Kifo cha pesa Beach Kidimbwi

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2021
Posts
6,432
Reaction score
25,646
Jumapili fulani nilikuwa na rafiki yangu mmoja aliyepiga mshindo wa hela ya mahali tumepozi mtaani. Jamaa akaniambia yooh Satoh wacha tukatembee mahali mida ya jioni, nikamuuliza wapi anataka twende maana mimi ni mwenyeji hapa mjini, akajibu twenzetu kidimbwi.

Nilisita maana sikutegemea kabisa kama angechagua kwenda huko mahali ila nikaona it's ok wacha tu twende, kwanza napasikia tu sijawahi kufika kwa kweli. Jioni ikafika tukajiandaa kisha haoo uelekeo wa mikocheni, roundabout ya Clouds tukamimina boda la kule chini Kawe Beach, Times FM, Mbezi beach then punde Kidimbwi hii hapa..tukafika.

TuLIfika mida ya saa 11, ni pa kawaida tu kwa kweli tofauti na jinsi panavyokuzwa. Basi ikafika usiku pakawa ni sehemu tofauti kabisa na jinsi palivyokuwa jioni wakati tumefika..Palikuwa pamechangamka sana, mataa ya rangirangi na watoto wakali kibaoo.

Niseme Tu ukweli kuna Wanawake warembo, warembo sana. Muda wote shingo haitulii kwa kuangalia uumbaji wa MUNGU, watoto wakali hadi unajiuliza mbona kam kuna wadada walipendelewa siku wanaumbwa!! (Ukitaka kupata kipimo sahihi kama una demu mkali au umeingia cha kike basi nenda nae Kidimbwi, ingawa ili kuepuka aibu ndogondogo ni heri ukaenda mwenyewe tu maana anaweza kukuona malaya sana kwa jinsi utakavyopata shida kuibiaibia kutazama watoto wakali)

Basi bwana 'mwanangu' ndy bosi na mimi nilikuwa kama 'chawa' wake usiku ule. malaya shobo kibao tulipokaa, mwonekano wa kishua ukiwadanganya kumbe muhuni mfukoni balance niliyokuwa nayo ni pesa ya kuamkia mihogo kwa mama Amina na supu ya kongoro tu. Jamaa ndiyo alikuwa tagi ubavu, ingawa sinaga zile swags za kushobokea pesa za watu(masikini jeuri) ila nilikuwa mtulivu sn huku tukila vitu vyetu

Mida km ya saa 4 ndy Kwanza pakawa km show imeanza ,nikaona kitu kilichonishangaza Sana ambacho kilinipelekea kukodoa macho kwa kustaajabu.Kuna mdada amebeba sahani alafu ndani kuna chupa moja ya kinywaji,pembeni kuna wadada kama wanne hivi wanakatika na kucheza vizuri sana huku wanaelekea meza fulani ambayo ipo mbali kidogo na tulipo.

Nikamcheki dada wa karibu aliyekuwa ananizongazonga akidhani Mimi ni wa kishua kumbe apecha alolo nikamuuliza 'hey lady,hawa warembo nini hiki wanafanya'? Akanijibu yule dada aliyebeba ule 'mbapa' ni kinywaji cha milioni moja na nusu(1.5mil) na anapelekewa 'Mnene' mmoja hivi kipande kile..aloo..!! 1.5mil ni kinywaji tu si uharibifu wa hela huu!!? Umasikini mbaya sana asee!!!

Jirani yetu pale ambaye alionekana ni mzoefu wa hili chimbo akadakia "mjomba mbona hiyo ni ishu ya kawaida sn hapa".

Akaniambia unakiona kile chumba pale (huku akionyesha kidole), nikajibu yeah nakiona,akasema Mzee Baba pale kuingia sharti uwe na milioni 1.. Yaani Haijalishi utakaa dakika moja au saa zima,pale unaadikiwa deposit ya 1m kisha unaagiza unachotaka ktk menu zilizoorodheshwa utumie,Yani wewe Tu unatumiaje shauri yako!! Nikazidi kujiona masikini na kujidharau (kimoyomoyo nikasema milioni moja si napata kiwanja vikindu ndani ndani huko hapa inakatika dakika kadhaa Tu si ufala huu,huku namkumbuka Mzee wa kinywaji cha 1.5m ).

Haikupita muda, nawaona wadada wengine wanakatika viuno wakitembea na mwendo wa madaha huku wanasindikizwa na nyimbo za majigambo kutoka Kwa DJ wanaelekea meza nyingine.Nikapenyezewa taarifa kuna mwamba mwingine amefanya km jamaa wa mwanzo amepelekewa kinywaji cha 1m..Safari hii nilikuwa nimeshazoea,si unajua kushangaa mara moja tu.

Kuna kitu nilijifunza ule usiku;kwa watu waliofikia kilele cha Uhuru wa kifedha (financial freedom) kwao kutumia hela siyo yoyote bila kuuliza uliza wala kukagua wallet siyo tatizo kbs.Ule usiku nilijiapiza kutafuta pesa Kwa bidii zote.

Kwa hakika usiku ule nilishuhudia watu wakiteketeza pesa vibaya mno.Kwa kweli ulikuwa ni "usiku wa kifo cha pesa".

Siku nikipata pesa nitarudi tena kidimbwi!!
 
wewe sio mwenyeji mjini. clouds hamna round about. alafu tafuta hela nenda kaitumie hiyo milioni kidimbwi ufe uajiona asubuhi yake. endelea kuuzoe mji, usije zoea majini.
Ahahah Ujuaji mwingi sn tatizo mko nao wabongo..pale maringo wengine tumezoea kupaita clouds Kwa sababu ya lile bango Lao.Tunapomwelekeza mgeni wa mji tunasema shuka hapo roundabout ya clouds ili kuepusha maneno mengi coz akifika atasoma lile bango ..tafuta chai nyingine kisha nikufafanulie
 
nimependa hapo kuhusu “financial freedom”...tutafute hela!! Ila ajabu matajiri huwaoni wakifanya hayo wala huwakuti kidimbwi
Yaani tajirj aende kidimbwi...acha ufala. Tajiri wannafanya yale wanayofanya waarabu kaka....kwenye boti lako unawakaribisha warembo unawapa mbwa wako wagegegdane nao huku wee unagonga monde yako tartibu
 
nimependa hapo kuhusu “financial freedom”...tutafute hela!! Ila ajabu matajiri huwaoni wakifanya hayo wala huwakuti kidimbwi

Watoto wa kishua ndio wanasumbua kidimbwii. Sio matajiri wenyewe..

Wasumbufu wengi kidimbwii ni wale baba gavana BOT.. ama baba CEO bandarini...

Na kuna wale wana urithi wa nguvu. Unakuta baba na mama wamefariki wamewaachia ukumbi za maharusi na appartments za kutosha dar.. hao ndio wanachezea hela kidimbwii.. maana zinaingia tu kila siku

Shida ya kidimbwiii madem wengi ni wadangaji tu.. ukiwaona pisiii kali jichanganyeee wakuuzie ukimwi
 
Wanakula maisha sana lakini mzee, ukifikia level ambayo kuspend million 2-3 per night sio ishu basi life limefikia kwenye kilele cha utamu.

Provided ni kijana huna kipengele hata kimoja mwilini uko 100% perfect kiafya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…