Uislamu ni dini ya mapokeo hususan ktk mambo ya ghaibu, yaani tunaamini kuran yote na Hadith sahihi zote tena si kwa uewelewa wetu bali kama walivyoelewa Maswahaba Allah awaridhie wote. Huu ni msingi muhimu sana ktk dini ya uislamu. Kwahivyo basi kwa mujibu wa Quran na Sunnah kama walivyofahamu Maswahaba Allah awaridhie wapo watu watakao kaa motoni MILELE na wapo watu watakaa motoni kwa muda fulani kisha watatolewa humo na kupelekwa motoni.
Mkuu kidula,kabla sijakujibu
Mkuu, kiduila, umenena vyema pale uliposema:- " Tunaiamini Qur'an yote na Hadithi zote (sahihi)"
Mfasirina wa kwanza wa Qur'an ni mtukufu mtume Muhammad (saw) yeye amepata kusema kwamba juu ya kuopolewa watu wa motoni kutoka motoni itakuwa hivi watu watakatifu watawaombea na hapo Mungu (Allah) atawatoa baadhi kutoka katika Jehanam halafu itakuja zamu ya Mtume (saw) kuwaombea hapo Allah atawatoa baadhi kutoka katika jehanamu na mwisho Allah mwenyewe ataweka qadar yake na hapo hatobaki yeyote ndani ya jehanam. (Nimejaribu kuitafuta hadithi hii ipo wapi nimeshindwa, lakini ipo).
Hadithi hiyo inaunga mkono aya hizi za Qur'an:- 78:22 na 6:128.
Katika Qur'an kuna aya kadhaa zinazozungumza kuhusu watu wa motoni na peponi ambapo neno "abada" limetumika na hasa utalikuta katika mtindo huu "khalidina fiiha abada" yaani watakaa humo "MILELE" neno "abada" siyo mara zote huwa na maana "MILELE" pia maana yake nyingine ni "KIPINDI CHA MUDA MREFU SANA". sasa kama baadhi ya watu watakaa motoni milele (kama ulivyosema) huoni kuwa kutakuwa na khitilafu ndani ya Qur'an !!?.
Kuna aya fulani (nimeisahau) inasema kuwa "pepo ni kipawa kisichokatishwa na jehanam ni kipawa kinachokatishwa" (maneno kama hayo).
Ukisoma katika Suratul Qaria katika aya ya 8, kuna maneno haya juu ya watu wa motoni:-
"Wa ammaa man khffati mawaaziinuhu faaummuhu haawiya" yaani:- na amma yule mizani yake ni hafifu basi MAMA YAKE ni (atakuwa) haawiya.
Hapo haawiya imeitwa mama kwa ajili ya wakosefu, sasa kwa nini Allah ameufananisha moto huo wa haawiya kama mama?!, ukifahamu kazi ya mama kwenye jukumu la malezi basi utajuwa kuwa wakosefu wanapokua ndani ya moto ni kama wanalelewa na baadaye "wakishakuwa wakubwa" yaani wakiwa safi kiroho baada ya kuchomwa na moto wa haawiya wataaingizwa peponi.
🍒Huyo ndiye Allah mtukufu na utukufu wake🍒