Monoko JMushi,
Naona kauli ya Miafrika Ndivyo Tulivyo inakukwaza sana na unafikiri ni lazima kuna kasoro kubwa kwa mtu kukiri kuwa katika Safari yetu kujijenga, kuna jambo fulani lisiloeleweka.
Mimi mapokeo yangu ya kusema ndivyo tulivyo ni kuwa sisi kama Watanzania na hata ukiongezea na kusemaWaafrika, tuna matatizo ya kukimbilia vitu vyepesi vyepesi, kuogopa kutoka jasho na kutwa ni kawaida yetu kulalamikana kutafuta mchawi.
Humu ndani JF, mchawi wetu ni CCM na Kikwete, lakini katika kundi letu hili la ulalamishi ni wachache ambao wakipewa nafasi ya kweli kwenda kufanya lolote nyumbani, wataishia kujiunga na kundi la CCM na Kikwete na hivyo kuendeleza libeneke lile lile walilokuwa wakilishikia bango.
Nina marafiki wengi ambao tulikuwa Wanamapinduzi pamoja, lakini baada ya wao kupata nafasi ya "kuneemeka" na kuajiriwa na awamu ya nne, wamesahau zile itikadi za mabadiliko na mwamko wa kimapinduzi ambao mimi bado naendelea nao mpaka leo hii.
Ndivyo tulivyo kwa kuwa hatuna malengo ya msingi na maana, bali ni malengo ya kushibisha tumbo kukidhi njaa tuliyonayo sasa hivi. Hatufikiri la kesho, sembuse la masaa matatu yanayokuja.
Kama tukibadilisha dhana na mtazamo wetu (mindsets), basi utaona kwa uharaka mkubwa kufutika kwa kauli kwua Ndivyo Tulivyo.
Ikiwa leo hii wewe bado unalia makovu ya ukoloni na utumwa na kukiri kwa nguvu ndiyo yaliyotudumaza, je ni lini utaachana na kukumbatia dhana hiyo ya unyongena kusema sasa unaamka kwa nguvu mpya na jukumu la wewe kuwa na maendeleo na umakini ni utashi wako na si msukumo wa mtu mwingine?
Mkuu nimekupata,ila kumbuka kuwa majeraha yanaweza kusababisha unfunctionality.
Kama tunataka kuangalia ni kwa kivipi tunaweza kufunction,ni lazima tuyafanyie utafiti majeraha hayo ambayo wewe umeamua kuyaita makovu,ndiyo maana huwa kuna surgery ili kuweza ku improve functionality....Nimetoa mfano huu wa surgery ya kiungo cha mwili kwasababu ndivyo dunia inavyo function,mfumo huo huo uliotuachia majeraha muda si mrefu uliopita ndio mfumo huo huo we hold dear to tukitegemea utupatie maendeleo tofauti na hapo awali.
Tusiwe wepesi wa kusahau kwasababu hata mataifa mengine pia hayakutumia miaka 50 tu toka yapate uhuru na kuendelea,ni lazima tuelewe bado tuna struggle,hizi dhana za globalisation nk ni mbinu tu za kutuchanganya waafrika tujione na sisi tuko sawa tu na sasa tunaishi kwenye dunia ambayo in reality si ya kwetu, kwa mfano JK anapotaka fly overs wakati hata treni na bara bara za kawaida yenyewe mbinde,ni kama mtoto wa kutambaa mwenye kuishi kifikra maisha ya mtoto mwenye uwezo wa kukimbia,na anajiuliza ni kwanini hawezi kukimbia na wakati ana uwezo wa kufikiri namna ya kukimbia.
Hili linahitaji kutuliza akili kwa hali ya juu na kutafakari,ni rahisi kuona mbili hii iko hapa na kwasababu kuna mbili nyingine pale,basi unajikuta uki conclude kuwa kuna nne,bila ya kujua kama hapo katikati kuna nini,yani ni minus ama plus ama divison?Hilo linapelekewa na tabia ya kuangalia tunapoangukia badala ya kuangalia pale tulipojikwaa.
Sasa tunasahau hata institutions kama world bank nk zinavyo play role kwenye issue kama hii.
Ufisadi nao ni more possible kwasababu kama hakuna ufisadi basi watakaobanwa zaidi ni wawekezaji,wawekezaji watahakikisha wana corrupt viongozi wetu,wanachohitaji viongozi wetu ni nini zaidi ya silaha za kijilinda na kusifiwa kuwa kuna demokrasia?Tunaambiwa tunaendelea na wakati inflation ni kama norm na kutoka huko hatuwezi kwasababu huwezi kutoka kwenye inlfation kama you always consume what tou cant produce,sheria zinatungwa za kuwatumikia wawekezaji na si wananchi,wawekezaji hao nao wanapewa sapoti na mataifa yao kwa mlango wa nyuma,yote hayo ni ya kuzingatia kwenye mjadala muhimu kama huu.
Hayo ya ndivyo tulivyo naomba tuyapumzishe kwasasa,tunaweza kuendelea na mjadala bila ya kujishusha.....At least kwa sasa....However ninaheshimu msimamo wako,ninacho hofu ni msimamo huo usije ukakufanya ukawa kama hao marafiki zako ambao sasa hawajali tena,mentality hiyo ikishakukaa vizuri basi unakuwa hivyo....Kwasababu ukikubali kuwa mambo ndivyo yalivyo ni kwamba una admitt kutokubelieve in change.
Mwisho nakubaliana na wewe kuhusiana na issue ya mind set....Ni kweli tunahitaji mwelekeo mpya kabisa ili tuweze kupata maendeleo kwasababu unaweza kujikuta kama hao marafaiki zako,inanikumbushia ule mchezo wa utotoni unapotumwa ukamwite flani na kukuta kuna mchezo na wewe uajiunga na kusahahu ulichotumwa,mwingine naye anatumwa anajikuta kakwama,the list goes on and on.
Ni lazima tujenge standars za tofauti,sasa issue kama ya viongozi kuwaaminisha wananchi kuwa sisi ni masikini inaonekana kama ni issue ndogo lakini ni kubwa kwasababu huwezi kumtaka mtu akademand something kutoka kwenye umasikini.
Revolution once again....Revolution itakayo revolutionize our mind,we need the rgt leaders thats for sure.
Hakuna nchi iliyopata maendeleo eti kwasababu wananchi wake wote wamesoma,hata wasiosmoma wana nafasi zao kwenye jamii,kuna skilled na unskilled labors wote wanaply part kwenye any given economy,kinachohitajika ni training tu kwenye respective fileds.
Ukiitoa gari kwenye gia namba moja na kwenda kwenye nne moja kwa moja hutapata ile acceleration unayohitaji,kabla ya kuyapata maendeleo ni lazima tujijengee mazingira ya kuyapata maendeleo hayo....Hivyo basi tuangalie ni wapi tumekwama badala ya kusokomeza migia tu huku tukijua gari imekwama,hatuwezi kusema haujakwama kwasabau tu eti tuna matairi na bado yanazunguka,hilo halina maana kuwa tuko kwenye motion.