Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,583
Naeleza tu baada ya kufikiri mambo kwa kina.We jamaa kwa battle upo vizuri.
Kwa mwendo huu wa kufanya misiba sehemu ya "public relations for brand promotion" watu wataanza kusaini mikataba.
Mtu atasema, msiba wangu udhaminiwe na kampuni ya bia, nikifariki kampuni ya bia iilipe familiayangu, lakini kwenye msiba pote kuwe na matangazo ya kampuni ya bia.
You "monetize" your own death and funeral!
Na kidau kikiwa kikubwa sana, na familia yangu ina matatizo sana, nawahi kujiua tu ili mradi najua kampuni ya bia itailipa hela nzuri familia yangu, katika juhudi nzima za kufanya misiba iwe sehemu ya brand promotion.
A very sick predicament.
Ndiyo maana nasema kama wameenda kutoa rambirambi on humanitarian grounds,kwa mapenzi kwa mashabiki tu, kwa uchungu kwamba mashabiki wamefariki, hilo ni jambo zuri la kuigwa.
Lakini kama wameenda kwa public relations reasons kukuza brand, waandikwe, jina lipae, wameufanya msiba sehemu ya kujitangaza kibiashara, ni jambo baya sana.