Kigamboni Bridge Contract Signed


asante kwa maelezo yako
 

Acha uongo!
Mimi ni mwanachama na hamjanishirikisha.

Hivi nyie, hizo pesa mnadhani ni zenu kiasi kwamba mnaamua kuzifanyia shughuli yoyote mnayotaka?
Vipi kuhusu fedha hizo kurudi moja kwa moja kwa wanachama kwa njia ya mikopo? Wanachama tayari wanayo security/bond (mi sio mtaalam wa mambo ya fedha lkn nina hakika umenielewa) kwa hiyo hawa ndio walistahili kipaumbele katika kufaidi mabilioni wanayochanga kila mwezi.

Kuna wakati niliwahi kuongea na Bw. Crescentius Magori na alinipa mkakati kuwa mojawapo ya products mlizoziandaa kwa wanachama ni mikopo (makarabrasha ninayo). Sasa yapata miaka mi5 hakuna hata dalili za mwanzo za utekelezaji wa kauli hiyo. Nimekuwa nikifuatilia hii kitu kwa karibu sana kwenye matawi yenu lakini sijawahi kupata majawabu sahihi. Badala yake tunashuhudiafedha hizo zikitiririka kuelekea maeneo ambayo hayamfaidishi mwanachama moja kwa moja (kama mtu mmoja mmoja).
 
naomba utoe ufafanuzi zaidi kama kuna kipengele kwenye mkataba unawasi wasi nacho

suala la mkataba ni kwamba cjauona,ila sasa hata hiyo ambayo hatujaiona inaonesha ina kasoro!
 
lina sehemu ya watembea kwa miguu? je nao watalipia?
So far kutakuwa na provision kadhaa wa kadhaa

lakini mambo ya kulipa na mengineyo yataamuliwa muda utakapofika panapo uzima na uhai
 
Hapana kaka ila mkurugenzi wa NSSF Dr Dau amekuwa kama whipping boy wa wana JF kuliko wakurugenzi wa mashirika mengine kama PPF au TRA na BOT ambako ufanisi na ufisadi umeshika hatamu

Sasa ndio maana tunaona bora tunaingia JF kama wanavyokuja wengine hapa ili kuweka records straight na si vinginevyo

Magufuli ni mwana siasa Dau ni technocrat kazi yake ni kutekeleza hili jambo ambali lilitakiwa litekelezwe toka enzi za mzee mkapa
 
Kwa nini moradi mingi ya NSSF inafanywa na hii kampuni ya CRJE?

Je ma sub contractor watakuwa wazalendo au kila kitu mchina?

Je ma sub contractor wazalendo ni wepi?

Site mnaingia lini rasmi?
Si kweli kuwa miradi mingi ya NSSF inafanywa na CRJE

Lakini pia haiondoi ukweli kuwa CRJE ni mmoja kati ya makampuni makubwa duniani ya ujenzi

Ma sub contractors ijuavyo wengi watachaguliwa na main contractor ambaye ataangalia mambo mengi kama quality na bei za bishaa na services zao

Fafanua unamaana gani ma sub contractor wazalendo

Site kama kila kitu kitakuwa sawa tunaingia mwezi ujao
 
Kwa maelezo yako inaonekana unajiamini kuwa unajua sana decision making process ya NSSF na unao ushahidi kuwa members hawajawakilishwa

naomba unipe ushaidi kuback up argument yako
 
Kwa maelezo yako inaonekana unajiamini kuwa unajua sana decision making process ya NSSF na unao ushahidi kuwa members hawajawakilishwa

naomba unipe ushaidi kuback up argument yako

MrNSSF usituchefue hapa,mnatuboa sana jinsi hela yetu mnaifanyia biashara wakati sisi wadau hatushirikishi na wala hatupati faida katika hizo project zenu,embu toeni mikopo kwa members wenu na sio kutupa hela yote kwenye miradi na pia kuchukua mafao hadi miezi sita wakati mifuko mingine ni wiki mbili,acheni kuwaibia wananchi nyie NSSF.
 

Hii hapa:

THE KIGAMBONI NEW CITY [ OFFICIAL ] - YouTube
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…