Kifo ni kifo, tofauti ni umekufaje.

Kifo ni kifo, tofauti ni umekufaje.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kifo ni kifo na kila mtu atakufa na ukifa hufi tena ila kwa yule ambae bado. Hata hivyo tofauti ipo kwenye umekufaje, umefia wapi na ulizikwaje.

Kazi yetu wote ni kupambana ili watu wafe kwa namna tutayoikubali na sababu tunazozikubali kijamii, kisayansi, na kidini.
 
Kifo ni kifo na ukifa hufi tena ila yule ambae bado. Hata hivyo tofauti ipo kwenye umekuje, umefia wapi na ulizikwaje.

Kazi yetu wote ni kupambana ili watu wafe kwa namna tutayoikubali na sababu tunazozikubali pia kijamii, kisayansi, na kidini.

Ndiyo sababu Mungu alitoa amri ya Usiue .... Cain alipomuua Abel, Mungu alimuadhibu.

Sasa hii ya Maza kudai kufa watu watakufa tu ni kauli inayohitaji kukemewa kwa kila hali. Watu hawawezi kuuwawa halafu ukasema ni sawa tu. Hayo ni mambo ya Kiswahili. Hayakubaliki.
 
Familia ya Kibao: Mengine ataamua Allah
Malipo stahili ni hapahapa kwetu na palepale kwao.

Ni ujinga mtu kusema ufanyike uchunguzi wa kimataifa ili kuchunguza mtu mmoja amekufaje. Hao wachunguzi watatoka nchi gani ambako kwao hakuna wanaouawa kama kwetu? Ziko nchi kubwa duniani ambazo hata Marais wao wameuwa kianaaina lakini hawakuitisha uchunguzi wa kimataifa sembuse sisi?

Ni kumwachia Mungu tu, maana watakuwa wamekufa mashahidi wa kisiasa, kidini au kijamii.
 
Kwa akili Yako Unadhani wakija Scotland Yard wataanza na Ally Mohamed Kibao huyu wa juzi tu? 😂

Wale wataanzia mbali hata miaka 20 nyuma, waulize Kenya Mauaji ya Robert Ouko 🐼
 
Kwa akili Yako Unadhani wakija Scotland Yard wataanza na Ally Mohamed Kibao huyu wa juzi tu? 😂

Wale wataanzia mbali hata miaka 20 nyuma, waulize Kenya Mauaji ya Robert Ouko 🐼
Kwanini Scotland Yard hawakwenda Marekani kusaidia nani hasa anataka kumuua mgombea? Kwanini aliyemuaa JF Kennedy hajapatikana hadi Leo? Scotland Yard hawahitaki huko? Huwezi kumpa fisi kazi ya kumtafuta mwizi wa mbuzi wako.
 
Virus is detected
Sisi watu wa disasters preparedness and management tunajua kuwa likitokea wimbi baya la machafuko lazima muwe makini sana katika kushuhulika na janga hilo. Lazima kuwe na uratibu makini wa kila kitu kinachohitajika ili kuepusha kusababisha tukio lingine baya zaidi.

Tuepuke mihemko itakayosababisha kumpa muathilika blanket badala ya shuka na viatu badala ya maji ya kunywa.

Kwanza nani kamuua Mzee Kibao? Alete ushahidi usioacha mashaka
 
Alisikika akisema, usitufundishe kuongoza nchi
 
Ufunuo wa Yohana 13:10
10
Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.

MUNGU siyo kiziwi ,ukitenda utatendewa vivyo hivyo .
 
Kama kifo ni kifo alale chini tumchinje yeye.
 
Back
Top Bottom