Kifo kupitia mikono ya POLISI – Kosa la Marehemu?


Hu mfumo unaendeshwa na katiba na sasa hivi kuna mchakato wa kubadili katiba. Usijidanganye kuwa kubadili chama ndio mwisho wa matatizo. Vyama vipya na hususan chama chenye mfumo kama wa chadema havifai kabisa, unaona wazi kabisa kuwa viongozi wa chadema hata maadili hawana, halafu unategemea lipi jema kutoka kwao?

Unaona kabisa jinsi wanavyoongea, wanavyosambaza chuki mpaka wanafikia kusema wazi kabisa kuwa hii nchi "haitatawalika" halafu bado unafikiri kuwa wao watakuwa bora? huo ni ufinyu wa mawazo. Nyota njema huonekana alfajiri. Chadema hawana madaraka ya nchi tunaona damu zikimwagika kila wanapopita wakishika madaraka jee?

Kwanza wasahau kupewa madaraka kwa kura, za nani? msidanganyike.
 
tawala dharimu zikaribiapo kuanguka haya hutokea. na sisi Tz wala sio exception. tunaona maajabu kwa vile sasa tu karibu kubadili utawala wa miaka mingi wa CCM na waanzilishi wake. na ndio maana mabadiliko kama haya yatokeapo, watawala waliopita huwekwa kitanzini kujibu hoja ya ukiukwaji wa haki za binadamu, rushwa nk. sio mambo ya kutokea duniani tu. Tz ni sehemu ya dunia na wala si kisiwa! Binafsi naona fahari kuishi Tz wakati huu wa kipindi hiki muhimu sana cha kui-shape future ya vizazi vingi vijavyo vya nchi hii....
 
Tatizo lako zomba Mkuu na wengine wa aina yako, ni kuwa nyiynyi mlionyeshwa maji ya bendera za vyama vyenu mnakuwa hamuoni mbali zaidi ya urefu wa pua zenu. Hamtaki kukosolewa wala kusikia kauli zinazopinga kile mnachoamini.

Mimi sipo hapa kuitetea Chadema na kuponda CCM wala kinyume chake. Ninatoa mawazo huru ambayo hayajanajisiwa na unazi wa chama chochote. Kama utakuwa unafuatilia michango yangu, huwa ninasema kile ninachoamini. sio ninacholazimishwa kuamini, tafauti na wewe, inapobidi kusifu, kushauri na kukemea ovu lolote nchini hufanya hivyo kwa watu binafsi na vyama vyote. Katika kufanya hivyo ninaweza kukosea kama binadamu, lakini ninahojivunia ni kuwa ni mawazo yangu huru, kwa hivyo ninapokosea sioni tabu kuomba radhi na kurejea kwenye mstari.

Angalia dondoo langu hili #9
kwenye ukurasa wa kwanza wa mjadala huu:

pamoja na dondoo hili #121
kwenye mada nyengine. Kama ni wa kutafakari, utaona kuwa mimi sisemei chama chochote:

Hiyo nyekundu niliwakusudia wengine lakini naona itakufaa wewe zaidi. Fikiri mwenyewe zomba, usikubali kuburuzwa kimawazo, mawazo huru ndicho kitu pekee mtu anaweza kujivunia, kwa sababu kimo ndani ya nafsi yake, sio mali, sio mke/mume, sio watoto, sio chama....
 
Last edited by a moderator:


Mkuu you need to remember that kuna njia mbili za kuwazuga watu. Ya kwanza ni kusema jambo hili limefanyiwa uchunguzi watuhumiwa wamekamatwa kesi iko mahakamani hatuwezi kuiingilia mahakama.....matokeo yake kesi inaenda miezi tisa...upepo unapita kombe linafunikwa. Ya pili inaundwa tume...hili sina haja ya kutolea mifano, kuna tume nyingi sana zimeundwa lakini hakuna hata moja ambayo ripoti zake zimetekelezwa, kama zimetekelezwa labda ni vipengele viwili tu kati ya 10 na zaidi.

Pamoja na kuwa tunasema nchi yetu ina mihimili mitatu ya dola, naona kivitendo uko mmoja tu na unaamua kila kitu.
 

Mkuu JingalaFalsafa,

Nimetafakari kwa kina hoja hii , Pamoja na utata wote unaoweza kujitokeza hapo nilipowekea alama ya bluu, nimekosa sababu za msingi za kunifanya nione vinginevyo...Ni tafakari ya upeo wa juu kabisa., Na bado niko kwenye kina cha tafakari hii kwa Ajili Ya matumizi ya jamii ya Kitanzannia.

Nimeona kwa kina dhana nzima ya UTU ilivyo Kuu na juu ya Dhana mbalimbali ... ndio Massha yenyewe. Watanzania wanahitaji Kujifunza na kuutambua UTU kama ndio UMOJA WAO wa KWELI na vinginevyote ni matawi tu!

Narudia tena, Ni Tafakari iliyo kwenye upeo wa juu kabisa ... Na labda iliyopitiliza kwa Matumiza ya Mtanzania wa leo. Si muoni Mtanzania wa kawaida wachilia viogozi wa CHADEMA , CCM au CUF wakikaa na kutakakari jambo hili!

Si oni Serekali ya sasa au ijayo ya Jamhuri ya muugano wa Tanzania Ikiogozwa na Mantiki ya UTU huru wa MTU!

Ni vipi Basi Mantiki hii inaweza kuwa na Maana yeyote ndani ya Jamii yetu?

Au Ni jambo la Nadharia Tu?
 
Azimio Jipya,
UTU ndio ufunuo wa fikra zetu.. UTU ndio kielelezo cha Ubinadamu wetu na kazi kubwa ya AKILI ni kupambanua right and wrong. Sasa kama hata hili linatushinda, sijui tuna tofauti gani na wanyama?..Tukikosa UTU basi ndio haya ya Unyama yanapochukua nafasi na tusione uharamu wake..
 

Hakuna Uhalisia mkuu kama MANTIKI yaani UTU, na ndio maana Realities nyingine zote zinazokiuka misingi hii ya UTU, zinashindwa kumfikisha binadamu katika maana halisi ya Maisha, yaani KUFURAHIA-FURAHA! Lakini bado tunashawishiwa kuzitumaini, hali kuwa zimesha-prove Failure! INAKERA SANA! INAUMA MNO!
Tunakataa kuishi MANTIKI na kukumbatia Nadharia Mfu! Kwa madai ya eti "imeandikwa au imesemwa kuwa, amesema, wanataka, n.k." Nani anaturoga kama sio sisi wenyewe?
"Maisha ni Furaha , na kama haipo ni upuuzi. Na Hakuna Furaha ya mtu ila watu"
MANTIKI haiwezgi kumuhukumu innocent kuwa ni guilty, wala guilty kuwa innocent.
Mungu wetu anaita sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…