Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 18,772
- 8,939
Lulu ana mimba ya afande....
Lulu mwenyewe kwenye kwenye kipindi cha Mikasi alifunguka kwamba she is 18.
Let her face the consequences.
kwa usalama wake ni lazima atulie humo mahabusu kidogo,
tatizo la watz wataanza kum fa nya hata huko huko aliko,
na katoto kenyewe akili ilishaharibika ataona ndo njia ya kumwokoa, lol.
Yule ni mtoto, walikuwa wanafanya nini uchi chumbani?Kwanza ni a clear self defense case.Nimefuatilia saga ya kale katoto Lulu kuhusiana na kifo cha Kanumba. Interesting, through their twitter accounts hawa waheshimiwa wamejitoa muhanga kumsaidia eti apate fair trial. How: wameenda kumuona na wanatafutia lawyer na psychologist, wamepata cheti chake cha kuzaliwa na kwamba she is only 17 So she is juvenile. wanachangisha michango kumsaidia mama yake na yeye etc.
Maswali yanayonigusa:
1.What precedent r we setting?
2. hivi ni wananchi wangapi tena ambao wananyanyaswa na wako mahabusu na ni wapiga kura wao hawa waheshimiwa wamewasaidia?
3. hivi watoto wetu mabinti wadogo tuwafundishe ubaya gani wa uasherati na uzinzi kama tunapopata mafundisha hatusemi ukweli tunakimbilia she deserves a second chance.
4.Hivi vyombo vya dola vifanye nini kwa kauli tata kama kifo kilifika-JK, ni mtoto mdogo-Zito na Halima?
5. mbona tunapreempty uchunguzi ili tuje tulaumu?
6. Hata kama nyinyi waheshimiwa mlikuwa mna hang nae, hizi hisia zenu kwa sisi wapenda maadili mnatukwaza.
My take: kumtafutia lawyer etc sawa, kuingilia uchunguzi si sawa. fair trial ni kwa both parties. mengine Tamwa na Tawla wapo, msituchanganye.
ha ha ha sio utani kanumba atazikwa kazi kwake yeye
TAARIFA YA TANZIA
BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) kwa masitiko makubwa linachukua fursa hii kutoa salaam za rambirambi na pole za dhati kwa vijana nchini na hususan kwa wasanii wa fani mbalimbali kwa msiba wa mmoja wa waigizaji mahiri, Steven Charles Kanumba.
BAVICHA inamtambua kijana Kanumba kuwa mmoja wa vijana wapambanaji ambao pamoja na serikali kushindwa kuboresha mazingira ambayo wasanii wangeweza kunufaika na kazi zao ipasavyo kama moja ya maeneo muhimu ya ajira yenye staha, yeye na wenzake wachache walimudu kupambana na vikwazo vingi hata wakaweza kuikuza na kuipatia jina, tasnia ya uigizaji nchini.
BAVICHA tunatambua juhudi binafsi za Kanumba na wenzake, ambazo zilisababisha vijana wengine kuweza kupata ajira kutokana na kazi zinazotokana na mchakato wa hatua mbalimbali za ukamilishaji wa filamu, kuanzia katika utungaji, utengenezaji hadi hatua ya uuzwaji wa filamu hizo.
Kwa dhati kabisa, BAVICHA inapenda kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na kwa Watanzania wote kwa ujumla walioguswa na msiba huo. Tunawaombea kwa Mungu, awajalie moyo wa subira wakati huu wa majonzi makubwa.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Marehemu Kanumba, Amina.
Imetolewa kwa vyombo vya habari na
John Heche
Mwenyekiti wa BAVICHA
Aprili 9, 2012
Dogo abakie tu huko mahabusu maana hata now akitoka ataongea na nani huko nje na atapita wapi??