akohi
JF-Expert Member
- Jul 13, 2012
- 787
- 526
Habari zenu wana JF wenzangu,
Nimekuwa nikifuatilia nyuzi mbali mbali na watu wengi wamekuwa wakilalamika kuwa matumbo yanajaa ges au wana vimbewa.
Kwanza hakikisha usiku kabla ya kulala unakunywa maziwa fresh ya uvuguvugu yenye vijiko viwili vya asali au green herbal tea yenye asali pia.
Achana kabisa na chapati, maandazi, vitumbua, soseji mbaya zaidi kuna wengi wetu wanakula chips yai na mishikaki asubuhi ...hatarii sana ndugu zangu tena anaongezea na soda juu...OMG!
Fanya hivi:
Madukani mengi siku hizi yana uza maziwa fresh ya mpaka 200ml ambayo unayapasha kisha unachanganya na ama conflakes au muesil au weetabix maana vina fibre nyingi na ni nafaka
Pia mwisho wa siku vinakusaidia kurahinisha chakula tumboni na hutakuja kupata tatizo la kuvimbiwa wala tumbi kujaa gesi.
Pia kwa muda wako jitahidi kula tango, papai, tikiti
Asanteni.
=========

Influenza said:
Kifungua kinywa kinachozungumziwa hapa ni kile ambacho kitaweza kukupa nishati lishe (kalori ) yenye theluthi moja ya nishati lishe inayotakiwa kwa siku ile.
Anza kunywa uji wa dona asubuhi au kunywa uji wa mtama au ngano ambayo haikukobolewa sana, kula magimbi, Muhogo uliochemshwa, au kama kuna viazi vitamu vile vyenye rangi ya njano hapo mambo ndipo yatakapo noga.
Ukipata kipande cha tunda la msimu kama embe, nanasi, tikiti maji, chungwa. Kwa wale wanaoishi ukanda wa pwani, uji kwa mafenesi ni chakula kizuri sana kwa mtoto aendae shuleni asubuhi au baba au mama aendae shambani au kwenye ajira yoyote ile.
Ukipata karanga kiasi kidogo tu, mlo wa asubuhi wenye mkusanyiko huo ndio mlo unakubalika kiafya. Achana na maandazi, chapati au vitumbua asubuhi vilivyojaa mafuta, vyakula kama hivyo hunenepesha mwili na sio vyakula asilia.
Vyakula asilia nilivyovianisha ndivyo vyenye mlomakapi (fibre) Vyakula vyenye mlomakapi haviyeyushwi na kusharabiwa na mwili, bali vinasaidia kusafisha mabaki ya sumu mbali mbali (free radicals) na pia husaidia anayekula vyakula vyenye mlo makapi, mtu huyo asilani katika uhai wake akiendelea kwa hatua hizo hataongezeka uzito kiholela, na pia atajiepusha na kupata saratani ya utumbo mpana (colon cancer) na ataweza kujikinga asipate ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu litapungua au kutoweka.
Tuwe na saa maalum za kula chakula cha jioni ili tuweze kupata mlo wa asubuhi wa kufungua kinywa wenye theluthi mbili za kalori zote zinazo hitajika kwa siku moja.
Watoto walale mapema wapigishwe mswaki kabla ya kulala. Asubuhi kunywa maji kama glasi mbili kuna saidia kusafisha tumbo. Fanya zoezi kidogo pata mlo wa asubuhi wenye moto kama uji na viazi vya kuchemsha magimbi na muhogo kama ipo matunda kidogo na karanga kama zipo.
Mlo huo pia ni mzuri kwa mtoto anayekwenda shule. Nishati yetu inatokana na chakula. Seli zako katika ubongo hazina sukari ya kutosha wakati wa asubuhi na huna hifadhi ya nishati lishe. Watu wengi huchoka kwa sababu hawali kifungua kinywa asubuhi. Wanakacha kifungua kinywa.