Kifo kinatisha kwa sababu hatujui kule tuendako

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
Kifo kimebaki kuwa siri nzito kati ya yule aliyepata umauti na mola wake kwa sababu moja tu kwenye kifo hakuna uhai unaoweza kumfanya yule aliye mfu kusema yale anayoyaona mara tu baada ya kifo chake,

Kuna elimu nyingi zinazoelezea Kifo ziko zile ambazo ukizisoma zinakuongezea maarifa na nini kinatokea baada ya kifo chako,

Refer;

Sanaa ya kifo - JamiiForums

Licha ya Elimu hizo Adimu lakini bado hakuna ithibati ya moja kwa moja hivyo Kumeweza kukifanya Kifo bado kuwa ni siri kati ya yule marehemu na mola wake,

Kuna mengi ya kujiuliza na yakuogopesha kwa kweli kwa mfano
Ukiingia kwenye upande wa imani tunaambiwa Lazaro alifufuka katika wafu kwa maana hiyo lazaro ni mmoja kati ya wale wachache walioonja chungu ya mauti na kurudishiwa uhai wake tena,

Kama ni kweli kwanini lazaro hakuwahi kusema kile alichokumbana nacho baada ya kifo chake na badala yake ametuachia maswali na indication nyingi kuhusu kifo naweza kusema lazaro alikuwa mbinafsi kwa nini hakutaka wengine tujue.?

Upande wa pili pia wanasema ukifa unaenda kukutana na starehe ambayo hujawahi pata tangu uingie duniani ,hakuna magonjwa ,misosi ya kila aina ,bila kusahau mademu wakali ambao ni bikra ,

Ukija pia kuangalia huyo anaekuelezea ilo somo na kukuhubiria kuhusu raha na starehe zinazopatikana baada ya kifo Maisha yake ni ya kugongea na tabu tupu,unabaki kujiuliza kama ni kweli kuna hizo starehe kwa nini Asife yeye akazipate hizo Raha?

Wakuu nisiwachoshe sana ila kuna indication nyingi sana kuhusu kifo,hakuna namna yeyote ya kuelezea kuhusu kifo,kifo kinatisha kwa sababu kila mmoja wetu anajua ni lazima atakufa lakini hakuna anaejua ni nini kitamtokea baada ya kifo chake,

Na ndio maana kifo kinaogopeka.
 
Sioni haja ya kuogopa kifo mkuu Zero IQ , uliwahi kujiuliza ulipokua upo tumboni kwa mamayo ama kama umepitia (IVF) in-vitro fertilisation ulikua unajua unaenda wapi, ama uko wapi? Kama ulikua hujui don't bother yourself about death experience! Je, kama uta transcend na kuingia kwenye another womb?
je, kama kabla ya kuwa hapo ulipo uliwahi kuishi sema tu upo clouded na conscious mind na hujawahi enda beyond ujue kuna nini?
Mfano, budha kabla ya kuzaliwa anasema alikuwa ni tembo.. vipi kuhusu wewe?
Btw,
Maisha mazuri sio jumla ya miaka uloishi hapa duniani bali ni kwa kiasi gani ume serve the humanity, universe.. sio unaishi kama methusela wa kwenye biblia ya wakristo and yet hakufanya chochote kwa mungu wake.
within u all answers to ur questions resides. .
Start ur journey home brother.
 
Mkuu nashukuru kwamba tuna mawazo yanayofanana kuhusu kifo ,nilishawahi kuja na bandiko hapa na kusema kwamba kama unajiuliza ukifa unaenda wapi basi jiulize kabla ya kuzaliwa ulikuwa wapi ?

Na ndio maana zilikuja theory nyingi zinazoelezea maisha ya kifo.
 
Ni kweli kabisa ukiwaza kuhusu kifo lazima furaha ikutoke. Ukifikiria kwamba umri wa kuishi hapa Duniani hauzidi karne moja (kwa walio wengi), wakati ukifa kuna maisha mengine ya milele (kidini), na hayo maisha yanategemea ulijiandaa vipi ulipokuwa hai, lazima furaha ikutoke
 
Kaka huwa unatumia nini yaani nyenzo gani kutafakari kuhusu kifo ? Hili swali la msingi sana.

Ukijibu swali hilo nakuja na swali lingine......
 
Ni kweli kabisa ukiwaza kuhusu kifo lazima furaha ikutoke. Ukifikiria kwamba umri wa kuishi hapa Duniani hauzidi karne moja (kwa walio wengi), wakati ukifa kuna maisha mengine ya milele (kidini), na hayo maisha yanategemea ulijiandaa vipi ulipokuwa hai, lazima furaha ikutoke
Wastani wa umri wa kuishi kwa zama zetu hizi ni miaka 70 ukitokea kupewa zaidi ya miaka hiyo ni rehma zake Mola Muumba.
 
Mama yangu ni nurse muhimbili zaidi ya miaka 30 , aliwahi kuniambia Kwa experience yake ya kuwaona wagonjwa wakifariki aliniambia Kwa mtu anayekufa taratibu anajua wapi anaenda.
Aliniambia amewahi kushuhudia zaidi ya Mara kumi wagonjwa wanatoa tabasamu wakifurahia malaika wakija kuwachukua huku wakisifia mji wanaokwenda ni mzuri sana, akazidi kuniambia utashangaa mgonjwa alikuwa Amalia maumivu makali ya ugonjwa Mara anabadilika anaanza kutabasamu na anakuwa kama anataka kupaa huku akiwasihi malaika wamchukue.
Na upande wa pili wanaokwenda sehemu mbaya ndio balaa bora niishie hapa
 
Hii sio chai kweli hii
 
Ili uende unatabasam jiandae sasa ukiwa hai kwa kujenga nyumba yako ya baadaye, lakini kwa sisi binAdam tulivyowabishi tumekazana kujenga nyumba ambazo tutaziacha kesho. Bila shaka hao waliokuwa wakitabasam walijiandaa mapema
 
Mama yangu ni nurse muhimbili zaidi ya miaka 30 , aliwahi kuniambia Kwa experience yake ya kuwaona wagonjwa wakifariki aliniambia Kwa mtu anayekufa taratibu anajua wapi anaenda.
Aliniambia amewahi kushuhudia zaidi ya Mara kumi wagonjwa wanatoa tabasamu wakifurahia malaika wakija kuwachukua huku wakisifia mji wanaokwenda ni mzuri sana, akazidi kuniambia utashangaa mgonjwa alikuwa Amalia maumivu makali ya ugonjwa Mara anabadilika anaanza kutabasamu na anakuwa kama anataka kupaa huku akiwasihi malaika wamchukue.
Na upande wa pili wanaokwenda sehemu mbaya ndio balaa bora niishie hapa
Duuuu
 
Back
Top Bottom