A
Anonymous
Guest
Changamoto ya Mbutu ni Barabara ya kutoka Dege kwenda Mkwajuni mpaka kwenye Machimbo ya Vifusi.
Kwanza naomba niwafahamishe yafuatayo;
1. Barabara zote za Kigamboni zitakazojengwa material yake nikimaanisha kifusi chake kitatoka Mbutu kupitia Kwa Malale hiyo njia ya
2. SJR material yalitoka hapo.
3. Daraja la Tanzanite na yametoka kwetu.
4. Barabara ya kimbiji material yametoka kwetu Mbutu.
5. Viwanda vya cement vinachukua materia kwetu.
6. Barabara zote na madaraja yaliyoharibiwa na hizi mvua wanategemea kifusi kutoka Mbutu.
Jambo la kushangaza, sisi ndio tuna Barabara mbovu kupindukia. Jamani tunajiona kama hatuna mwakilishi wa kutusemea. Tumetelekezwa Magari ya kifusi usiku kucha yanaharibu Barabara na kutucha na mavumbi tupu mvua zikikatika.
Viongozi wanaohusika waone na wasikie kilio chetu.