Kigamboni nauli zimepanda tayari

Kigamboni nauli zimepanda tayari

aise

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2018
Posts
5,175
Reaction score
16,488
Nauli za bajaj tayari zimepanda kutoka 500 mpaka 1,000/=

Na hakuna ufafanuzi wowote.
Jana natoka zangu mishe naambiwa nauli 1000 badala ya 500.
Hii siyo haki.
 
Ni kero sana kwa kweli, hasa hii njia ya kisiwani ambayo haina daladala.
 
Nauli za bajaj tayari zimepanda kutoka 500 mpaka 1,000/=

Na hakuna ufafanuzi wowote.
Jana natoka zangu mishe naambiwa nauli 1000 badala ya 500.
Hii siyo haki.
Kuna genge la watu wachache linaiyumbisha nchi, kuna mtu alikuja na takwimu humu kwamba kuna nchi ni landlocked na zinapitishia mafuta Tz ila bei za mafuta yao ziko chini kuliko sisi
 
Nauli za bajaj tayari zimepanda kutoka 500 mpaka 1,000/=

Na hakuna ufafanuzi wowote.
Jana natoka zangu mishe naambiwa nauli 1000 badala ya 500.
Hii siyo haki.
90% nauli za usafiri zinapandishwa na mateja .

Teja linapopiga Debe nauli 1000 basi na mwenye bus/bajaj unawaachia nauli ya mtu mmoja.

Ni wao ndy wanaropoka nauli husika.

Mateja yote pumbavu zenu.
 
90% nauli za usafiri zinapandishwa na mateja .

Teja linapopiga Debe nauli 1000 basi na mwenye bus/bajaj unawaachia nauli ya mtu mmoja.

Ni wao ndy wanaropoka nauli husika.

Mateja yote pumbavu zenu.

Ni changamoto sana mkuu!
Lakini bajaj hazina wapiga debe.
 
Ni changamoto sana mkuu!
Lakini bajaj hazina wapiga debe.
Kwani Bajaji Zinakuwa Regulated na Mamlaka Kwenye Kupanga Nauli??? Hiyo 500 ya mwanzo nani aliwapangia? Nafahamu Hizo za Daladala zinakuwa zimesajiliwa na mamlaka na mamlaka ndio hupanga nauli, bajaji nani anawapangania nauli??
 
Nitawakera wengi najua.

Ebu tutafakari pamoja; dereva anaishi kwa kutegemea makusanyo ya hizo nauli.

Yumkini amepanga chumba, analipa umeme, maji, ada za watoto, anaivalisha familia yake pamoja na dharula za kijamii k.v sherehe, misiba, matibabu

Aya za hapo juu sikutaja chakula. Twende pamoja sasa kinachompa msukumo wa kupandisha bei ya nauli; dukani kwa mangi:

Kupanda kwa vyakula na mahitaji ya nyumbani
*Lita ya mafuta ya kupikia imetoka 3,500 hadi 6,000
*Kilo ya nyama 7,000-9,000
*Mchele 1,500-2,300
*Sukari 2,500-3,000
*Ngano 1,400-2,000
*Sabuni kufulia ongezeko la 100-200-300
*Dawa ya meno 1,000-1,200-1,500
*Kopo la mkaa 500-700

Kanda ya ziwa (makazi yangu) kuna baadhi ya soda/juice za kampuni fulani zilikuwa zimeshika soko barabara; japo sio msingi sana nazo zimepanda bei.

Kwa mchanganuo huo kila mwenye shughuli yake ya kujikimu amejikuta hawezi kumudu gharama za kuendesha maisha hadi naye asogeze kiwango cha hesabu zake. Mwisho wa siku mlaji wa mwisho ndiye anayeumia.
 
Back
Top Bottom