Kifo kinatisha sana na ni chenye maumivu makali yasiyoweza kuelezeka. Uhai ni wa thamani pindi tu ukiukosa

Kifo kinatisha sana na ni chenye maumivu makali yasiyoweza kuelezeka. Uhai ni wa thamani pindi tu ukiukosa

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
600
Reaction score
1,843
Utakapokufa katu hutoweza kurudi tena duniani.

Ukweli ni kwamba watu wengi wanaogopa kufa, ijapokuwa wapo ambao inafikia hatua hawaogopi kifo kabisa, lakini pia inaweza kufikia hatua kwa baadhi ya watu mpaka wakakiomba kifo. Hii huwenda ni kutokana na shida na taabu walizo nazo. Lakini katika uislamu IMEKATAZWA KATU KUTAMANI KIFO.

Mtume (s.a.w) amesema: “Asitamani mmoja wenu MautI (kifo) ima akiwa ni mwema kwani huenda akazidisha heri ama akiwa ni muovu huenda akatubia.

Mtume wa Allah ametukataza tusitamani kufa yaani mauti.
Tusitamani kufa kwa hali zozote tulizo nazo tukiwa ni wachamungu sana ama tukiwa ni waovu sanaa.
Ukiwa mchamungu uhai wako unaweza kuutumia vyema na ukazidisha uchamungu hivyo ukapandisha daraja yako kwa Allah

Ukiwa ni muovu unaweza kutumia fursa ya uhai uliyonayo na ukatubu na Allah akakusamehe na ukaweza kuipata pepo. Kwani Allah husamehe madhambi yote pindi mja akitumia toba ya kweli.

Uhai ni wa thamani pindi tu ukiukosa hutoweza kufanya jambo lolote tena.

Mtume s.a.w amesema “asitamani mmoja wenu mauti na wala asiyaombe mauti kabla hayajamjia kwani hakika pindi atakapokufa, amali zake zote zinakatika, na kwa hakika hautamzidishia muumini umri wake isipokuwa heri”.

Tusitamani kufa na si kutamani tu bali hata tusithubutu kufa, kwani kama tutapewa uhai zaidi na tukiwa wema huenda uhai wetu ukawa ni chachu ya sisi kuzidisha wema. Na kama tukiwa ni waovu huenda tukatubu.

Mtu akifa amali zake zote zinakatika. Yaani kama ni muovu na hajatubia madhambi yake kwa Allah basi hatoweza tena kutubia, na kama ni mwema hatoweza kufanya tena mambo mema.

”Atakapokufa mwanadamu amali zake zote (matendo) hukatika isipokuwa matendo ya (amali) aina tatu SADAKA YENYE KUENDELEA, ELIMU YENYE KUPATISHA MANUFAA AU MTOTO MWEMA ATAKAYEMUOMBEA DUA”. Haya ni katika matendo ambayo yataweza kutupatisha faida pindi tutakapo fariki.

1669240321331.png

BAKIIF ISLAMIC
P.O.BOX 55185
Kimara Korogwe,
KAM College Road, Kivulini Street
House no 36
Phone +255 755 351 262
 
Ngoja waje marehemu watarajiwa ndio utajua mbichi na mbivu
 
Je wale wanaofia usingizini nao huwa na maumivu yapi? Nimewahi kumshuhudia babu yangu anakata roho tulikuwa tunaongea nae ghafla akawa kimya tu sasa kama angepitia hayo maumivu unayodai wewe na Mohammad si tungemuona jinsi anavyorukaruka kama kuku aliechinjwa?
 
Labda kifo cha kuchinjwa au kuliwa na Mnyama.
 
Sasa mbona kuna makundi ya waislamu wenye siasa kali, hutumia vijana wa kujitoa mhanga, suicide bombers?
Wakati huo huo Muhammad SAW alisema tusitamani kifo kwa jambo lolote.
 
Back
Top Bottom