KIFO KUINGIZWA KWENYE ORODHA YA HAKI ZA BINADAMU

KIFO KUINGIZWA KWENYE ORODHA YA HAKI ZA BINADAMU

Decree Holder

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2015
Posts
2,559
Reaction score
3,745
HAKI YA KIFO

Wanajamvi salamu!

Huwenda mmekuwa mkisikia haki mbalimbali za binadamu mpaka haki ya ushoga lakini hamjawahi kusikia haki ya kufa. Naamu "right to die" ni haki ya binadamu ambayo sasa inatetwa kwa kasi sana kama haki zingine kwamba watu waachwe wafe let them die if they wish men.

Huenda ukashangaa kwa maana sote tunafahamu kuwa kufa ni lazima na siyo swala la watu kudai kama haki za binadamu. Vitabu mbalimbali vitakatifu vimeandika kuwa kufa ni lazima wote tunajua.

Haki hii ya kufa imezua mjadala mzito iwapo kama kweli mtu ana haki ya kufa? Kivipi? Kwani kuna mtu anayenyimwa kufa? Ndiyo!

Mjadala mkubwa wa kisheria ulitokea katika kesi ya Pretty V United Kingdom ni kesi ya uingereza kwenye mahakama ya haki za binadamu ya umoja wa Ulaya. Katika kesi hii mwanamke aitwaye Pretty alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa unaoshambulia misuli ambao hauna tiba. Alipooza kuanzia shingoni kushuka chini alibaki kichwa tu hivyo alikuwa anafahamu zote (akili timamu). Aliomba asaidiwe afe tu ili kuondokana na mateso ya ugonjwa ambao anajua mwisho wa siku hatapona. Aliomba aruhusiwe mume wake amsaidie kujiua (assisted suicide) kutokana na kwamba amepooza. Wanasheria na waendesha washitaka walikataa kwani Uingereza kumsaidia mtu kujiua ni kosa la jinai hivyo wakasema kama mumewe atamsaidia lazima mume huyo atakuwa na hatia. Hii kesi ilikatiwa rufaa kwenye mahakama zote za Uingereza mpaka mahakama za juu za Uingereza haki hii ya kufa ikakataliwa. Katika Mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya ilifika na mjadala ukawa iwapo kama kifo ni haki ya binadamu. Wataalamu mbalimbali walieleza kwamba kama tunakubaliana kwamba binadamu ana haki ya kuishi basi lazima tukubaliane kwamba binadamu anaweza kususia haki ya kuishi kama watu wanavyosusia haki nyingine let say haki ya kula. Kwanini mtu asususie haku yake mwenyewe ya kuishi? Mjadala mkali ulijikita kwenye sheria mbalimbali za kimataifa za haki za binadamu kama the Internationa Covenant on Civil and Political Rights (ICCPR), Universal Declaration of Human Rights (UDHR). Sheria hizi zimetambua haki ya kuishi ambapo baadhi ya wataalamu walidai kwa kuitambua tu "kuishi" kama haki basi pia kuna haki ya kufa kwamba mtu atachagua ama kufa au kuishi yeye mwenyewe. Katika kesi hii iliamriwa kuwa kuweka haki ya kufa kunapingana na haki ya msingi ya kuishi.

Hata hivyo katika nchi za Uholanzi, Marekani na Ubeligiji kuna kitu kinaitwa EUTHANASIA kimeruhusiwa kisheria ambapo mgonjwa ambaye yupo katika hali mbaya ambayo imethibitika hawezi kupona anaruhusiwa kuomba kifo cha haraka kwa msaada wa daktari ili kuepukana na mateso ya kuugua kwa muda mrefu ambapo mwisho wa Siku atakufa tu. Euthanasia inaitwa GOOD DEATH au MERTH KILLING.

Euthanasia imekuwa ikitekelezwa zaidi kupitia haki ya binadamu ya hivi karibuni ambapo mgonjwa anayo haki ya kugomea matibabu ili afe (the right to refuse treatment) ili kuepukana na matibabu ambayo yanarefusha muda wa kuishi japo kwa mateso makubwa.

Katika kesi moja ya nchini Uingereza ya Airedale NHS Trust v Antony Bland,
Antony Blanda alipata ajali akapoteza fahamu akiwa hospitali alikuwa akilishwa kwa kutumia mirija, madaktari walithibitisha kuwa hataweza kupona. Wanafamilia waliiomba hospitali na madaktari kuondoa mirija ya chakula ili ndugu yao afariki kwani hata akiendelea kulishwa hatapona. Lord Lowry ni mwanaharakati wa kutetea wasiojiweza alipinga kitendo hicho, kesi ilifika mahakama ya juu ya Uingereza ambapo madaktari waliruhusiwa kutoa mirija hiyo ili Bland afe. Jaji aitwaye Lord Mustill. alisema

" The conclusion that the declaration be upheld depends, crucially on a distinction drawn by the criminal law between acts and omission, and carries with it inescapably a distinction between, on the one hand what is often called "mercy killing", where active steps are taken in a medical context to terminate the life of a suffering patient..."

Nchi ya kwanza kuruhusu Euthanasia ilikuwa Uholanzi mwaka 2000,
Tukio la kwanza lilianza na Daktari aitwaye Philip Sutorius ambaye alimsaidia kufa seneta mstaafu aliyeitwa Bongersma aliyekuwa na umri wa miaka 86 kwa sababu kwamba alikuwa mgonjwa aliyechoka na maisha asiye na matumaini yoyote. Daktari Philip alishtakiwa kwa kuua na mahakama ya juu ya Uholanzi (Supreme Court) haikukubaliana na utetezi wa Dokta Philip ilimkuta na hatia ya kuua kwa kukusudia lakini haikumpatia adhabu yoyote. Kutokana na umaarufu wa huyo Seneta mjadala mkubwa uliibuka muswada ukapelekwa bungeni ukapitishwa hivyo Euthanasia ikaruhusiwa nchini Uholanzi rasmi mwaka 2002.

Nchini Uingereza muswada wa kuruhusu Euthanasia ulifeli kupitishwa mwaka 2006 lakini tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa madaktari nchini Uingereza hufanya Euthanasia indirect kwa kutumia dawa za kupunguza maumivu zinazofupisha maisha inasadikika zaidi ya asilimia 30 ya vifo vya wagonjwa mahospitalini hufa kwa njia hiyo huku uholanzi ikiwa na asilimia 25,

Badhi ya nchi zilizoruhusu Euthanasia ni Ubeligiji na marekanu
 
Back
Top Bottom