Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Picture%2B1.png


Angalia hii jamani eti anamuita BABA ...........


Picture%2B6.png
YA%2BKWANZA.png


Cheki jamaa anavyochunga mzigo, Hope anachunga KI- ZYGOTE chake wasije kikiharibu.



Picture%2B3.png




Mhhhh!
na hii je,
Eti "HAKI ZOTE ZIMEIFADHIWA" Zipi hizo?
 
what kind of statements to the public. Why dont they mute to awaiting for the judicial position.
 
kwa usalama wake ni lazima atulie humo mahabusu kidogo,
tatizo la watz wataanza kum fa nya hata huko huko aliko,
na katoto kenyewe akili ilishaharibika ataona ndo njia ya kumwokoa, lol.
 
hao wanaojifanya wanalia sana kwanini hawakumtumia
baba kanumba nauli, bongo ni umbeya na majungu ndo yanatawala tu.
 
kwa usalama wake ni lazima atulie humo mahabusu kidogo,
tatizo la watz wataanza kum fa nya hata huko huko aliko,
na katoto kenyewe akili ilishaharibika ataona ndo njia ya kumwokoa, lol.

Dogo abakie tu huko mahabusu maana hata now akitoka ataongea na nani huko nje na atapita wapi??
 
mama atakuwa anafahamu
katoto ka miaka 18 kana gari wewe
utakuwa hujui kweli, saa 6 usiku katoto
kapo kwa kanumba wewe hujui kweli.
sijui lakini.
 
Nimefuatilia saga ya kale katoto Lulu kuhusiana na kifo cha Kanumba. Interesting, through their twitter accounts hawa waheshimiwa wamejitoa muhanga kumsaidia eti apate fair trial. How: wameenda kumuona na wanatafutia lawyer na psychologist, wamepata cheti chake cha kuzaliwa na kwamba she is only 17 So she is juvenile. wanachangisha michango kumsaidia mama yake na yeye etc.
Maswali yanayonigusa:
1.What precedent r we setting?
2. hivi ni wananchi wangapi tena ambao wananyanyaswa na wako mahabusu na ni wapiga kura wao hawa waheshimiwa wamewasaidia?
3. hivi watoto wetu mabinti wadogo tuwafundishe ubaya gani wa uasherati na uzinzi kama tunapopata mafundisha hatusemi ukweli tunakimbilia she deserves a second chance.
4.Hivi vyombo vya dola vifanye nini kwa kauli tata kama kifo kilifika-JK, ni mtoto mdogo-Zito na Halima?
5. mbona tunapreempty uchunguzi ili tuje tulaumu?
6. Hata kama nyinyi waheshimiwa mlikuwa mna hang nae, hizi hisia zenu kwa sisi wapenda maadili mnatukwaza.

My take: kumtafutia lawyer etc sawa, kuingilia uchunguzi si sawa. fair trial ni kwa both parties. mengine Tamwa na Tawla wapo, msituchanganye.
Yule ni mtoto, walikuwa wanafanya nini uchi chumbani?Kwanza ni a clear self defense case.
Sitetei walichofanya kina Zitto, however kusema wasi raise issue kwasababu kuna watoto wengine mahabusu, haina mantiki. Kwenye dunia ya sasa, mfano huu utatumika kama fundisho.
Hao ndo masuper star wenu, unless otherwise useme siyo.
 
Kifo hakizoeleki kinauma sana.
R i p kanumba, bwana alitoa na bwana ametwaa. Amen
 
Nasikitika kafa dhambini,lakini simlilii.Kama unamlilia wewe.


TAARIFA YA TANZIA

BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) kwa masitiko makubwa linachukua fursa hii kutoa salaam za rambirambi na pole za dhati kwa vijana nchini na hususan kwa wasanii wa fani mbalimbali kwa msiba wa mmoja wa waigizaji mahiri, Steven Charles Kanumba.

BAVICHA inamtambua kijana Kanumba kuwa mmoja wa vijana wapambanaji ambao pamoja na serikali kushindwa kuboresha mazingira ambayo wasanii wangeweza kunufaika na kazi zao ipasavyo kama moja ya maeneo muhimu ya ajira yenye staha, yeye na wenzake wachache walimudu kupambana na vikwazo vingi hata wakaweza kuikuza na kuipatia jina, tasnia ya uigizaji nchini.
BAVICHA tunatambua juhudi binafsi za Kanumba na wenzake, ambazo zilisababisha vijana wengine kuweza kupata ajira kutokana na kazi zinazotokana na mchakato wa hatua mbalimbali za ukamilishaji wa filamu, kuanzia katika utungaji, utengenezaji hadi hatua ya uuzwaji wa filamu hizo.
Kwa dhati kabisa, BAVICHA inapenda kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na kwa Watanzania wote kwa ujumla walioguswa na msiba huo. Tunawaombea kwa Mungu, awajalie moyo wa subira wakati huu wa majonzi makubwa.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Marehemu Kanumba, Amina.
Imetolewa kwa vyombo vya habari na
John Heche
Mwenyekiti wa BAVICHA
Aprili 9, 2012
 
Back
Top Bottom