Kifua Kikuu ; Adui anayewatesa zaidi watu maskini

Kifua Kikuu ; Adui anayewatesa zaidi watu maskini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
mgonjwa.jpg


Mgonjwa wa Kifua Kikuu Sugu ambaye amepata nafuu katika kiwango cha juu akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu ya Kibong'oto Mkoani Kilimanjaro. Mgonjwa huyu na wenzake wanaiomba Serikali kupunguza muda wa tiba ya Kifua Kikuu.

KWA UFUPI
Takwimu za maambukizi hayo ni kwa mujibu wa shirika la USAID la Marekani , mwaka 2007.Kati ya watu hao (120,191), 56,233 ni wale ambao wamegundulika kuwa na ugonjwa huu kupitia makohozi, kitaalam sputum smear positive (SS+ )

Kifua Kikuu (TB) ni ugonjwa ambao unafahamka kwa watu wengi katika Tanzania kutokana na madhara mengi ambayo yamejitokeza na kuonekana iwe katika familia au katika jamii kwa namna moja au nyingine.

Huu, ni ugonjwa ambao umedumu kwa karne nyingi tangu ulipogunduliwa na mtaalam kutoa Ujerumani, Dk Robert Koch mwaka 1882 na kuushangaza ulimwengu wa tiba kwa ugunduzi wake huo.

Dk Koch aliduwaza wengi kwa kutangaza mjini Berlin kuwa alikuwa amegundua chanzo cha ugonjwa huo ambao nyakati hizo ulikuwa ukisumbua wengi huko Marekani na Ulaya, kusababisha vifo.

Mgunduzi wa Kifua Kikuu, Robert Koch alipewa tuzo ya amani ya Nobel kwa ugunduzi wake huu ambao kwa kiasi kikubwa umeiokoa dunia.

Wakati ule, TB ilisababisha kifo kwa mtu mmoja kati ya saba na tangu wakati huo harakati mbalimbali zimekuwa zikiendelea katika kukabiliana nao.

Zikiwa zimebaki siku mbili dunia iadhimishe siku hiyo, Machi 24 ni vyema kuuzungumzia ugonjwa huo ambao umeendelea kuwa hatari, unaoua mamilioni ya watu ingawa kwa sasa si Marekani au Ulaya kama zama za Dk Koch, bali katika nchi maskini.

Siku ya Kifua Kikuu Duniani
Kwa nyakati tofauti, walimwengu wakiwamo wanasayansi walikaa na, kukubaliana hivyo kuanzisha Siku ya Kifua Kikuu duniani, Machi 24.
Siku hiyo ni mahsusi kwa ajili ya kufanya mapitio kuhusu hali halisi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo.


Kwa hiyo, siku hiyo ya ugunduzi wa Dk Koch hadi sasa imekuwa ikiadhimishwa kote duniani kila mwaka, kwa mwaka huu ikiwa na kauli mbiu, ‘zuia nisipate kifua kikuu.'

Azimio la UN
Mwaka 1996, Umoja wa Mataifa (UN) kupitia shirika lake la afya (WHO) ulitangazwa kuwa ugonjwa huo ni janga la dharura la dunia,hivyo kila nchi mwanachama kutakiwa kuchukua hatua madhubuti katika kupambana na ugonjwa huu.
Hii ilitokana na ugonjwa huo kuendelea kusababisha vifo vingi na madhara makubwa.


Kifua Kikuu ni nini
Kitaalamu, unaelezwa kuwa ni ugonjwa wa kuambukiza kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa.


Inaelezwa kuwa mtu menye vijidudu vya ugonjwa huo akihoa, kupiga chafya au kwa namna yoyote nyingine kurusha vitone vya makohozi yake kutoka katika mfumo wake wa hewa na kuvieneza hewani na mtu mwingine kumpata akivuta hewa ndani na hivyo kuingia katika mfumo wa hewa.

Ugonjwa wa kifua kikuu ni kati ya magonjwa matatu yanayotokea kwa kiasi kikubwa na kuwapata watu masikini zaidi .Magonjwa mengine katika jamii ambayo yanasumbua zaidi ni Malaria na Ukimwi.
Hadi sasa, Kifua Kikuu huathiri asilimia 98 ya watu katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania, Ukimwi unachukua asilimia 95 na Malaria asilimia 90.

Magonjwa haya matatu husababisha vifo asilimia 10 ya idadi ya watu wote duniani kwa ujumla, ambapo inakisiwa watu wote duniani ni 6.91 bilioni kulingana na Idara ya Sensa ya Marekani.

Kwa upande wake, Tanzania inakadiriwa kuwa watu 120,191 hupata ugonjwa huu kila mwaka.

Takwimu za maambukizi hayo ni kwa mujibu wa shirika la USAID la Marekani , mwaka 2007.
Kati ya watu hao (120,191), 56,233 ni wale ambao wamegundulika kuwa na ugonjwa huu kupitia makohozi, kitaalam sputum smear positive (SS+ ).


Vifo vinavyotokana na ugonjwa wa kifua kikuu ni 32,000 kila mwaka katika Tanzania.
Kulngana na WHO, Tanzania ni ya 15 kati ya nchi 22 ambazo zimeathiriwa na ugonjwa huu barani Afrika.


Kati ya asilimia 50 ya wagonjwa wa Kifua Kikuu waliopimwa virusi vya Ukimwi mwaka 2007, inakadiriwa kuwa asilimia 47 walikuwa pia na virusi vya Ukimwi.

Ugonjwa sugu wa kifua kikuu au multi-drug resistant tuberculosis uliathiri watu 1,300 katika Tanzania kulingana na taarifa za mwaka 2007.
Chanzo au sababu za Kifua Kikuu


Ugonjwa huu husababishwa na bakteria waitwao, Mycobacteria tuberculosis.
Kuna aina nyingi za jamii hii ya Mycobacterium kama Mycobacteria tuberculosis (ambao husababisha kifua kikuu), Mycobacteria leprae (wao husababisha ugonjwa wa ukoma),


Mycobacteria bovis (huathiri ng'ombe na binadamu), Mycobacteria afrikanum na wengineo.
Ugonjwa wa Kifua Kikuu unaweza kuathiri mapafu, mishipa ya fahamu, mifupa, mfumo wa mzunguko wa damu, ngozi, viunganishi vya mifupa (joints) na mfumo wa tumba zakuchuja vimelea vya maradhi(lymphatic system.


Mycobacteria bovis ambao huathiri ng'ombe, ni jami inayoweza kuambukiza pia binadamu kama atakula nyama au bidhaa zinazotokana na maziwa ya ng'ombe ambayo yameathirika na bakteria hawa.

Mazao mengine ya mifugo kama vile siagi, mtindi, maziwa yenyewe, cheese, ice cream na kadhalika, yanaweza kumdhuru mwanadamu endapo yalikuwa na virusi hao.

Aina hii ya bakteria huathiri mapafu, tezi (lymph nodes), tumbo na sehemu nyingine za mwili.
Wataalam wanaeleza kuwa asilimia 10 tu ya watu walio na bakteria hao jamii ya Mycobacteria tuberculosis hawapati ugonjwa huu wa Kifua Kikuu. Aina za Kifua Kikuu

Kuna aina kuu tatu za ugonjwa wa Kifua Kikuu;
-Kifua kikuu kinachosababisha madhara (active tuberculosis) – Huu hutokea pale ambapo bakteria waliopo mwilini wapo hai na kinga ya mwili imeshindwa kuwadhibiti hawa bakteria wasisababishe madhara. Watu hawa wanaweza kumuambukiza mtu yoyote kifua kikuu kwa njia ya kuvuta pumzi kama watakohoa, kutema mate, kupiga chafya, kupiga kelele iwapo watafanya vitendo hivi karibu na watu wasio na ugonjwa huu.


-Ugonjwa usiosababisha madhara (inactive tuberculosis) – Kwa kitaalamu huu pia huitwa Latent TB. Hapa inaamaanisha kuwa kinga ya mwili imeweza kuwadhibiti bakteria na kuwafanya kushindwa kusababisha madhara.

Mtu mwenye Latent TB, hana dalili za ugonjwa huu, hajisikii mgonjwa na hawezi kuambukiza mtu mwingine ugonjwa wa kifua kikuu.

Aina hii inaweza kujirudia baadaye na kuathri sehemu ya juu ya mapafu na hivyo kusababisha kikohozi cha kawaida ambacho baadaye huongezeka na kusababisha kikohozi cha damu au makohozi, homa, kupungua hamu ya kula, kupungua uzito bila sababu ya msingi na kutokwa jasho kwa wingi kuliko kawaida wakati wa usiku.

-Ugonjwa uliosambaa mwilini (milliary tuberculosis) – Hii hutokea pale ambapo kinga ya mwili imepungua na kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu kuenea kupitia damu hadi sehemu nyingine za mwili kama mifupa, mishipa ya fahamu, ngozi, figo, kibofu cha mkojo, ngozi ya moyo (pericadium), mfumo wa uzazi, viunganishi vya mifupa (joints) na lymphatic system.

Husababisha homa, kupungua hamu ya kula, kuchoka na kupungua uzito.
Vihatarishi vya ugonjwa wa Kifua Kikuu


Vihatarishi vya ugonjwa huu ni;
-Uzee
-Unywaji pombe kupindukia
-Kuishi sehemu zilizo na mrundikano wa watu kama mabweni, kambi za jeshi, hospitali, mabasi ya abiria.
-Magonjwa yanayoathiri kinga ya mwili kama Kisukari.
-Wafanyakazi wa huduma ya afya
-Ugonjwa wa Ukimwi
-Utapiamlo
-Umaskini au hali duni ya kipato
-Kuishi kwenye nyumba za jamii, mfano nyumba za wazee
-Wale wasio na makazi
-Baadhi ya dawa – Dawa za ugonjwa wa maumivu ya mifupa (athritis)
-Wasafiri au watalii kutoka nchi zilizo na idadi kubwa ya ugonjwa wa kifua kikuu.


Dalili na viashiria vya ugonjwa wa Kifua Kikuu
-Kukohoa zaidi ya wiki 2-3 na kuongezeka kutoa makohozi
-Kukohoa damu
-Homa za mara kwa mara
-Kupungua au kukosa hamu ya kula
-Kupungua uzito kwa asilimia 10.
-Kutokwa na jasho kwa wingi hasa wakati wa usiku
-Uchovu
-Maumivu makali ya kichwa
-Maumivu ya kifua
-Kupumua kwa shida
Vipimo vya Kifua Kikuu
-Kipimo cha makohozi (Sputum for AFB) – Makohozi huchukuliwa kwa siku tatu mfululizo muda wa asubuhi na kupelekwa maabara kufanyiwa uchunguzi ili kuweza kugundua kama mtu ana TB.


Kwa wale wagonjwa wasioweza kutoa makohozi au wale wenye TB ya tumbo, basi hufanyiwa kipimo cha gastric lavage.

Kifua Kikuu ; Adui anayewatesa zaidi watu maskini - mwanzo - mwananchi.co.tz





 
Back
Top Bottom