zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
zomba kuna wakati mwingine mkuu wangu sio lazima uchangie kitu hasa ktk maswala mazito kama haya kwa ushabiki wa chama. Uchadema na UCCM ni vitu vingine kabisa inapofikia kifo cha raia, mwananchi tena mwandishi wa habari ambaye hakuwa na silaha isipokuwa akiwa kazini. Zaidi ya hapo Polisi waliambiwa wazi kuwa huyo wanayempiga ni mwandishi wa habari na walimwona aki record pande zote mbili na mfarakano na hata huyo mkuu wa Polisi alimwona vile vile.
Unachojaribu kujenga hoja hapa ni sawa na sheria ya Makaburu (Apartheid) ambapo wananchi wafanyakazi waligoma kwenda migodini kwa madai ya nyengeza ya mshahara wakauawa bila huruma halafu kisheria ndio wenye kubeba lawama na makosa kusababisha vifo hata kama walikuwa wakidai haki zao pasipo kumshambulia mwenye mgodi ama kufanya fujo mgodini..Kuna vitu vya kutetea na hasa vinapokuwa vya kisiasa lakini sio hili.
na ifahamike tu kwamba hatuna madaraka mikoani, swala la sensa ni swala la Kitaifa, swala la Jamhuri nzima hivyo huwezi kutoa amri kuzuia watu kutofanya shughuli zao mkoani wakati nchi nzima watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida isipokuwa wneye dhamana ya kuhesabu ndio wanawafuata watu majumbani mwao na kuwahesabu. Ingekuwa hivyo basi hata wale waliokutwa hawapo majumbani wangekamatwa, wote walioenda kazini wakait wa kuhesabu wangewajibishwa vile vile. Ilani pekee iliyotolewa Kitaifa ni kwa wale watakao kataa kuhesabiwa.
Na Polisi hawahusiki kabisa na utoaji tahadhali ikiwa kamati ya sensa haikuomba kuahirishwa kwa shghuli zote ili kuwawezesha wafanye kazi kwa ufasaha na haraka.. Polisi wameingilia kazi isikuwa yao kwa sababu walijua ni Chdema tu mkoani Iringa waliokuwa na shughuli kati ya siku hizo..Hivyo wanaposema ilani ile ni kwa vyama vyote sidhani kama wanasema ukweli maana hapakuwepo na shughuli nyingine yoyote zaidi ya ile ya Chadema.
Hivi ni Polisi wangapi Tanzania hususan FFU ambao hata magazeti hawaruhusiwi kusoma wanaejuwa kuwa huyo Daudi alikuwa Mwandishi?
Hivi ni nani duniani zinapotokea fujo anatoka alikotoka kuja ku cross police line na kumvaa mkubwa wao akasilimika?
Tuache unazi. Kifo ni kifo zilizobaki ni sababu na hizo sababu nilizoweka juu haziepukiki kwa kifo cha huyu Daudi.
Ni nini kilichokuwa kinamtambulisha kuwa yeye ni Mwandishi wa habari lilipotokea tukio? ni nini kilichomfanya akamvae mkuu wa polisi, tusiwe biased kwenye hilo. Nasema huyo amma alikuwa amaemuwa kufa au kupona lakini hakubali mkutano wa chama chake uzuiliwe, au aliigia kujitowa Mhanga aondoke na askari wengine au hajui kujihami au kuhhami mwenzake zinapotokea fujo kama hizo. Yote hayo yanaishi kwenye suicide.