Kigali peace marathon june 2025 ninatarajia kushiri naombeni ushauri wenu

Jeep wrangler

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2024
Posts
524
Reaction score
1,093
Bila shako mko salama jf members wote, nawatakia kwaresma njema na mfungo wa Ramadhani.

Ninatarajia kushiriki Kigali peace marathon ambayo hufanyika kila mwezi June kila mwaka, Kigali, Rwanda.

Lengo kuu la kushiriki sio kushinda bali ni moja ya:
1. Kujifurahisha kwa njia ya michezo.

2. Kupata wasaa wa kuchangamana na mataifa mbali mbali ( fursa)

3. Utalii ( napenda sana utalii)

Maandalizi;
Nimeanza kufanya mazoezi ya kukimbia mbio ndefu na maeneo yafuatayo nimeyachagua kwa ajili ya kujifua;
1. Mbeya (Rungwe)
2. Iringa (,Mafinga na Iringa mjini)
3. Arusha( Oldonyo sambu na Ngaramtoni)
4. Kilimanjaro ( Moshi mjinj na Marangu)

Maeneo haya nimeyachagua kutokana na hali ya hewa inayo shabihiana na Kigali.

Muda wa mazoezi;
1. Alfajiri na jioni
2. Mara 4 kwa wiki.

Baada ya utangulizi huo, nakaribisha ushauri kwa wenye uzoefu.

Asenteni.
 
Kwamba wewe una Kampuni zinakuingizia fedha bila ww kuwepo au??,au unaanza kujenga career kupitia hayo mashindano au ww ni mwanafunzi
 
hivi unawezaje kumtakia mtu Kwaresma hapo hapo ramadani njema? ni aidha Kwaresma au nothing …
 
Peace na M23?
 
hivi unawezaje kumtakia mtu Kwaresma hapo hapo ramadani njema? ni aidha Kwaresma au nothing …
Hapa kuna dini zote.
1. Waislam wamefuna na wakristo pia.
Hilo tu ndio umeliona?
 
Kwamba wewe una Kampuni zinakuingizia fedha bila ww kuwepo au??,au unaanza kujenga career kupitia hayo mashindano au ww ni mwanafunzi
Sijaja kueleza hapa kuwa nina nini na sina nini, hilo niachie mimi kila mtu aishi atakavyo
 
Peace gani wakati kuna umwagaji damu na ujambazi DRC?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…