AJ umeongea meengi kwa kina na msingi tena kwa kugusa hasa kitu gani humfafanua mwanadamu... In a way inagusia lile ambalo nimeandika katika moja ya bandiko hapo juu, kuwa wamefanya kazi yao kwa kuikumbatia na kufurahia sababu hata kama 'Amri' waliopewa ni nenda kakomeshe vurugu (Sidhani kama walisisitizwa kuwa lazima mmtese sana mtae mkamata... Hata hivo mim na wewe hatuwezi kujua)
Umegusia swala la unyama na jinsi gani inaweza kuwa vigumu kumrudisha mtu katika mstari kuwa mwanadamu wa kawaida na utu ndani yake. Naomba niseme kuwa sio kila mwanadamu kabahatika kuwa na akili yake timamu ya maamuzi kuegemea na kugubikwa na busara... Kuna watu wanaendeshwa kabisa kama mtoto mdogo hasa katika kazi ambazo watu hufanya kazi kwa makundi.
Pamoja na kusema kuwa askari katika hili wana tatizo - nadiriki kusema kama walivosema wadau wengine kama Nguruvi hapo nyumba kuwa tatizo lipo kwa uongozi wa juu na wao ni kama vidagaa. Kama IGP, RPC na Waziri wa Ulinzi wangesimamia/wangekuwa wanasimamia hili swala kwa manufaa ya wananchi hata waliopoteza maisha yao wangekuwa bado wapo miongoni mwetu. Walau thats what i think.
Ukiangalia wakuu wa Ulinzi wa Taifa hawa, Waziri wa ulinzi, IGP , RPC na hata kamanda Mkuu kutokuwa na Mtizamo wa kuturidhisha sisi wananchi juu ya tatizo hili kutapelekea KUUMIA MIOYO YA WATANZANI NA KUISONONEKA ...
... Kwa Mtizamo wangu hii ni HATARI KUBWA KWA USALAMA SIO WA NDANI WA TAIFA ILA WA
MIPAKA YETU PIA.
NIJIELEZE!
KUTISHA, KUTESA hadi KUUA
MTANZANIA... MBELE YA KAMERA Kwa MAMLAKA iliyokusudiwa KUMLINDA NA KUMTETEA ... Kuna muachia MTANZANIA Picha ya UCHUNGU NA MAJONZI MOYONI!
Watu wengi hasa VIONGOZI WETU WA KITAIFA inaonekana kutokutambua madhara ya Kinachojijenga ndani ya Ufahamu(MIOYONI) wa waadhrika ambao ni Wananchi wanao waongoza.
Picha ya Mateso ya Dr Ulimboka iliyobaki ndani ya fahamu za Watanzania
"... Haijafa .. " yaani iko ACTIVE ikitafuta EXPRESSION kwa kila Mtanzania aliyegushwa na Tukio Lile. Kwani ni hakika kila Mtanzania aliona kwa Macho yake Dr Akitirikwa na Damu na majeraha ambayo WATANZANIA wengi wanaamini kuwa yamesababishwa na MAMLAKA iliyotegemewa KUMLINDA.
Kwa kifupi kama mamalka husika haikujisafisha mbele ya Watanzania na KUWARIDHISHA juu ya tukio lile picha hiyo itaedelea kudumu ambalo ni jambo la hatari. Ni hatari kwani kilicho moyoni kama msigano na uchungu lazima kijielelze nje hadharani, ndio maana mtindo huo wa Kutisha, Kuumiza hadi Kuua unaweza UKAANZA KUWA TAMADUNI NA MAZOEA kwenye jamii yetu kama expression ya kilichobebwa mioyoni.
Hili litafanywa bila hata mtu kufikiria mara mbili kwani ni mbegu iliyoko mioyoni kwa kila Mtanzania na Mamlaka za Ulinzi kushindwa kuwajibika Kuifuta kwa kuwaridhisha Waathirika, MTINDO huo utaanza kuwa mfumo wa kawaida wa maisha. Ndio maana Mwerevu yeyote angetegemea Tukio lile kuendelea kujirudia na kuanza kuonekana la kawaida na namana ya pekee ya jamii ya Kitanzania kijitatulia matatizo yake... "Kutisha, kuumiza hadi Kuua" ... na Ndicho kinachotokea na kitakachotokea hadi Suluhu ya haki katika misingi ya UTU NA UBINDAMU IFANYIKE wazi hadharani kupitia mamlaka hizo hizo.
Watanzania wakiendelea kuduguliwa kwa ZANA ZA KIVITA ambazo zilitegemewa kulinda MIPIKA YETU. Ina maana wote ambao wamekufa kupitia Mamlaka hizo wangetakiwa wawe ni maadui wa mipaka yetu. Lakini sivyo ilivyo ni Watanzania innocent kabisa, Picha ya Marehemu David Mwangosi ilivyoharibika inafanana na zile tulizoziona enzi hizo za MAADUI WA VITA YA KAGERA! Kwa adui aliyejaribu kuchezea mipaka yetu na kufanywa kama David alivyofanywa hiyo inaeleweka kuwa ni tabia ya VITA.
Lakini Gundua hapa kuwa Sasa ADUI amekuwa ni Mtanzania Ndani ya Nchi yake. Kinachotakiwa Kumlinda kinatumika KUMPONDAPONDA na Kumteketeza. HUU NI UDHAIFU unaoweza kutoa mwanya kwa majirani/maadui kuona kuwa sasa huu ni wakati muafaka kufanya wanachotaka maana
Wanajishambulia na kujiangamiza Wenyewe!!
Hali hii ikienedelea hivi, inaweza
KUWATAMANISHA MAJIRANI/MAADUI zetu Kutufanyia kile ambacho tunajifanyia sisi wenyewe lakini wao watakifanya kutokea kwao, hivyo dhidi ya mipaka yetu. Kwani ni kweli kabisa kuwa UDHAIFU WA KIULIZI UNAO ONYESHWA NA MAMLAKA ZA ULIZI ZA TANZANIA NDANI YA NCHI YAKE, KAMWE HAIWEZI KUWA UJASIRI NA UHODARI KWENYE KUILINDA MIPAKA YAKE!!