiti wa wanasayansi wa Ufaransa walichambua vipande vya meno ya Adolf Hitler ili kudhibitisha kuwa alikufa mwaka 1945, baada ya kujipatia sumu (cyanide) na kujipiga risasi kichwani. Utafiti huo, uliochapishwa katika Jarida la ulaya la Internal Medicine, Mei 2018, hii ilimaliza kabisa nadharia nyingi juu ya kifo cha Adolf Hitler kupitia uchambuzi wa kisayansi wa meno na fuvu la dikteta Huyo.

"Utafiti wetu unathibitisha kwamba Hitler alikufa mwaka 1945,"

mwandishi mkuu wa utafiti huo Philippe Charlier aliiambia AFP.

"Ni Meno halisi ya Hitler na hakuna shaka"

View attachment 1735003
PHILLIPE CHARLIER

Ingawa imejulikana hivyo kwamba Hitler alikufa katika jumba lake la Utawala pale Berlin, lakini uvumi wa kutoroka na kukimbia ni mwingi sana.
Utafiti wao unathibitisha kwamba hakufanikiwa kukimbia

"hakukimbilia Argentina kwa manowari, wala hakwenda katika kituo kilichofichwa "

Alisema Charlier

Inaelezwa Mwishoni mwa Aprili 1945, wakati vikosi vya Soviet vilipovamia Berlin, .
Hitler alifanya mipango ya kujiua hii ni baada ya kuagiza vidonge vya Sumu kabla hajaacha wosia wa mwisho.
Siku mbili kabla , Mussolini alikuwa amepigwa risasi na kikosi cha warusha risasi na kisha kunyongwa hadharani ,katika uwanja huko Milan Italia.
Hatima kama hiyo ilionesha hiltler hakutaka imtokee akachukua maamuzi kama hayo. Akajiua.

Aprili 30, miili ya Hitler na mkewe Eva Braun, ilipatikana ndani ya jumba hilo, huku ikiwa na shimo la risasi

View attachment 1735004

Aprili 2018, Chapisho la Kiingereza la kumbukumbu za mkalimani wa Urusi ilidokeza jinsi alivyokabidhiwa meno kadhaa mnamo 1945, na akapewa jukumu la kulinda rekodi zote kuanzia meno, na habari za dikteta za na vyote vinavyomuhusu vilibaki mikononi mwa Urusi

Baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa, Secret service ,Ya Urusi ,FSB na serikali ya Urusi ziliwapa watafiti ruhusa ya kuchunguza kipande cha fuvu na vipande vya meno yake. Kipande cha fuvu kilikuwa na shimo upande wake wa kushoto, sawa na jeraha la risasi,
Ingawa wanasayansi hawakuruhusiwa kuchukua sampuli kutoka kwenye fuvu hilo, walibaini katika utafiti huo, muonekano wa sura ya fuvu hilo ilionekana kufanana kabisa na picha za fuvu la kichwa la Hitler lililochukuliwa mwaka mmoja kabla ya kifo chake.

View attachment 1735009

Picha za meno zilizochapishwa katika utafiti huo zinaonyesha taya iliyotengenezwa na meno chuma. na inaelezwa Wakati wa kifo chake waliandika katika ripoti kuwa Hitler alikuwa na meno manne tu yaliyosalia.katika kinywa chake.

View attachment 1735005

Uchambuzi huo ulithibitisha madai yaliyotajwa hapo, lakini hawakuweza kuthibitisha kabisa kama hitler alichukua sumu (cyanide) kabla ya kujipiga risasi. Lakini mabaki ya rangi ya Ubluu kwenye meno yake fake(metal), watafiti waliandika, inawezekana chemical Reaction ilifanyika katika meno yake bandia na sumu hiyo wakati wa kifo

Swali mabaki mengine yalizikwa AU???

"Bila kuchukua sampuli kwa uchambuzi, ni ngumu kusema kwa uhakika"

"Hatukujua ikiwa alikuwa ametumia Sumu ya (cyanide) kujiua au ikiwa ni risasi kichwa, ila kuna uwezekano wa vyote kufanyika "

Charlier alisema.

View attachment 1735007

Kwa vyovyote vile, utafiti unaweza kusaidia hatimaye kuweka kando stori za kukimbia kwa hitler Argentina kupumzika Vurumai la Vita, na habari zingine zingine juu ya kifo chake.

DA'VINCI XV

Hongera sana DA' VINCI XV kwa kufanya utafiti kuhusu taarifa za huyu Mwendawazimu wa karne ya Ishirini Adolf Hitler.

Kutokana na taarifa hizi za karibuni hii inathibitisha utafiti wa Prof. Hugh Trevor Roper Mwanahistoria aliyezuru Ujerumani mapema baada ya vita vya pili vya dunia na kukusanya ndondoo kuhusu siku za mwisho za maisha ya hitler! jamaa alilalamika sana kwamba Mwisho wa Siku za Uhai wa Hitler ziligubikwa na mafumbo na uzushi mwingi sana .

Sababu kuu aliyoitoa ni kwa sababu walio ikomboa berlin hawakuwa Waingereza,Wafaransa wala Wamarekani bali walikuwa Warusi - hawa ndio waliotengeneza mazingira magumu ya ukweli wa Hitler alikufa pale pale ngomeni au alitoroka na kukimbilia Amerika ya Kusini.

Trevor Roper anadai kwamba Mara General George Zukhov aliyeyaongoza majeshi ya Wajamaa (Red Army),kuivamia na kuikomboa Berlin aliruhusu Uhuru uliopitiliza wa utoaji taarifa kumhusu Hitler ( George alitaka watu wajue hitler hakuwa jambo la maana sana na amekufa kama watu wengine tu).

Rias Stalin alipoendelea kusoma kwenye Gazeti maarufu la Urusi kuhusu habari za Mstari wa Mbele Vitani "Pravda" na kupewa taarifa za Siri kutoka kwa Maafisa wake Ghafla aliagiza George Zukhov arudi Moscow haraka, anakapelekwa Kamanda mwingine ambaye aliminya utoaji wa Taarifa kwa makusudi,kutokana na maagizo aliyopewa na Stalin.

Hii ilifanywa makusudi na Stalin kwa sababu zake binafsi - alishaingia hofu kubwa kuwa aliyewaunganisha wajamaa na Mabeberu ameshakufa - Uhasama unaweza kurudi kwa kasi ya Vifurushi vipya vya TCRA,ilikupata muda wa kujipanga aliamua kuendeleza uzushi wa kuwa hitler yupo hai.

Lakini tayari Hugh Tervor roper alishakusanya taarifa za kutosha na kuhitimisha kuwa ADOLF HITLER Alijipa risasi na kufa papo hapo na Mkewe EVA BRAUN alijiuwa kwa kunywa sumu aina ya Cyanide kwa hiyari yake.

Ni maagizo ya Hitler Mwenyewe kuwa miili yao ichomwe iwe jivu,Inasemekana kuwa Red Army wangechelewa kidogo labda wangekuta jivu tupu.

Asante.
 
Nakazia hapo "he was a fool with military powers" halafu inawezekana alikuwa na matatizo ya kisaikolojia imagine Hitler alikufa na 56 years hakuwa haya na mtoto.Kuna fununu kuwa inawezekana jogoo lilikuwa halipandi mtungi.Ujue watu wa namba hii huwa wanakuwa na inferiority complex
Pia kuna taarifa alikuwa na Korodani moja huyu mwamba ni kweli??
 
Baada ya ujerumani kuona dalili za kushindwa vita ya pili ya dunia iko dhahiri walijua kitakachofuata ni kukamatwa na majeshi ya ushirikiano(Allies) ambayo yalikuwa ni majeshi ya nchi ya nchi tatu Great Britain,Russia,na United States).Wajerumani walijua watakapotiwa mikononi na haya majeshi watakuwa na hali ngumu ukizingatiwa walikuwa wamefanya uhalifu mbaya dhidi ya binadamu,walijua kabisa kitakachofuata ni kushtakiwa.Baadhi ya viongozi wa SS walianza kutoroka huku wakimsaliti Hitler, mmoja wao akiwa ni huyo Heinrich Himmler ambaye alikuwa ameamua kutoroka akisafiri kwa kutumia fake documents lakini alikamatwa na majeshi ya allies.

Hitler nae baada ya kuona allies wanaingia Berlin ndipo yeye na baadhi ya wasaidizi wake wakaamua kujiua kwenye fuhrer bunker.Hii fuhrer bunker ni andaki ambalo alikuwa analitumia hitler kujikinga na mashambulizi ya anga.Hivyo hitler na baadhi ya wasaidizi wake akiwemo joseph goebbels (Waziri wa Propaganda)walijiua huko kwenye handaki.

Neno fuhrer kwa kijerumani maana yake ni kiongozi ni neno ambalo lilikuwa linatumiwa kumaanisha kiongozi wa ujerumani(Third Reich)ambaye ni Hitler kama North Korea wanavyotumia Supreme Leader kumaanisha ni Kim Jong un.

Viongozi wengi wa serikali ya Hitler walikuwa ni wanachama wa SS.Hii ilikuwa ni organization kubwa na imegawanyika katika nyanja mbalimbali mfano SS ilikuwa na vitengo kama vya intelligence,Administration ya Death Camps na Concentration Camps,vikosi vya vita vya SS(Waffen SS) kwa kifupi SS ilikuwa ni Organization kubwa ya Nazi Party.

Hawa waliokuwa wanaendesha hizi death camps na concentration camps walikuwa ni kutoka kitengo kinachoitwa Death Head Unit(Totenkopfverbande) ambao walifundishwa kuwa watu katili mno na kuwachukia wayahudi walikuwa ni watu wasio na huruma hata kidogo na binadamu anayeitwa jew(Myahudi).

Kuna vitengo vilikuwa vinaratibu kabisa usafiri wa treni wa kuwasafirisha wayahudi kwenda kuuwawa kwenye death camps.Wayahudi wakishazingirwa wanapelekwa kwenye vituo maalumu wanapakiwa kwa kujazwa kwenye treni za mizigo na kupelekwa kuuwawa na death camps watoto,wazee,wanawake kwa wanaume.

Baada ya Allies kuiteka ujerumani baadhi ya viongozi wa serikali ya Hitler walikamatwa ikiwa ni pamoja na Heinrich Himmler (mkuu wa SS) na Herman Goering (supreme commander of the Luftwaffe).

Luftwaffe maana yake ni jeshi la anga la ujerumani wakati wa Hitler.
Baada ya wahalifu hawa kukamatwa walifunguliwa mashtaka kwenye mahakama iliyoundwa na nchi tatu uingereza,marekani na urusi na mashtaka haya yalijulikana kwa jina la Nuremberg trial pengine inawezekana mahakama hii ilikuwa kwenye mji wa Nuremberg huko ujerumani.Hukumu mbalimbali zilitolewa kufuatana na uzito wa makosa.Wengine walihukumiwa kunyongwa na wengine vifungo na wasio na hatia bila shaka waliachwa huru.SS organisation ilitangazwa kuwa ni criminal organization na ilipigwa marufuku na mahakama.Chama cha Nazi cha Adolf Hitler nacho kilitangazwa kuwa ni criminal organization na kikapigwa marufuku hata organization mbalimbali kwenye utawala wa Hitler zilipigwa marufuku wakiwemo Gestapo(Secret Police)

Nazi party ni chama cha Adolf Hitler ambacho kilichukua nchi kuanzia mwaka 1933 - 1945 na mara kiliposhika nchi ndipo mateso kwa wayahudi na hata wajerumani yalipoanza.Kirefu cha Nazi ni Nationalsozialistische Deutsche Arbeiterpartei.Hivyo mahakama ilikipiga marufuku chama hiki na kukitangaza kuwa ni criminal organization.

Viongozi wakubwa wawili ambao walikwepa kunyongwa ni Heinrich Himmler na Herman Goering.Hawa walijiua wakiwa rumande kabla hata adhabu zao hazijatekelezwa.Na chanzo cha vifo vyao ni sumu aina ya cyanide ambayo mpaka leo inashindwa kueleweka waliipata wapi wakati walikuwa rumande.

Hizi na baadhi ya picha za SS(Schutzstaffel) kutoka division ya totenkopfvernande(Death Head Division ambao ndio walikuwa na kazi ya kuendesha death camps na concentration camps zilizokuwa zinaua sana wayahudi na watu wengine.Kwenye kofia zao kuna alama ya fuvu linaloashiria kifo.
View attachment 1741946

View attachment 1741947
Shukraani mkuu
Tumeongeza kitu
 
Pia kuna taarifa alikuwa na Korodani moja huyu mwamba ni kweli??
Sina uhakika mkuu ila niseme tu kama korodani moja inaweza athiri mtu asiweze Kuzaa basi inawezekana huenda ikawa kweli huyu mwamba alikuwa na kende moja maana Hitler mpaka umri wa miaka 56 hakuwahi kuwa na mtoto.sijajua pengine nini kilisababisha awe na kende moja ila huyu bwana aliwahi kuwa mwanajeshi na alipigana vita ya kwanza ya dunia na inasemekana aliwahi kujeruhiwa huko vitani ikiwa pamoja na kupofushwa na gesi ya sumu maana vita ya kwanza ya dunia ilikuwa ni vita ya kwenye mahandaki na yenye kutumia gas za sumu hivyo huyu bwana aliwahi athiriwa na hiyo gesi ya sumu.
 
Huwa sielewi kabisa. Mtu anayeua mpaka watoto anakuinspire vipi? Imagine katoto kako ka kike na ww na mkeo mmepanga mstari mkiwa watupu mnasubiri risasi kwa amri ya anayekuinspire. He was a fool with military powers.
he was a poor boy who claim greater power,ananiispire kama kijana mpambanaji na siyo muuwaji
 
Unamkubali sababu ya uuaji wake??[emoji44][emoji44][emoji44]
Nje na kuua kimsingi jamaa ukisikiliza hotuba zake alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuhamasisha (Convincing power) mpaka watu wanapata morali ya kufanya jambo kitu ambacho si rahisi.

Nilimtazama akiwa anahutubia katika kiwanda cha krupp hotuba iliyopewa jina la Reoccupation of the Rhineland kimsingi hata Mimi nilimkubali mbali na kumtazama kama muuaji.
 
Speech zake wajerumani walikuwa wanazielewa sana alipendwa sana na wajerumani wakati anaomba kuchaguliwa kuwa chansela wanasema alikuwa na charisma.Ila alipokamata tu dola ndio wakamjua ni adolf hitler ni nani
 
Hongera sana DA' VINCI XV kwa kufanya utafiti kuhusu taarifa za huyu Mwendawazimu wa karne ya Ishirini Adolf Hitler.

Kutokana na taarifa hizi za karibuni hii inathibitisha utafiti wa Prof. Hugh Trevor Roper Mwanahistoria aliyezuru Ujerumani mapema baada ya vita vya pili vya dunia na kukusanya ndondoo kuhusu siku za mwisho za maisha ya hitler! jamaa alilalamika sana kwamba Mwisho wa Siku za Uhai wa Hitler ziligubikwa na mafumbo na uzushi mwingi sana .

Sababu kuu aliyoitoa ni kwa sababu walio ikomboa berlin hawakuwa Waingereza,Wafaransa wala Wamarekani bali walikuwa Warusi - hawa ndio waliotengeneza mazingira magumu ya ukweli wa Hitler alikufa pale pale ngomeni au alitoroka na kukimbilia Amerika ya Kusini.

Trevor Roper anadai kwamba Mara General George Zukhov aliyeyaongoza majeshi ya Wajamaa (Red Army),kuivamia na kuikomboa Berlin aliruhusu Uhuru uliopitiliza wa utoaji taarifa kumhusu Hitler ( George alitaka watu wajue hitler hakuwa jambo la maana sana na amekufa kama watu wengine tu).

Rias Stalin alipoendelea kusoma kwenye Gazeti maarufu la Urusi kuhusu habari za Mstari wa Mbele Vitani "Pravda" na kupewa taarifa za Siri kutoka kwa Maafisa wake Ghafla aliagiza George Zukhov arudi Moscow haraka, anakapelekwa Kamanda mwingine ambaye aliminya utoaji wa Taarifa kwa makusudi,kutokana na maagizo aliyopewa na Stalin.

Hii ilifanywa makusudi na Stalin kwa sababu zake binafsi - alishaingia hofu kubwa kuwa aliyewaunganisha wajamaa na Mabeberu ameshakufa - Uhasama unaweza kurudi kwa kasi ya Vifurushi vipya vya TCRA,ilikupata muda wa kujipanga aliamua kuendeleza uzushi wa kuwa hitler yupo hai.

Lakini tayari Hugh Tervor roper alishakusanya taarifa za kutosha na kuhitimisha kuwa ADOLF HITLER Alijipa risasi na kufa papo hapo na Mkewe EVA BRAUN alijiuwa kwa kunywa sumu aina ya Cyanide kwa hiyari yake.

Ni maagizo ya Hitler Mwenyewe kuwa miili yao ichomwe iwe jivu,Inasemekana kuwa Red Army wangechelewa kidogo labda wangekuta jivu tupu.

Asante.
Aisee shukraani mkuu

watu
kama kina Hugh Tervor wamepambana kutufunulia kuja tusiyoyajua
 
sawa sawa mkuu shukraani
Sina uhakika mkuu ila niseme tu kama korodani moja inaweza athiri mtu asiweze Kuzaa basi inawezekana huenda ikawa kweli huyu mwamba alikuwa na kende moja maana Hitler mpaka umri wa miaka 56 hakuwahi kuwa na mtoto.sijajua pengine nini kilisababisha awe na kende moja ila huyu bwana aliwahi kuwa mwanajeshi na alipigana vita ya kwanza ya dunia na inasemekana aliwahi kujeruhiwa huko vitani ikiwa pamoja na kupofushwa na gesi ya sumu maana vita ya kwanza ya dunia ilikuwa ni vita ya kwenye mahandaki na yenye kutumia gas za sumu hivyo huyu bwana aliwahi athiriwa na hiyo gesi ya sumu.
 
sawa sawa mkuu shukranii uwepo wako umekuwa muhimu sana hapa🙏
Sina uhakika mkuu ila niseme tu kama korodani moja inaweza athiri mtu asiweze Kuzaa basi inawezekana huenda ikawa kweli huyu mwamba alikuwa na kende moja maana Hitler mpaka umri wa miaka 56 hakuwahi kuwa na mtoto.sijajua pengine nini kilisababisha awe na kende moja ila huyu bwana aliwahi kuwa mwanajeshi na alipigana vita ya kwanza ya dunia na inasemekana aliwahi kujeruhiwa huko vitani ikiwa pamoja na kupofushwa na gesi ya sumu maana vita ya kwanza ya dunia ilikuwa ni vita ya kwenye mahandaki na yenye kutumia gas za sumu hivyo huyu bwana aliwahi athiriwa na hiyo gesi ya sumu.
 
Jamaa alikuwa mtalaamu wa kuongea sana

Back
Top Bottom