Kifo cha mashabiki wa WCB: Diamond anawafunza wasanii wenzake Public Relations

Kifo cha mashabiki wa WCB: Diamond anawafunza wasanii wenzake Public Relations

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau.

Najua wengi tumeona habari za ajali ya vijana wawili ambao ni mashabiki tu wa WCB >> Tanzia: Team Diamond, Nevvo Msafi na Platnumzmond wafariki dunia

Imekuwa huzuni mitandaoni, msiba mkubwaaa kama amefariki mfanyakazi wa Diamond, kumbe ni mashabiki tu!

Msibani wameenda kina Queen Darleen na wengineo wengi hadi mama Diamond nae... Hii inaonesha kuheshimu mashabiki wao na hata vijana wengine wanaomshabikia Diamond wanapata nguvu zaidi kuonesha WCB ina upendo..

Msiba umemkuta Diamond nje ya nchi ila angekuwa Bongo angeenda pia na wanamsifia amechangia kidogo alichonacho kusapoti mazishi ya mashabiki wake..

Je, kina Juma Nature walikuwa wanajua hata majina ya mashabiki wao? Je, kina Lady Jaydee pia enzi wanatamba walikuwa wanaheshimu mashabiki wao?

Nakumbuka enzi za ujana niliendaga nunua T-shirt za East Coast Team pale Upanga .. Majibu niliyopewa eti hawauziii t-shirt madogo... ha ha ha imagine msanii anamkataa shabiki wake kisa ni dogo!

Kwa hizi mbinu za Diamond, WCB itawanyoosha sana wasanii wasiojua biashara inahitaji mbinu gani..

Mwarabu Fighter ni mlinzi tu lakini anaheshimiwa WCB na bosi wake kuliko hata mwalimu anavyoheshimiwa na Mkurugenzi ambaye ndie bosi wake.
 
Nashukuru nimepata mtu asiyependa hivi vineno vya kuji-humble kinafki...

"Tugawane umasikini" etc.
Vinanichefua sana

Kama unamilion weka mezani sio Mara nini Mara nn

Ni kujiendekezea umaskini tu
 
Ni public relations au ubinadamu tu?
Ndio ni public relation on how to create reputation, creadibility and image promotional, disseminate organisation brand ni pamoja na kushiriki community issues........
 
Msanii bila mashabiki hawezi fika mbali,Wcb inatambua mchango wa mashabiki wao ndio mana wamejitolea na kuonesha umma kua jeuri wanazopata zinatoka kwetu wenyewe.hongeren sana wcb kwakutambua mchango wa mashabiki zao
 
Ndio ni public relation on how to create reputation, creadibility and image promotional, disseminate organisation brand ni pamoja na kushiriki community issues........
Kwa utamaduni wetu kuleta public relations stunts kwenye msiba ni kashfa.

Msiba ni msiba tu. Hauna sehemu ya public relations. Ukileta public relations kwenye msiba utaambiwa mwanga unatangaza biashara yako kwenye msiba wa wenzio.

Utapewa marehemu uwale nyama. Kwa wanaoelewa utamaduni wetu wataelewa. Ila kama hujui habari hizi unatumia mtumba mpaka utamaduni, huwezi kuelewa.

Msiba wa mtu si sehemu ya kwenda kupandisha brand kwa public relations stunts. Public relations stunts za kupaisha jina kwenye misiba ndiyo mwanzo wa kuambiwa Diamond ni freemason anatoa mashabiki kafara ili kusafisha nyota yake na kupaisha brand kwenye misiba na upuuzi kama huo.

Msiba ni sehemu ya kutoa rambirambi kibinadamu, si public relations stunts za kupaisha brand.
 
Kwa utamaduni wetu kuleta public relations stunts kwenye msiba ni kashfa.

Msiba ni msiba tu. Hauna sehemu ya public relations.

Ukileta public relations kwenye msiba utaambiwa mwanga unatangaza biashara tako kwenye msiba wa wenzio.

Utaoewa marehemu uwale nyama.

Kwa wanaoelewa utamaduni wetu wataelewa.

Ila kama hujui habari hizi unatumia mtumba mpaka utamaduni, huwezi kuelewa.

Msiba wa mtu si sehemu ya kwenda kupandisha brand kwa public relations stunts.

Public relations stunts za kupaisha jina kwenye misiba ndiyo mwanzo wa kuambiwa Diamond ni freemason anatoa mashabiki kafara ili kusafisha nyota yake na kupaisha brand kwenye misiba na upuuzi kama huo.

Msiba ni sehemu ya kutoa rambirambi kibinadamu, si public relations stunts za kupaisha brand.
Mekuelewa mkuu, hujakataa lkn umezingatia sana utu ni sawa.......!!!!
 
Kwa utamaduni wetu kuleta public relations stunts kwenye msiba ni kashfa.

Msiba ni msiba tu. Hauna sehemu ya public relations.

Ukileta public relations kwenye msiba utaambiwa mwanga unatangaza biashara yako kwenye msiba wa wenzio.

Utapewa marehemu uwale nyama.

Kwa wanaoelewa utamaduni wetu wataelewa.

Ila kama hujui habari hizi unatumia mtumba mpaka utamaduni, huwezi kuelewa.

Msiba wa mtu si sehemu ya kwenda kupandisha brand kwa public relations stunts.

Public relations stunts za kupaisha jina kwenye misiba ndiyo mwanzo wa kuambiwa Diamond ni freemason anatoa mashabiki kafara ili kusafisha nyota yake na kupaisha brand kwenye misiba na upuuzi kama huo.

Msiba ni sehemu ya kutoa rambirambi kibinadamu, si public relations stunts za kupaisha brand.
We jamaa kwa battle upo vizuri.
 
Back
Top Bottom