Kifo cha Ruge kinaonesha jinsi Tanzania tulivyo wanafiki

Status
Not open for further replies.
Kila mtu ana mema na mabaya yake..
Kama Ruge alizingua wakati yuko hai unategemea watu wangempigia makofi kisa tu akifa watakosa cha kuongea..

Kwenye mazuri tutamsifia kwenye mabaya tutamsema..
Lakini wakiwa hiki ni kipindi cha msiba tunayaacha mabaya kwanza tuwafariji wafiwa....tutamkumbuka kwa mazuri na tutajifunza kwa mabaya yake..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi naona waliomantain tofauti zao na jamaa kipindi anaumwa basi waendelee kumute hivyo hivyo hata sasa.


Hapo upo sawa kabisa,
maana kuna wapumbavu waliamua kuingiza tofauti hadi kipindi ruge anapigania uhai wake,,
hawa ndo watakuwa wanafki wakubwa kama wataonesha kusikitika.
 
Alizingua Nn?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna vifo watu hushangiilia ila kuna vifo watu huuzunika

Ruge pamoja na madhaifu yake lakini mema yake yalikuwa mengi ndio maana hata waliokuwa na ugomvi nae kwa namna moja au ingine wameungana na wengine kuombea boss Ruge

RIP boss sote njia moja



Sent using Jamii Forums mobile app
 
..Kifo cha ndugu Ruge kimenifunza Yafuatayo.
1. Fedha sio kila kitu
2. Masikini mwenye afya ni bora kuliko tajiri mgonjwa
3. Ugonjwa unaweza kuupuputisha utajiri wako hadi ukabaki huna kitu
4. Tusijione tumefika na kujivika kilemba cha kuwa waamuzi wa maisha na muskabali wa watu wengine
5. Ni vyema sana kujiepusha kujenga maadui (heri yao wapatanishi)
6. Watu wanapokulalamikia, usishupaze shingo. Jikague na ikibidi jirekebishe
7. Qullu nafsi dhaalikal maut
πŸ™πŸ™πŸ™
 
Kwa hiyo kifo chake hakijakupa funzo la kwamba ukiwa na nfasi watengenezee njia wengine kama alivyowafanyia wakina Nandy,Diamond,Barnaba etc?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…