Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Benson Kigaila amesema tabia ya serikali kushiriki kuvunja sheria inatakiwa kupingwa na kila Mtanzania anayetaka utawala wa sheria, hadharani na sirini. Haya mambo lazima yapingwe kwa nguvu zote kwani yanahatarisha misingi ya demokrasia nchini.
Kigaila amefafanua kuwa Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 haitaki vyama kuomba kibali, bali kutoa taarifa ya saa 48 kwa Jeshi la Polisi ili liandae ulinzi na sio kuzuia mikutano.
Soma: Rungwe: Mwalimu alikuwa anaingilia majukumu ya mwenyekiti, Halmashauri kuu imemtengua
Amesisitiza kuwa kisingizio cha "taarifa za kiintelijensia" kinatumiwa vibaya na viongozi wa serikali, akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani, kuzuia shughuli halali za vyama vya upinzani. Kigaila ameeleza kuwa ikiwa kuna tishio lolote la usalama, jukumu la polisi ni kuongeza ulinzi au kumkamata mleta tishio na sio kupiga marufuku mikutano ya vyama.
Zaidi soma;