Hata jibu lako hili linaonesha ulivyo mtu wa kukurupuka kujibu. Ikiwa unaamini kwamba kuna mambo yanayoweza kupita kimo cha ufahamu wangu, kwanini basi nisiamini hivyo kwako kwamba hata hilo la Mungu ni jambo lililokupita kimo chako cha ufahamu? .
Unaweza kuamini chochote unachotaka kuamini. Lakini kuamini hivyo hakufanyi Imani yako kuwa kweli.
Unaweza kuamini kwamba Mungu ni jambo lililonipita ufahamu.
Lakini, nimekupa nafasi kuthibitisha kama mungu yupo.
Umeshindwa.
Hivyo, unaamini habari isiyothibitishika.
Ukitaka kuamini kitu kipo kwa kusema kimepita uelewa wetu, unaweza kuamini chochote.
Unaweza kuamini mungu yupo, na kapita uelewa wetu.Na hapohapo ukaamini mungu hayupo, na kuelewa hilo kumepita uelewa wetu.
Dhana nzima ya kutafuata ukweli kwa mantiki inavunjika.
Utakubali vipi habari ya kwamba mungu yupo na kapita uelewa wangu wakati hata huwezi kumuelezea na kuthibitisha yupo?
Nikiondoa mungu na kuweka neno lingine lolote, kwa mfano, "nyani mkuu" aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyopo, yupo, na humjui kwa sababu kapita uelewa wako tu, utawezaje kukataa kama umekubali kwamba mungu yupo na kapita uelewa wangu tu?
Ukitaka nikuthibitishie na kukuonesha jinsi ulivyochanganyikiwa, nioneshe kwanza na kunithibitishia kwamba Mungu hayupo.
Inaonekana hujaelewa habari nzima niliyoiandika kuhusu falsafa ya uthibitisho.
Tena nimeandika Kiswahili usije kusema nimeandika lugha ngeni hukuelewa.
Visivyopo havithibitishiki kwamba havipo.Kwa sababu havipo.
Vinavyothibitishika ni vilivyopo, kwa sababu vipo.
Ndiyo maana hata polisi wakija kumkamata mtu kwa kosa la kuwa na madawa ya kulevya nyumbani kwake, hawamwambii "thibitisha kwamba nyumba yako haina madawa ya kulevya". Hata akiichambua nyumba hiyo kwa miaka milioni moja kutaka kuonyesha kwamba nyumba haina madawa ya kulevya, hilo halitathibitisha kwamba nyumba haina madawa ya kulevya.
Njia pekee ya uhakika kuthibitisha ni Polisi kusachi nyumba kwa taratibu na hakika mpaka wapate madawa ya kulevya.Hapo watakuwa wamethibitisha kwamba madawa ya kulevya yamo kwenye nyumba hiyo.
Sasa unachofanya wewe ni sawa na polisi anamwambia mtu "thibitisha nyumba yako haina madawa ya kulevya". Ni kutoelewa falsafa ya uthibitisho.
Unachotakiwa kufanya ni kuonyesha madawa ya kulevya yapo.
Sasa wewe unayesema mungu yupo, unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?
Najaribu kukusoma kwenye michango yako, kwa mfano unasema imani ya kuwepo Mungu ilianzia zama za giza, je unaweza kutupa uthibisho wa kuwepo kwa zama hizo? .
Kabla ya kukujibu, unaelewa nini mtu akikwambia "zama za giza"?
Wewe ni atheist lakini msimamo wako huo umejengwa juu ya wengine ndio maana unapata ujasiri wa kuturejesha kifikra kwenye zama ambazo hukuwepo na hakuna anayethibitisha kwamba zilikuwepo.
Wewe unayekubali mungu wa kutungiwa na wengine na kuletewa kwenye vitabu ulikuwepo wakati huyo mungu alivyofanya hayo anayosemwa kuyafanya kwenye vitabu?