Mwanakijiji, hayo yote au mengi ya uliyoyasema na kuyataja yanahusu Tanzania. Je, ina maana na kwingineko Afrika hususan kusini mwa sahara (black Africa) na kwenyewe tatizo lao ni uongozi mbovu? Kama ni hivyo ina maana uongozi mbovu ni common denominator Afrika nzima kusini mwa jangwa la sahara. Sasa kwa nini kote huko kuwe na uongozi mbovu? Ndivyo Tulivyo kuwa hatuwezi uongozi? What is it? Maana mimi siamini kabisa kuwa hizo nchi zingine za Kiafrika zimetuzidi kihivyo. Nimeshabahatika kutembela baadhi ya nchi za Kiafrika na sikuona lolote la ziada tulilozidiwa. Kama ufisadi hata Cameroun upo. Kama vya kupenda vya Ulaya basi hata Niger wanapenda vya Ulaya. Sasa nisichoelewa ni kwa nini Afrika nzima kusini mwa sahara ni sehemu iliyo ktk kundi la nchi za ulimwengu wa tatu. Sielewi kabisa hili. Inakuwa kuwaje eneo kubwa kama hili kiwango cha maendeleo kinakuwa kimefanana sana?
Bara la Ulaya sio nchi zote zilizoendelea saana kihivyo. Hakuna uniformity ya maendeleo. Huwezi kulinganisha kwa mfano maendeleo ya Ujerumani na Uholanzi na yale ya Romania. Lakini hata hao Romania wameendelea kuliko nchi karibu zote kama sio zote kabisa za Afrika, Sasa huu uongozi mbovu ina maana upo Afrika nzima? WTF.....
Nyani unanishangaza sana,na pia nashangazwa sana kuwa wengi wanakubaliana na wewe,yani nashangazwa haswa.
Kutokana na uzoefu wa mijadala mingi hapa JF,nilishawahi kusema kuwa kwenye mijadala yoyote ambayo inaelekea kuuliza maswali ya kwanini haya na kwanini yale,ni LAZIMA turejee kwenye historia,hilo ndilo hatupendi kujifunza inapokuja kwenye mijadala kama huu.
Na pia nilishawahi kukueleza kuhusu double standards....Kwenye maelezo yako hapo juu umetoa mfano kwa kulinganisha nchi za Ujerumani na uholanzi vs Romania bila ya kujali historia na hata issue za iron curtain countries nk.....Umezungumzia similarities za waafrika kwa kuwasingle out kama blacks na wakati unazugumzia mataifa hayo ya wazungu,unakuja kuyalinganisha tena kwa vigezo vingine bila kuzingatia historia.
Huwezi ukazungumzi mambo haya na haya yako hivi bila kusema ni kwanini yako hivyo,at least hapa JF tungeweza kuwa na standards hizo,za kujaribu kufikiria zaidi na zaidi.
Kwenye issue zako ulizozungumzia hapo juu kama unge include history,basi ungezungumzia mambo mengi tu kuanzia Neo Colonialism, colonialism and all the way back to slavery,certainly pia tungezungumzia kuhusu issues za Iron curtain countries kwasababu Romania ni mojawapo,tungezungumzia pia issue za east and west German,tungezungumzia pia kuhusu Benelux,yani Belgium,Nedherlands na Luxemborg,tusingesita pia kuzungumzia impact za Capitalism,Socialism na hata Communism.
Haya mambo ni more than just kuja tu na kusema eti hawa blacks hivi and ndivyo yalivyo,and then eti hata hawa wazungu wengine wa Romania ni better than blacks blah blah wahta crap!
Halafu watu weee!maajabu!
Kwa mfano hukujiuliza ni kivipi impacts za Iron curtain Countries ama za Cold wars zilivyo tofauti na zile za Slavery,Colonialism na Neo Colonialism.
Hatuna historia bado ya kujilinganisha na wazungu,jambo ambalo hatulitambui ni kwamba sisi kama waafrika bado tunahitajika tuwe kwenye struggles za uhuru wa kweli,uhuru tulionao ni wa bandia bado,lakini kwasababu viongozi wetu wamekuwa kama watoto waliopewa suckers toka tupate uhuru wa bandia,basi na wao wanatumia nyenzo kama za mataifa yaliyoendelea kwenye kutawala na wakati ukweli ni kinyume.
Hatuwezi kukaaa hapa JF na kusema eti sisi ndivyo tulivyo,ilitakiwa useme sisi bado tuko kwenye struggles za uhuru wa kweli ambao ndio utatupatia maendeleo ya kweli.
Umezungumzia uongozi mbovu kuwa ni common denominator ya Afrika bila kutaja ukweli kuwa common denominator ya Afrika ni unique history yake...Colonialism na mengineyo niliyoyasema hapo juu ni common denominator ya Afrika,kwanini ukutake that into consideration?Mjadala huu ni mpana sana na si wa kuparamia kwa maswali na majibu rahisi rahisi,at least nilitegemea hapa JF tungekuwa hivyo.
If you dont know where you coming from,how can you know where you goin?
Unashangazwa nini na Afrika nzima kuwa na uongozi mbovu na wakati historia yao ni moja?