KERO Kigamboni kuna kero ya umeme kukatika mara kwa mara, tunaunguza vitu kila mara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero yangu ni TANESCO Kigamboni wanatutesa sana, hakuna siku umeme haukatiki na sio mara moja umeme unakatika, kuna muda mpaka mara 10 kwa siku.

Vifaa vyetu vinaungua na hakuna anayelipa, tunaomba sana ujumbe huu uwafikie TANESCO wajue wanatutesa.

Ujumbe huu uwafikie Waziri Mkuu, Waziri wa Nishati, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bwana Lazaro aone na Meneja wa TANESCO Kigamboni.

Hali hii haijaanza leo, ni zaidi ya mwaka hatuoni mwanga.

Pia soma:
~ Kila siku TANESCO wanakata umeme jioni Pugu Majohe hadi imekuwa kero
~
Mkuranga, Pwani tuna tatizo la umeme unakatika mara kwa mara, ahadi ya TANESCO kushughulikia haijatimia
 
Habari, Ndugu Mteja.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukupatia mrejesho kuhusu suala hili. Akaunti yetu ilikuwa inakabiliwa na changamoto, ambayo kwa sasa imetatuliwa na huduma imerejea katika hali ya kawaida.

Kwa kuwa muda umepita tangu ulipowasilisha taarifa yako, tunaomba tufanye ufuatiliaji wa hali ya huduma kwa sasa, kwa kuzingatia changamoto uliyoieleza awali. Baada ya kukamilisha ufuatiliaji huo, tutarejea kwako kwa mrejesho na mwongozo stahiki.

Tunaomba uvumilivu wako wakati tunaendelea kulifanyia kazi suala hili.

Asante kwa ushirikiano na uvumilivu wako. ^HN
 
Kumbe mpo humu mnasoma?
Kwakweli hii changamoto ni nchi nzima mtaunguza vi-tivii vyetu vya mkopo nyie watu..!! Haiwezekani mnakata na kurudisha kila mara..
 
Ndiyo, Ndugu Mteja. Tunapokea na kujibu changamoto na maulizo ya wateja kupitia ukurasa huu. Hata hivyo, akaunti yetu ilikuwa inakabiliwa na changamoto kwa kipindi fulani, hivyo kusababisha kuchelewa kwetu kutoa mrejesho.

Kwa sasa, tumeshaanza kufanya ufuatiliaji kuhusu changamoto yako ili kufahamu hali yake na hatua zinazohitajika kwa ajili ya kupata suluhisho.

Tunaomba utupatie muda kidogo kukamilisha ufuatiliaji na kupata taarifa kamili, kisha tutarejea kwako kwa mrejesho na mwongozo stahiki.

Asante. ^HN
 
Back
Top Bottom