Kifo kinatisha kwa sababu hatujui kule tuendako

Kifo kinatisha kwa sababu hatujui kule tuendako

ila ikitokea hujaishi hiyo miaka inakua rehema za nani?
Wastani wa umri wa kuishi kwa zama zetu hizi ni miaka 70 ukitokea kupewa zaidi ya miaka hiyo ni rehma zake Mola Muumba.
 
Hujawahi kutana na mtu anafanana copyright na mtu mwingine wasio na uhusiano smbae ashakufa?
 
bado tangawizi mkuu ..


Ni kweli kabisa, hakuna shaka yoyote na jambo hilo, na inatupasa tujitahidi kutafuta njia sahihi za kufanya Ibada na kufanya mambo mema hapa duniani ili tutakapo kufa tukalale mahala pema huko Akhera.
 
Hakuna maisha baada ya kifo!
Ukishakufa stage unayoiendea ni kuoza na kuisha kabisa hadi kufikia hali ya udongo kamili

Tulikuwa hatupo, tumewepo na hatimaye hatutokuwepo tena mahala popote ulimwenguni

Ukisema kuna maisha baada ya kifo inamaanisha unaupinga ukweli unaoujua wewe mwenyewe ya kwamba, afapo kiumbe yeyote anaoza na kuharibika!

HAKUNA MAISHA BAADA YA KIFO

Kama vile ambavyo hukumbuki lolote nyuma kabla ya kutunga kwa mimba yako, ndivyo hivyo itakavyokuwa baada ya kufa kwako

Lakini kifo sio cha kuogopa maana lazima tujue kuwa, kama kuna kuwepo basi kutokuwepo kupo pia

Kifo ni rafiki mzuri kuliko uzima
Hata hali ya utoto tukiwa bado wachanga hatukumbuki,lakini hio sio kwamba hakukuwa na chpchote kipindi hicho ndiyo mana hatukumbuki.
 
ila ikitokea hujaishi hiyo miaka inakua rehema za nani?
Unajua maana ya wastani bro ? Au hujui ? Kama hujui usiandike au kujenga hoja juu ya jambo usilolijua.

Hapo hujauliza swali bro,labda baada ya haya ndio utauliza swali.
 
Sioni haja ya kuogopa kifo mkuu Zero IQ , uliwahi kujiuliza ulipokua upo tumboni kwa mamayo ama kama umepitia (IVF) in-vitro fertilisation ulikua unajua unaenda wapi, ama uko wapi? Kama ulikua hujui don't bother yourself about death experience! Je, kama uta transcend na kuingia kwenye another womb?
je, kama kabla ya kuwa hapo ulipo uliwahi kuishi sema tu upo clouded na conscious mind na hujawahi enda beyond ujue kuna nini?
Mfano, budha kabla ya kuzaliwa anasema alikuwa ni tembo.. vipi kuhusu wewe?
Btw,
Maisha mazuri sio jumla ya miaka uloishi hapa duniani bali ni kwa kiasi gani ume serve the humanity, universe.. sio unaishi kama methusela wa kwenye biblia ya wakristo and yet hakufanya chochote kwa mungu wake.
within u all answers to ur questions resides. .
Start ur journey home brother.
nimekuelewa sana bradha,asante.
 
mbona umesema ulikua haupo kisha ukawepo ,thena utakua haupo milele,kwanini baada ya kutokuwepo isitokee uwepo tena kisha uwe haupo then uwepo tena,kwanini baada ya kutokewepo hii mara ya pili iwe ndio forever wakati hata mwazo ulikua haupo kisha ukawepo
 
Huwa tunarudi kivingine,Roho haiwezi kufa bali mwili,kwa mtazamo wangu
 
Sawa,tufanye tu umeambiwa unakufa halafu utatokezea marekani hautagopa kufa..?
 
Mkuu nashukuru kwamba tuna mawazo yanayofanana kuhusu kifo ,nilishawahi kuja na bandiko hapa na kusema kwamba kama unajiuliza ukifa unaenda wapi basi jiulize kabla ya kuzaliwa ulikuwa wapi ?

Na ndio maana zilikuja theory nyingi zinazoelezea maisha ya kifo.
No fear, nachojua nitarudi nilipokuwa... roho itarudi pale ilipokuwa kabla haijaingia ndani ya mwili wangu! Kwa sababu wat goes around must come around..! Nitarudi nilipokuwa maana kazi iliyonileta duniani itakuwa imeshakwisha...
 
Kifo kimebaki kuwa siri nzito kati ya yule aliyepata umauti na mola wake kwa sababu moja tu kwenye kifo hakuna uhai unaoweza kumfanya yule aliye mfu kusema yale anayoyaona mara tu baada ya kifo chake,

Kuna elimu nyingi zinazoelezea Kifo ziko zile ambazo ukizisoma zinakuongezea maarifa na nini kinatokea baada ya kifo chako,

Refer;

Sanaa ya kifo - JamiiForums

Licha ya Elimu hizo Adimu lakini bado hakuna ithibati ya moja kwa moja hivyo Kumeweza kukifanya Kifo bado kuwa ni siri kati ya yule marehemu na mola wake,

Kuna mengi ya kujiuliza na yakuogopesha kwa kweli kwa mfano
Ukiingia kwenye upande wa imani tunaambiwa Lazaro alifufuka katika wafu kwa maana hiyo lazaro ni mmoja kati ya wale wachache walioonja chungu ya mauti na kurudishiwa uhai wake tena,

Kama ni kweli kwanini lazaro hakuwahi kusema kile alichokumbana nacho baada ya kifo chake na badala yake ametuachia maswali na indication nyingi kuhusu kifo naweza kusema lazaro alikuwa mbinafsi kwa nini hakutaka wengine tujue.?

Upande wa pili pia wanasema ukifa unaenda kukutana na starehe ambayo hujawahi pata tangu uingie duniani ,hakuna magonjwa ,misosi ya kila aina ,bila kusahau mademu wakali ambao ni bikra ,

Ukija pia kuangalia huyo anaekuelezea ilo somo na kukuhubiria kuhusu raha na starehe zinazopatikana baada ya kifo Maisha yake ni ya kugongea na tabu tupu,unabaki kujiuliza kama ni kweli kuna hizo starehe kwa nini Asife yeye akazipate hizo Raha?

Wakuu nisiwachoshe sana ila kuna indication nyingi sana kuhusu kifo,hakuna namna yeyote ya kuelezea kuhusu kifo,kifo kinatisha kwa sababu kila mmoja wetu anajua ni lazima atakufa lakini hakuna anaejua ni nini kitamtokea baada ya kifo chake,

Na ndio maana kifo kinaogopeka.
Mtaalamu wa hatima yetu baada ya kifo ni Kiranga
 
Back
Top Bottom