Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Ilikuwa kama ni sheria nyumbani kwetu kuwa chakula cha jioni tujumuike sote kula na baba mezani na si kama nyumbani kwetu kulikuwa na watu wengi.
Mtoto nilikuwa mimi peke yangu na ikiwa hakuna wageni ilikuwa chakula tunakula mimi na baba lakini nyumba yetu ilikuwa haipungui wageni, ndugu na jamaa walikuwa wakimtembelea sana baba yangu.
Akitoka huyu anaingia huyu.
Kwa ajili hii basi mara nyingi tunakuwa watu watatu au wanne kwenye meza ya chakula na huu ndiyo wakati baba anasikiliza taarifa ya habari kutoka TBC.
Sote tunakuwa kimya tukisikiliza taarifa ya habari hadi imalizike. Baada ya hapo baba huweza akasema hili na lile na mazungumzo yakawepo na wageni wake.
Hii ilikuwa miaka ya katikati ya 1960 na TBC kulikuwa na wasomaji wawili wa taarifa ya habari mimi nikiwausudu sana - Suleiman Hegga na David Wakati.
Baada ya chakula ukumbini si muda mrefu panakuwa patupu lakini mimi nitabakia pale ili nisikilize vipindi vyangu nilivyokuwa navipenda katika English Service, vipindi vya muziki wa Kizungu na kama kuna kijana mdogo umri wangu nitachukua gazeti na kujifanya mimi ni mtangazaji niko studio nasoma taarifa ya habari.
Hapo nikawa najifananisha na Suleiman Hegga au na David Wakati.
Wasikilizaji wangu wakinisifia kuwa nasoma vizuri.
Ajabu na hadi leo sijui kwa nini nilikuwa nafanya vile nilikuwa najiona nimevaa shati jeupe na nimefunga tai niko studio.
Nilivutiwa sana na utangazaji wa watu hawa wawili na katika akili yangu nikajenga fikra kuwa nitakapokuwa mkubwa nifanyekazi TBC na niwe msomaji wa taarifa ya habari kama David Wakati na Suleiman Hegga.
Miaka ikaenda katika umri wangu wa kujaza akili nikaja kufahamiana na David Wakati na ikawa kila tukikutana tutazungumza mengi katika utangazaji na vipindi vyake ambavyo mimi nikivipenda sana.
Zamani katika miaka ya katikakati ya 1960 David Wakati Jumapili saa nne asubuhi alikuwa na kipindi, ‘’Negro Spirituals.’’
Kipindi hiki David Wakati alikuwa akipiga nyimbo za kanisani za vikundi vya Kinegro na wanamuziki maarufu wa kuimba ‘’Gospel,’’ lakini siku hizo wakiita ‘’spirituals.’’
Ilikuwa David wakati ndiye aliyenisomesha mimi muziki huu na kuwafahamu magwiji wa mtindo huu kama Mahalia Jackson, Ella Fitzgrerald na Louis Armstrong.
Nyimbo ambayo David Wakati akiipenda sana kuipiga mara kwa mara ilikuwa, ‘’Go Down Moses Let My People Go,’’ ya Louis Armstrong.
Alikuwa pia ana kipindi kingine katika miaka ya 1980 kikirushwa kila Jumamosi baada ya taarifa ya habari kikiitwa, ‘’Nipe Habari,’’ ambacho signature tunenyake ilikuwa nyimbo, ‘’South of the Border Down Mexico Way,’’
Ikawa wakati mwingine hasa panapotokea kifo cha mtu maarufu David Wakati atafanya katika kipindi hiki namna ya taazia na kueleza wasifu marehemu.
Nakumbuka kuna vipindi viwili alivifanya ambavyo marehemu nikawafahamu mmoja kwa kujuananae bayana, Raymond Chihota na mwingine, Rashid Mamboleo Makoko.
Mamboleo Makoko nilimfahamu kwa kusoma barua zake alizokuwa akimwandikia Ally Sykes kutoka London katika miaka ya 1950/60 barua ambazo nilizisoma wakati natafiti maisha ya Abdul Sykes ili niandike kitabu cha historia ya TANU.
Mamboleo Makoko alikuwa na kalamu ya Kiingereza si mchezo.
Ikawa nikikutana mjini na David Wakati tutazungumza kuhusu vipindi vyake na kwa hakika alipenda sana kuzungumza na mimi.
Nilipata kuzungumza na yeye kuhusu kuhusu marehemu Raymond Chihota ambae alikuwa kijana wa Dar es Salaam aliyefanyakazi TBC kabla ya kwenda Urusi kusoma mwanzoni mwa miaka ya 1960.
Kabla hajakwenda Urusi wakati akiwa mtanganzaji wa TBC Raymond Chihota alikuwa mmoja wa vijana katika kundi la Chipukizi akiongoza ‘’Chipukizi Club,’’ kipindi cha TBC ambacho vijana walipiga muziki wa Kizungu na bendi moja ya vijana wa Kigoa ikiitwa, “The Blue Diamonds.’’
Kipindi hiki alikiongoza Raymond Chihota mwenyewe na alikuwa mmoja wa waimbaji wa Chipukizi pamoja na Hussein Shebe, Cuthbert Sabuni, Badrin, Henin Seif, na Salim Hirizi.
Kipindi hiki kilipendwa sana na vijana.
Hizi zilikuwa enzi za Beatles, Elvis Presley, Cliff Richard, Fats Domino, Helen Shapiro na Connie Francis.
Mtu aliyefanya hiki kipindi kiwepo alikuwa David Wakati na hili walinifahamisha wenyewe Chipukizi miaka mingi baadae.
Juu ya haya David Wakati inapofika sikukuu ya Pasaka au Christmas vipindi hivi kutoka kanisani kutangaza ibada hizi alikuwa anashika yeye mwenyewe na utafurahi na nafsi yako jinsi alivyokuwa anaitumia sauti yake kueleza pambio zilizokuwa zinaimbwa.
David Wakati akieleza majina ya nyimbo na kueleza nani alikuwa mpiga kinanda cha kwaya hiyo na ni ukurasa upi kutoka Tenzi za Moyoni nk.
Hiki itabu Tenzi za Moyoni ni kitabu cha nyimbo yaani, ‘’hymns,’’ na David Wakati alikuwa kahifadhi baadhi ya beti za hizi nyimbo na akizisoma ghibu kuasomea wasikilizaji wake.
Hakika ukimsikiliza unatambua kuwa David Wakati alikuwa katika furaha kubwa.
Mimi sikuacha hata mwaka mmoja kumsikiliza David Wakati katika sikukuu hizo.
Lakini nilikuja kumjua David Wakati zaidi kadri miaka ilivyokuwa inasogea na mambo yanazuka yanayohitaji taarifa za serikali zisomwe na yeye.
Taarifa hizi alikuwa David Wakati akizisoma kwa ufundi wa hali ya juu sana kiasi cha kumtisha msikilizaji.
Nitatoa mfano mmoja.
Katika ya miaka ya 1990 palitokea mgongano kati ya Waislam na serikali kuhusu hali ya elimu ya vijana wa Kiislam na mchango wa shule za Waislam zilizojengwa na EAMWS lakini ziko chini ya BAKWATA.
Vijana wa Warsha wakiongozwa na marehemu Burhani Mtengwa na marehemu Mussa Mdidi walifanya jitihada za kuzigeuza shule hizi kuwa seminari za Kiislam kuwanufaisha wanafunzi wa Kiislam.
Serikali haikuafiki jambo hili ikidai zirejeshwe ziwe shule za kawaida.
Hoja yaWaislam ilikuwa kama Wakristo wana seminari basi na Waislam na wao wawe na zao.
Serikali ikatoa amri ya kuzifuta shule hizi na kuzirejesha kama zilivyokuwa awali.
Marehemu Abbas Kilima akiwa kiongozi wa mabadiliko haya aliitisha mkutano wa Waislam Shule ya Kinondoni ili wazungumze hali ya baadae ya Waislam katika elimu ya watoto zao.
Taarifa hii ilienea kote na Waislam walipania kwenda kusikiliza yatakayosemwa katika mkutano ule agenda yake iikiwa kujadili hatua ya serikali kufuta saminari za Kiislam.
Tatizo la elimu ya Waislam toka kabla ya uhuru ni jambo nyeti na serikali haikuwa tayari kuingia katika mjadala na Waislam katika hili.
Usiku wa kuamkia siku ya mkutano David Wakati aiingia studio kusoma taarifa ya serikali kuonya kuwa mkutano huo ni batili na asijitokeze mtu kwenda kuhudhuria. Taarifa hii nimeisikia kwa masikio yangu na nikajiuliza kwa nini taarifa hii isomwe na David Wakati?
Bahati mbaya sikupata kufahamiana na Suleiman Hegga lakini kila nilipokuwa namsikiliza David Wakati katika vipindi vya Pasaka na Christmas basi lazima fikra zangu zitakwenda kwa Suleiman Hegga nikitamani na yeye nimsikilize siku moja labda akitangaza Maulidi ya Mfungo Sita au Sikukuu ya Eid kwa ubingwa ule ule alionao katika kusoma habari.
Hata vivyo Allah alipokea dua yangu nikabahatika siku moja kumsikia Suleiman Hegga akirushwa mubashara kutoka Ukumbi wa Arnautoglo, Dar es Salaam katika Baraza la Iddi tarehe 17 April 1991, Mgeni wa Heshima akiwa Rais Ali Hassan Mwinyi.
Suleiman Hegga akiwa Makamu Mwenyekiti wa BAKWATA katika hotuba yake ya kumkaribisha Rais Mwinyi aliishutumu serikali kwa kusita kuwashughulikia Waislam wanaopinga BAKWATA.
Nilimuhurumia sana Suleiman Hegga kwani nilikuwa najua hali iliyokuwa ikimkabili yeye kama kiongozi wa BAKWATA katika kipindi kile cha uongozi wa Rais Mwinyi.
Nilifahamu fika kuwa ile hotuba ya Suleiman Hegga itakuwa imepita mikono mingi kurekebishwa hapa na pale na watu wenye mamlaka makubwa kushinda yeye. Hotuba ile haikuwa hotuba iliyostahili kusomwa katika siku ya furaha ya kusheherekea Eid kwani ilikuwa hotuba inayorejesha machngu kwa Waislam.
Nilimsikitikia kwa ule mzigo alioubeba katika hotuba ile kwani daima nilijua itaishi katika kumbukumbu za nchi na ndani ya fikra za Waislam na nani atakaeihangaisha akili yake kutafuta undani wa maneno ya Suleiman Hegga katika hotuba ile ili kumnusuru na maneno yale ambayo pengine hata si yake?
Nikawa najiuliza kipi kilichomfanya David Wakati awe vile na Suleiman Hegga awe hivi? Nikawa pia kila ninapomkumbuka Suleiman Hegga na hotuba ile huishia kwa kusema, “’Allah ndiye Mjuzi.’’
Allah amsamehe mzee wetu Suleiman Hegga na amfanyie wepesi safari yake.
Amin.
PICHA:
Suleiman Hega
Kulia mbele ni Henin Seif na kushoto ni Hussein Shebe. Aliyesimama nyuma ya Henin ni Raymond Chihota na aliyesimama kushoto kwa Mzungu ni Mbarak maarufu kwa jina la Mbarak Bata kwa kuwa akifanya kazi Bata Shoes na katikakati ya Mzungu na Raymond Chihota ni Hussein.
Picha ya tatu ilipigwa katika mgahawa wa Sadiki Patwa Tanga wakiwemo Mwalimu JK Nyerere na Bw. Patwa kulia kwake unapoitazama picha. Kulia mwenye koti na kofia Mzee Rashid Makoko na wa pili yake ni mwanae Rashid Mamboleo Makoko na kushoto mwenye koti na kofia Mzee Makata Mwinyimtwana tajiri mkubwa Tanga katika miaka ya 1950/60.