Lameck Masanja
Senior Member
- Aug 5, 2011
- 153
- 238
Mambo ya Walawi, 11:45 inasema hivi, Kweli, ni mimi Bwana niliyewaondoa katika nchi ya Misri nipate kuwa Mungu wenu; basi ninyi mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.Hakuna binadamu anyeitwa mtakatifu huku ni kudanganyana,Mungu ameumba binadamu wa aina mbili,Mitume na binadamu wa kawaida,Mitume wamepewa uwezo au kalama tofautitofauti sisi tumeumbwa na mapungufu, hakuna binadamu aliyekamilika kila unayemuona anamapungufu kwa nini umuite Mtakatifu wewe ndiye uliyemuumba
Na Mtume Petro katika barua yake ya kwanza (1 Pet 1: 14-16) anakazia kwa kusema, "Muwe watoto watiifu. Msifuate tena tamaa zenu kama wakati mlipokuwa hamjui bado kitu. Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, hivyo yawapasa ninyi pia kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote. Kwa maana imeandikwa: "Muwe watakatifu kwa kuwa mimi nilivyo mtakatifu."
Sent using Jamii Forums mobile app