Nitawakera wengi najua.
Ebu tutafakari pamoja; dereva anaishi kwa kutegemea makusanyo ya hizo nauli.
Yumkini amepanga chumba, analipa umeme, maji, ada za watoto, anaivalisha familia yake pamoja na dharula za kijamii k.v sherehe, misiba, matibabu
Aya za hapo juu sikutaja chakula. Twende pamoja sasa kinachompa msukumo wa kupandisha bei ya nauli; dukani kwa mangi:
Kupanda kwa vyakula na mahitaji ya nyumbani
*Lita ya mafuta ya kupikia imetoka 3,500 hadi 6,000
*Kilo ya nyama 7,000-9,000
*Mchele 1,500-2,300
*Sukari 2,500-3,000
*Ngano 1,400-2,000
*Sabuni kufulia ongezeko la 100-200-300
*Dawa ya meno 1,000-1,200-1,500
*Kopo la mkaa 500-700
Kanda ya ziwa (makazi yangu) kuna baadhi ya soda/juice za kampuni fulani zilikuwa zimeshika soko barabara; japo sio msingi sana nazo zimepanda bei.
Kwa mchanganuo huo kila mwenye shughuli yake ya kujikimu amejikuta hawezi kumudu gharama za kuendesha maisha hadi naye asogeze kiwango cha hesabu zake. Mwisho wa siku mlaji wa mwisho ndiye anayeumia.