Kifo hakipangwi na Mungu

Ni kweli kabisa! Kuna kijana jirani yangu anaitwa Joshua kauawa kwa kupigwa nyundo kichwani umri chini ya 35.Ati watu wanasema kuwa ni mapenzi ya Mungu!
 
Ni kweli kabisa! Kuna kijana jirani yangu anaitwa Joshua kauawa kwa kupigwa nyundo kichwani umri chini ya 35.Ati watu wanasema kuwa ni mapenzi ya Mungu!
Mungu ni hadithi tu, hayupo.

Kama mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini aruhusu ulimwengu ambao mtu anaweza kufa kifo cha hivyo wakati angeweza kuumba ulimwengu usio na kifo kabisa?
 
Kama mwanadamu unapaswa kutambua kwamba, pamoja na ufahamu ulionao lakini si kila kitu unaweza kukijua au lazima ukijue, vile vile kutokujua uwepo wa kitu fulani hakumaanishi kitu hicho kuwa hakipo. Mimi sifahamu wewe ni nani nje ya network, au mahali ulipo lakini naamini wewe ni mtu, je ikiwa sikujui basi maana yake haupo? Wewe ukisema upo nitakuwa na hakika gani kwamba ni kweli upo na hudanganyi?

Ikiwa unakubali kwamba wewe ni atheist, je, unaweza kututhibitishia kwa kiwango kile kile unachopinga kwamba Mungu hayupo?
 
Unaonekana kutoelewa falsafa ya uthibitisho.

Uthibitisho ni kwa vilivyopo, visivyopo havithibitishiki kwamba havipo, kwa sababu havipo ili kuthibitishwa kwamba havipo.

Kutokujua kitu hakumaanishi kitu kipo, wala hakumaanishi kitu hakipo, kunamaanisha hujui.

Ili kujua kwa uhakika kwamba mungu yupo, huwezi kusema unajua hilo kwa sababu hujui kila kitu. Hiyo sababu haitatosheleza.

Na maadam visivyokuwepo havithibitishiki (kwa sababu havipo ili kuthibitishika kwamba havipo) na uthibitisho ni uwanja wa vilivyopo, swali linaenda kwa wanaosema mungu yupo.

Wanaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?

Ukiniuliza mimi nithibitushe kwamba mungu hayupo, nitakwambia siwezi kuthibitisha kwamba hayupo, kwa sababu hayupo.

Kama wewe usivyoweza kuthibitisha kwamba pembetatu duara haipo.

Wanaosema mungu yupo wanaweza kuthibitisha mungu yupo?
 
Majibu yako tu yanaonesha jinsi ulivyochanganyikiwa. Hebu rudia kusoma ulichonijibu na nilichoomba unijibu.
 
Majibu yako tu yanaonesha jinsi ulivyochanganyikiwa. Hebu rudia kusoma ulichonijibu na nilichoomba unijibu.
Mara nyingine waliochanganyikiwa huona wengine wamechanganyikiwa.

Kama hujaweza kuonyesha nimechanganyikiwa vipi na wapi, inawezekana wewe ndiye umechanganyikiwa kwa kutoweza kuelewa mambo yaliyokupita kimo.
 
Mimi naamini Mungu yupo ila nakuwa mwangalifu na imani hiyo. Mambo ya Mungu ni magumu, usipokuwa mwangalifu unapoteza uwezo wako wa kufikiri na kung'amua mambo.

Kusema Mungu hupanga kifo ni kisingizio cha kuendelea kuwa wavivu na wajinga.
 
Kwa nini unaamini kwamba mungu yupo?
 
Juzi Magufuli kasema Mungu yupo na yeye...
sasa soon itakua ukimkosoa Magufuli unamkosoa Mungu
Watawala tangu enzi za Wababeli, Wachina na Wamisri wametumia gia ya Mungu kujinufaisha katika utawala wao.

Hata Kikwete walisema ni chaguo la mungu.

Hakuna jipya hapo.
 
Mara nyingine waliochanganyikiwa huona wengine wamechanganyikiwa.

Kama hujaweza kuonyesha nimechanganyikiwa vipi na wapi, inawezekana wewe ndiye unechanganyikiwa kwa kutoweza kuelewa mambo yaliyokupita kimo.
Hata jibu lako hili linaonesha ulivyo mtu wa kukurupuka kujibu. Ikiwa unaamini kwamba kuna mambo yanayoweza kupita kimo cha ufahamu wangu, kwanini basi nisiamini hivyo kwako kwamba hata hilo la Mungu ni jambo lililokupita kimo chako cha ufahamu?
Ukitaka nikuthibitishie na kukuonesha jinsi ulivyochanganyikiwa, nioneshe kwanza na kunithibitishia kwamba Mungu hayupo.

Najaribu kukusoma kwenye michango yako, kwa mfano unasema imani ya kuwepo Mungu ilianzia zama za giza, je unaweza kutupa uthibisho wa kuwepo kwa zama hizo? Wewe ni atheist lakini msimamo wako huo umejengwa juu ya wengine ndio maana unapata ujasiri wa kuturejesha kifikra kwenye zama ambazo hukuwepo na hakuna anayethibitisha kwamba zilikuwepo.
 
Watawala tangu enzi za Wababeli, Wachina na Wamisri wametumia gia ya Mungu kujinufaisha katika utawala wao.

Hata Kikwete walisema ni chaguo la mungu.

Hakuna jipya hapo.
Unawezaje kututhibitishia uwepo wa zama hizo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…