Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Tanzania Bara na aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kivule, Benson Kigaila, amepinga madai kuwa wananchi wa jimbo hilo walimkataa kwa kukosa sifa za kuwawakilisha, akisisitiza kuwa anajiamini na anatosha kabisa kuwa mbunge wao.
Akizungumza kwenye mahojiano na mwandishi Edwin Odemba, Kigaila ameeleza kuwa kutochaguliwa kwake kulitokana na mambo mbalimbali na si kwa sababu wananchi walimwona hafai, kwani uwezo na sifa za kuwatumikia anazo.
Kigaila amebainisha kuwa mfumo wa uchaguzi nchini tangu mwaka 1995 umekuwa ukikabiliwa na changamoto na kasoro nyingi zinazozuia kuwepo kwa uchaguzi huru na wa haki.
Amefafanua kuwa sheria na muundo wa Tume ya Uchaguzi unategemea misingi ya sheria za mwaka 1985 na Katiba ya mwaka 1977, mifumo ambayo ilitengenezwa wakati wa mfumo wa chama kimoja, hivyo haiwezi kutoa uwanja sawa wa ushindani katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Kigaila amesema changamoto zilizojitokeza kwenye uchaguzi uliopita 2025, kuwa kulikuwa na viashiria na matendo mengi ya ukosefu wa haki, ikiwemo mawakala wao wengi kuzuiwa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura hivyo kutokana na kasoro hizo za kimfumo zilizopo miaka yote, matokeo ya uchaguzi hayajawahi kuakisi uamuzi halisi wa wananchi bali ni matokeo ya mfumo usio sawa wa uchaguzi.
"Haiwezekani kwamba waliona sitoshi. Huenda waliona walikuwa na chaguo lingine. Lakini kwa maana kwamba mimi natosha kuwa mbunge wa Kivule, natosha, na kila mtu anaweza kujua kwamba mimi natosha kuwa mbunge wa Kivule."-Amesema Kigaila
Soma Kigaila alipoulizwa kuhusu kwanini wengi waliokimbia CHADEMA kutokuwahi kushinda uchaguzi?