PreGE2025 Kigamboni: Mwana CCM Habib Mchange akamatwa na TAKUKURU kwa Rushwa

PreGE2025 Kigamboni: Mwana CCM Habib Mchange akamatwa na TAKUKURU kwa Rushwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tetere hivi anaweza kweli kuwa mbunge? Anaota ndoto za mchana ,ajikite kwenye vipeperushi tu vyake.
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imemkamata mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Habibu Mchange kwa tuhuma za rushwa inayohusishwa na uteuzi wa ndani ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Mkuu wa TAKUKURU kanda ya Temeke, Joseph Makungu amesema walipokea taarifa za mtuhumiwa kuandaa wajumbe wa chama hicho kwa lengo la kuwapa rushwa ili jina lake lipitishwe bila kupingwa kwenye kuomba uteuzi wa ndani ya chama hicho kwa anafasi ya ubunge wa jimbo la Kigamboni.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

TAKUKURU mna deal na mambo mado madogo sana. Hivi haya mambo yanayofanywa na high profiles siyo rushwa mbona mnakamata dagaa tu?
 
Kutia Nia ni kosa la kisheria? Kuna ushahidi Gani kwa yeye kuonyesha kutia nia?
Mama Shally Kule Kilimanjaro,kagawa sukari,mkoa mzima Kwa wajumbe,Takukuru,imepiga kimya,hilo hamkuliona? Au Kilimanjaro ni Kenya?
Tatizo la kisheria usilolijua mkuu ni kwamba, kosa la mtu mwingine halikupi kinga ya kutenda kosa.

Na kosa la mtu mwingine halitumiki mahakamani kama kielelezo cha utetezi.

Likikukumba janga baba, hauwezi kujitetea kwamba 'mbona na fulani alifanya?'

Itakula kwako kwa sababu kwanza utakuwa umekiri kosa!
 
Mwacheni, CCM wote mchezo wenu ndo huo huo.
 
Back
Top Bottom