Kifo kupitia mikono ya POLISI – Kosa la Marehemu?


Mkandara,

Tunahitaji elimu maalum kwani inaweza kutuepusha kufikia ufumbuzi kwa njia ya Maumivu na taabu kama tunayoipitia sasa.

Unyama ni utambulisho kwa Wanyama wote wanaoishi mbugani pamoja. Unyama ni commonness na unity inayofanya diversity ya hao wanyama wengi. Kwa kuwa wanyama WANATII unyama wao na diversity yao kama jamii wanakuwa HAWANATATIZO linaloipata jamii ya “WATU na UTU wao”.

Wanyama wanakubaliana ndani ya Unyama wao kuishi pamoja huku wakizingatia utofauti wao kama wanyama lakini usio pinga unyama wao. Yaani, tumbili, simba, chui, viboko, tembo nk pamoja na kuwa wanaonekana tofauti napamoja na kuwa wanazingatia tofauti zao na kuziheshimu lakini bado ni Wanyama na kwa kuzingatia tofauti zao wanajenga ecosystem ambayo nayo inawatedea haki kwenye uso wa dunia kwa kuwapa maisha bora na yeneye mafanikio.

Kwa jamii hii ya wanyama hakuna tatizo la “elimu” kwani Divesity imetumika ku “reinforce the unity which is the essence”.

Kwenye familia Baba kama kiongozi anajikuta na watoto kumi. Anajitahidi kuwajenga pamoja na tofauti zao za ujana kuwa LAZIMA kutotofautiana na lazima kuwa familia moja yenye umoja na mshikamano. Inafika hata wakati mwingine anapitiliza na kuwalazimishia, Imani, lafudhi ya lugha ya kabila lao, aina ya mavazi, sanaa, itikadi za siasa, mke au mume wa kuoa au kuolewa nk. Wanapokuwa kwenye umri mdogo hilo linaonekana kama “kuwezekana” na kuonekana kama familia iliyoshinda tofauti zote na kusimamia UTU na maadili ya familia na/au kwa mtizamo mpana unaweza kuliona TAIFA LETU!

Sasa lina miaka 50 kila mtoto kakomaa! Sio motto tena!!Anajitambuana anataka kujielelza kila mmoja kwa uhalisia wake.

Mkuu wangu umeniambaia sasa tujitahidi tuwaelimishane kuwa "KIMSINGI TOFAUTI ZETU HAZINA TATIZO .." wote kama familia au TAIFA tuzikubali kwa hekima na busara na kuzielekeza kujenga "Umoja wetu" wa UTU kwa kuwa wote sisi ni WATU kama familia na kama Taifa. Kwani Mbona WANYAMA na UNYAMA wao huko mbugani wamefuzu na kulitekeleza jambo hili kwa VITENDO. Mbona WATU wa ulaya na UTU wao wa ulaya wameweza?

Itashindiakana vipi kwa UTU wa WATU wa Tanzania wenye umriwa miaka 50? Tuuite UTU wa Watanzania kuwa ni UTANZANIA kwani ni kweli Utu ni mmoja lakini wenye kubeba Tofauti (Diversity) kadhaa zinazoendena na kila Mtu!

VEMA! Tukubaliane kuwa sasa Tutoe elimu ya Utanzania unaobeba na kuheshimu tofauti za kila mtu na imani yake, itikadi yake, jinsia, tamaduni, mavazi, taaluma nk. Nasisitiza elimu kwani bila elimu tutafikiaje lengo hilo? Mtaniambai?

Kwa kuwa Almasi itabakia kuwa almasi, Unyama kuwa unyama na Utu kuwa Utu, basi tunaamini hatuwezi kama Watu kushindana na ukweli huo.

Kwa kushindwa kuelimishana na kutii elimu hiyo basi Uasili ambao ndio Utu na Ubinadamu wetu utatuadhibu vikali kama njia ya UASILI HUO Kutafuta Utambulisho wake usiopingika kwa mamlaka yeyote ya kibinadamu. Tuki elimika, kuerevuka na kukubali kukokota tofauti zetu katika kujenga na kurutubisha Utu amabao ndio Utanzania wetu tutaokoka waandishi wa habari kulipuliwa kinyama, vijana kukibizwa mtaani na polisi kama panya na paka, VITA, MAJANGA, MATESO, MAUMIVU ambayo honestly "IS JUST A WAKE UP CALL" ya kuturudisha kwenye Uzalendo na Utanzania wetu unaobeba tofautizote kwa HESHIMA NA UELEWA unaoatikana ndani kabisa kwenye UTU wa MTU.

1. Ni nani atoe elimu hiyo? 2. Kama Sio CHADEMA ni CCM? 3. Kama sio kwa njia ya ELIMU juu ya swala hili ni njia IPI Itumike?

4. Kama njia zote zikikataliwa si kweli kwamba kinachotokea sasa hivi Tanzania tukiache kienedelee kwa amani na utulivu kwani MWALIMU atakaye tufaa atabaki kuwa ni MAUMIVU NA MISUGUANO MIKALI! Kwani huko Ulaya na Marekani walifika vipi hapowalipo? Kwa Chaki na Mwalimu wa darasani au Maumivu ya Minyukano kama inayoendelea hapa kwetu sasahivi? Ninaami kuna tumaini jema na kuwa Tutakubali kujieleimisha na kubadilika kwa hekima na busara.
 
Kila siku nazidi kuwachukia POlice wa Tanzania
Nikipishana nao naona chuki tu
Waongo
Wazandiki
Wakorofi/Waonevu
Hawana Huruma
Wanashirikiana na Majambazi
wanakula Rushwa
Wananyanyasa
Nk Nk
Wamefundishwa kusema uongo na Serikali yao

Sijui kama hiyo ndo CV ukitaka kuwa Police uwe hivo:A S cry:
 
Polisi wanahitaji mabadiliko makubwa kama ilivyo kwa vyombo vingine vya usalama. Kuua bila sababu si kitu chema.
 
Serikali kwa kutumia vyombo vya dola wanatumia mbinu za kihuni na kitoto kabisa kujaribu kufitinisha wananchi dhidi ya CHADEMA. Kujenga mazingira kwamba kila wanapofanya mikutano lazima zitokee vurugu na damu imwagike. Hii mbinu nayo inawashinda sasa wameamua kuua live!
 
Azimio Jipya,

Shukran sana ktk hoja yako na hakiika kama umenisoma sana humu JF muda wote nimekuwa nikizungumzia UMOJA wetu kwa kujali UTU wa Mtanzania lakini hauwezi kupatikana ikiwa ELIMU haikupewa kipaumbele ca juu sana na kuweka mfumo ambao utawaelimisha wengi kwa Usawa usiokuwa na shaka.

Na sintoweza kuwalalamikia watu wenye tofauti zao wanapopiga makelele ya kuonewa kwa sababu mfumo uliopo umeiweka elimu kuwa ni ya UPENDELEO (Previlege) hivyo kusahau kwamba upendeleo wa mtu hufuatia upendeleo wa maamuzi ya mtoaji elimu. Ni hulka ya Binadamu (character ya mnyama) kutafuta kujitosheleza mahitaji ya siku badala ya maandalizi ya kudumu kama wanyama wengine walioko porini. Isipokuwa tu pale ELIMU inapoingia kati ndipo utofauti wa mwanadamu na mnyama wa porini unapojitokeza, hivyo pasipo elimu binadamu huwa hana tofauti na mnyama wa porini.

Tofauti kubwa iliyopo baina yetu na wale Simba wa Serengeti ni kwamba wao hufikiria chakula kwa misimu yote ya mwaka ktk mazingira yao ili waishi (wanaishi ili wale) wakati sisi binadamu tumepewa akili ya kufikiri kama msingi wa UTU wetu..maana sisi tunakula ili tuishi, tupate nguvu na clear mind ya kufanya majukumu makubwa zaidi ya chakula. Akili pasipo Elimu ni sawa na mnyama pori. Mkuu tuko mstari mmoja...
 
Having said that, I start to wonder where is the Camera he used on that day - could be the reason behind all this (the smoking gun)..
 


Mkuu Nguruvi3 kama uliona kuwa kitu pekee cha maana ambacho Nchimbi angefanya ni kuunda tume, kama tulivosikia kaiunda tume.. Nabaki tu hapa kujiuliza hivi kuna tume ngapi hadi sasa? Maana hata sitambui! Mana jana kulikuwa na habari kuna tume imeanzishwa na Jeshi la polisi wakilenga kushirikisha the so called vyombo vya usalama kutoka jeshi la Polisi na Jeshi la Wanachi wa Tanzania… Leo naona tena kuna tume ilioandaliwa na Nchimbi (ikiongozwa na Judge Mstaafu Ihema) hapo hapo kama sikosei kuna nyingine ilio huru pia ilioandaliwa na CDM. Tume zote hizi tuombe tu Mungu something productive will come out of it.

Kuhusu hio sentensi yako ya mwisho… Naomba nipingane na wewe kidogo, tuna kila sababu ya kuwalaumu askari (sio lawama yote ni yao ILA bado wapo entitled kwa lawama baadhi. Kama ulivogusia hata wewe kwenye post yako jinsi walivo husika.

Katika utendaji wa kazi hivo kuna ile hali ya utimilivu wa huo wajibu wao ambao unatoa picha kuwa wanafurahia huo wajibu kwa kutimiza malengo yao with ‘Relish'. Tukitumia kifo cha marehemu David Mwangosi (R.I.P) kama case study nadhani umeona/umesikia maelezo ya mashahidi (1[SUP]st[/SUP] degree) kuwa walikuwepo askari walio kuwa wakimuadhibu kwa kipigo marehemu (watu sio chini ya 6), kuna Yule aliyekumbatia kumtetea kuwa sasa imetosha! Kuna aliyekuja na nguvu zake zote na silaha yake ya moto na kumpiga na silaha tumboni hadi kusababishia askari aliyemkumbatia kuvunjika mguu….

Naelewa ni kwa nini umesema kuwa wao wanatimiza tu wajibu – ILA bahati mbaya sana inaonesha wanafurahia mno kufanya huo wajibu wao wa maagizo na sio kwa walioapishwa (usalama kwa wananchi). Sad.
 
AshaDii,
Nimekupata sawia. Niliposema tusiwalaumu sikuwa na maana waachwe huru.
Maana yangu ni kuwa tusielekeze nguvu zetu huko, tatizo ni kubwa kuanzia kwa Mwema, Nchimbi, Chagonja, Kamuhanda hadi kuwafikia hao kuruta.

Nilichokusudia ni kuwaambia watu wasiondoe jicho lao katika tatizo halisi kwa ku-deal na vidagaa. Wale askari wanaweza kuswekwa ndani na OC tu na kufunguliwa mashtaka. Nchimbi na Mwema je?

In other words tusiangalie tulipoangukia, tuangalie tulipojikwaa! Lets go direct to the source. Nchimbi and Mwema.
 

Bongolander,

Nakubaliana na kila uliloongea, niombe samahani kuwa sikubaliani na kubadilisha sharia ikija kwa upande wa Polisi. Sheria zipo sawa ila implementation ndio tatizo kama ilivo katika sekta mbali mbali ambavo sharia zake hazifatwi ipasavo. Kama ilivo ada sharia mama za chombo chochote hubeba mantiki ya mission na vision ya taasisi hio. Kwa faida ya wengi nimejaribu kuingia website yao nikashindwa ila nimepata hizi (nikiamini ndizo zenyewe) angalia za polisi kama nilivo bandua kwao na kubandia hapa na tujiulize kwa kazi ya Police siku ya tukio Iringa ama Morogoro kuna mahala walifuata nguzo zao hizo?

Mission Statement

The mission of the Tanzania Police Force is to ensure the public security, safety and protection of both life and property of all inhabitants of our community; to regulate and control the flow of traffic in order to facilitate the movement of persons and goods within our towns and to reduce the impact of crime on the inhabitants of community through investigation, apprehension, and adjudication of persons involved in criminal offences.


Vision Statement

To have professional, modernisation and community policing that support maintenance of peace and tranquility by reducing incidences of crime and fear of crime; justice administration, rule of law and good governance and public safety in the country. The reformed Police Force must earn community confidence and trust, recognition and acceptance by its professional response to crimes and incidents in application of modern talents, technology and equipment.

Hapo the underlined blue hapo... ndipo the whole real deal lies... kuwa sasa nini kitafuata kama wananchi tunaendelea kupatwa na haya na serkali hata haioneshi ushirikiano wa kujali?
 


Hapo nimekupata na nakubaliana na kila neno la post yako.... Asante sana kwa mchango wako mkuu, pamoja sana.
 
AshaDii,
Swali kubwa ninalojiuliza ni competence ya askari polisi wetu? Are they that competent to know they are guided by rule of law? Training zao zinawaandaa kuhandle changamoto za sasa ndani ya Taifa letu? Au wao wanajua kupiga tu ndio suluhisho?

Hapo ndio the whole key issue inakuwa, kuwa wanasukumwa na nini na hali ni universal knowledge kuwa jukumu lao kubwa ni usalama wa raia? Hio ndio inayozaa theories kuwa wametumwa na Serkali.


Umezungumza la Msingi... mie mtazamo wangu ni kuwa hata kama Serkali inaonekana ndio inahusika moja kwa moja kuwa kupelekea vifo na kujeruhi raia bado ukweli unabaki kuwa hata CHADEMA Inabidi watambue kwa njia moja ama nyingine wanahusika moja kwa moja; tena positively na negatively...

Hawana haja ya kuendeleza shughuli zao kwa ili mradi wananchi kwa kiasi kikubwa wanawaunga mkono, inabidi wawahakikishie usalama hao wana nchi kwa kuweza kufanya njia zozote ambazo zaweza epusha vurugu na hatimae vifo vya wananchi...
 
Nitashangaa sana kama thread hii itaisha kwa malalamiko tu dhidi ya Polisi. Imetosha sasa ni wakati wa vitendo zaidi kuliko porojo. No compromise with killers.

Matola nakubaliana na wewe, this thread is just a start... Naomba tu nisema kuwa kutenda kumetofautiana. BUT kinachojalisha ni kuwa unatenda kwa ajili ya unafuu kwa lolote lile kwa jinsi kila mmoja awezavo. Naahidi kabisa nishapanga na so pushed in playing my part, naomba tu tuwe pamoja katika hilo...


Safari hio statement yako iko so absolute... Kwa maoni yangu ukifikiria na kufikia hitimisho hilo ni vema kuweka nafasi ya walakini. Kuna makundi mengi ambayo yanaweza kunufaika kwa CDM kuchafuliwa jina na kuanguka kabisa. Hasa katika Serkali yetu ambayo kuna marais wengi wa ngazi za juu... Hivo imani yako yaweza kuwa sawa ama sio sawa ama tu ni nusu ukweli wa ukweli kamili.
 
Bado maswali mengi yanazuka kila muda unavyokwenda na tunavyotahmini unyama huu:
1. Tume imekwenda kufanya uchunguzi wa kitu gani
a] Forensic examination ilifanyika kujua chanzo cha kifo?
b) Askari wanaotuhumiwa wamepewa usalama kwa kuwekwa rumande
c) Je, taarifa ya tume inatumika kama ushahidi au ni yakuweka kabatini kwa Nchimbi
d) Je,taratibu gani zinamuongoza mwendesha mashtaka wa taifa, au hii itakuwa kesi ya kijeshi?
e)Serikali ya mkoa wa Iringa ina kauli gani kwakuwa tukio hili limetokea Iringa
f) Mbunge wa sehemu husika ameshiriki vipi katika hatua za awali za kulishughulikia tatizo
 

AJ umeongea meengi kwa kina na msingi tena kwa kugusa hasa kitu gani humfafanua mwanadamu... In a way inagusia lile ambalo nimeandika katika moja ya bandiko hapo juu, kuwa wamefanya kazi yao kwa kuikumbatia na kufurahia sababu hata kama 'Amri' waliopewa ni nenda kakomeshe vurugu (Sidhani kama walisisitizwa kuwa lazima mmtese sana mtae mkamata... Hata hivo mim na wewe hatuwezi kujua).

Umegusia swala la unyama na jinsi gani inaweza kuwa vigumu kumrudisha mtu katika mstari kuwa mwanadamu wa kawaida na utu ndani yake. Naomba niseme kuwa sio kila mwanadamu kabahatika kuwa na akili yake timamu ya maamuzi kuegemea na kugubikwa na busara... Kuna watu wanaendeshwa kabisa kama mtoto mdogo hasa katika kazi ambazo watu hufanya kazi kwa makundi.

Pamoja na kusema kuwa askari katika hili wana tatizo - nadiriki kusema kama walivosema wadau wengine kama Nguruvi hapo nyumba kuwa tatizo lipo kwa uongozi wa juu na wao ni kama vidagaa. Kama IGP, RPC na Waziri wa Ulinzi wangesimamia/wangekuwa wanasimamia hili swala kwa manufaa ya wananchi hata waliopoteza maisha yao wangekuwa bado wapo miongoni mwetu. Walau thats what i think.
 
Sisi tulioshuhudia Mageuzi wakati yanaanza miaka ya '90 tunakumbuka NCR walivyotuahidi pepo kisha wakatuacha porini na na njaa pamoja na kiu. Sipendi kuamini kama cdm nao watawaacha watu kabla safari haijafika mwisho.

Hili ambalo umegusia ni la msingi.. na nakubaliana na post yako yote ila nimekoti hapa mahala sababu kwa sasa ndio hasa ninapotaka kugusia. Nguvu ya sasa ya CDM huwezi kufananisha na nguvu ya chama pinzani chochote kile kilichowahi pita. CHADEMA kwa kweli wamejipanga, ila tu tatizo ni kwamba na wao kwa kiasi fulani wana matatizo ndani ya chama chao ambacho inabidi washughulikie haraka iwezekanavo kwa faida ya kuimarisha chama chao na shughuli zao za kisiasa.

Tatizo lingine pia... Wanajiamini mno! Sio nzuri kujiamini sana sababu tu wanaona kama vile umma kwa kiasi kubwa umewakubali... Mie ni mchanga katika siasa ILA bado natambua kuwa katika Ushindi hilo sio pekee lenye tija na umuhimu; Hivo wao pia wana kazi ya ziada kujiweka sawa na pia napenda kusisitiza kuwa waepushe kuhusishwa na vurugu.
 

Mkuu Mkandara,

Watanzania ki utamaduni tulishazoea kulishwa na kutafuniwa habari… Tatizo ambalo hadi sasa bado lipo. Wengi wa wanaotoa mawazo/misimamo juu ya maswala mbali mbali ya jamii hasa Siasa ni wafuata upepo na hawaelewi ni kwa nini wanasimamia hilo wanalozungumia ama kujadili. Hapa naomba nikunukuu wewe mwenyewe katika moya ya mjadala tushawahi jadili… Uliita aina hii ya Siasa kuwa ni "Ready-Made Politics"; huwa natumia huo msemo mara kwa mara sababu ya the way it fits the meaning.

Inasikitisha kuwa huo utamaduni wa kumeza vitu bila kutafakari kwa kasi sana inakuza ‘Udini' na ‘Ukabila' ndani ya nchi yetu ambayo miaka ya nyuma ilikuwa haina hata chembe. Kwa sasa badala ya viongozi kugombea tu amani na yale ambayo wanasimamia – wana kazi ya ziada ya kuhakikisha hili la udini na ukabila linauwawa na kupotezwa daima. Ni kazi ngumu ila kwa akili na malengo inawezekana na yaweza fanikiwa pia.

Naomba nigusie kuwa pamoja na Imani yako ambayo naomba ni nukuu "...ukweli kuwa mfumo wa Utawala nchini bado ni wa chama kimoja chenye mamlaka juu ya ya kuwepo vyama vingi. Tunajidanganya sana kuwepo kwa UHURU wa vitabuni, HAKI za vitabuni na USAWA unaotazama ujenzi wa siasa za Ujamaaa na Kujitegemea..Kifupi Wadanganyika wamezidi kuchanganyikiwa zaidi"

Mie kwa mtazamo wangu naona kama kuna unafuu kuliko ingekuwa tu kuwa twaongozwa na chama kimoja. Haya mambo yanaenda taratibu na kwa hatua (baby steps), alivo saa raia wa Tanzania katika utambuzi wa mambo yanayo mzonga kijamii na kisiasa ni tofauti na miaka mitano iliyopita, ambayo pia wa miaka mitano iliyopita ni tofauti na miaka 10 iliyopita kama ilivo guaranteed kuwa itakuwa tofauti na miaka 5/10 ijayo. Hivo ni bora na huko huko ndiko tunaelekea (kwenye chama kipya kushika madaraka); Haijalishi kuwa itakuwa 2015/2020/2025 ila tu FACT inabaki kuwa watatolewa kwa njia moja ama nyingine hasa wakiendelea na ukiritimba wa sasa wa kila Nyanja na namna….

Nina swali kidogo hapo mkuu katika hio paragraph ya pili ya post niloqoute... Unaposema kuwa polisi wasilaumiwe ina mana kwa mtazamo wako unaona kama lawama yao ni kiwango kidogo sana ama haitakiwi kabisa walaumiwe?
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Zakumi,
So far you have mentioned two, I can add up a lot more to that… (Bear in mind the basis is from eye witnesses accounts and the so crystal clear pics). Adding to your first and second;

Third – In the act of drumming and thrashing him there appeared another police who tried to liberate the deceased by covering him while urging his associates to stop while urging that it was enough (But still they proceeded with the punishment.

Fourth – Like the above (third) was not adequate enough another officer came with a gun (don't know If I should call it that) and hit at point black in cold blood which resulted to the ‘on spot' death of the late David Mwangos, i in the process injuring the Police who was trying to defend him.

Fifth – The police attempted to say the pictures where fake and that the late may have been hit by striking cloud (a story which has not been revisited since yesterday; my guess was they later observed there was too much damage for the story to stick)

Take note the concern is more on how as days go on the police are increasing their brutality towards citizens instead of protecting them..
 

Well. It depends on what it means when they say public security and protecting life. Ukiangalia kiundani unaweza kuona kuwa sasa hivi polisi wetu ni source ya insecurity...unajua polisi wetu wanaua, wanapiga, wanatesa, wanatishia, wanadai rushwa kwa nguvu wakati mwingine kwa kutumia silaha....these do not show that the force is for public security as it claims.

Kimsingi sheria na taratibu nyingi zinazoongoza jeshi la polisi lengo lake ni kiundani sio kuserve wananchi, lengo lake ni kuserve serikali[kumbuka ni sheria za mkoloni na mkuu wa koloni alikuwa gavana]. Leo hii kama mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya au mkuu wa kijiji ni mhalifu na anatenda uhalifu dhidi ya raia, kimaandishi (kisheria) hazifanyi kazi.

Unajua ukiangalia kinachoandikwa na kinachofanyika unaweza kuona ni mambo tofauti kabisa. Ukitaka kujua angalia kama polisi yeyote atachukuliwa hatua halisi, that is when you will know what they say they do and what they actually do, are two different things.
 
AshaDii,

Police brutality has existed for many years in the country and the worse part is some of us support it. When they killed people at Mwembechai, only UDSM professors dared to speak against the police. The rest of us thought that police were entitled to use deadly force and we accepted the government narrative.

Today the Journalist has been killed. I am pretty sure some sympatheziers of the ruling party will continue to support police's actions no matter what you tell them.

The truth is the police force still uses the colonial manuals to train its personnel. So the tradition is police are above the law and they can do anything against innocent civilians.
 
Last edited by a moderator:
AshaDii

"Never get angry. Never make a Threat. Reason with People" -God Father/Mario Puzo

I no longer support state investigations by forming the so called tume. Kwanza report zake hatuzisikii na hakuna msaada wala mabadiliko yoyote tume hizo zimeshaleta so far.

Ila nakubaliana na Mario Puzo...never show anger to your enemies...treat them with respect ili siku ukiwarudi heshima iendelee kuwepo
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…