Kigamboni planning authority

Tuna matatizo makubwa Bandari ya Tanga imekufa hivi hivi tunaona leo hii unajenga lingine kwa mwenye akili ni vigumu kuona mantiki ya uamauzi huu!

Mie si Mchumi wana uchumi watatupa mwanga wa kipi hasa is Economicaly viable!

Kigamboni Blue Diamond haizungumzwi tena ,na mwelekeo ni Bagamoyo kwa sasa!



Tega siko pengine Mhe.Tibaijuka naye anavijisenti vya kuwalipa wale wa Kibada!




 
Leo nimewasikia waziri mkuu na waziri wake wa ardhi akipiga propaganda pale Bungeni,hivi hawa watu wa Kigamboni mnataka wawe wezi au panya road ndio muwapige risasi !! Mpaka sasa mnajua wanaishije wao na familia zao ikiwa sasa ni mwaka wa sita tangu wazuiwe kufanya shuhuli yoyote ktk maeneo yao ?kuna maneno yanasemwa mtaani itabidi tuyaamini sasa kuwa Kigamboni ilishauzwa kwa George Bush ili awekeze na fedha zote alishatoa serikali imezitafuna kupitia CCM.
 


Ujue inachosha zaidi na kuumiza unaposikia porojo ile ile kiwa wakati tena kwa watu waliopewa dhamana kubwa!

Mhe. Anna Tibaijuka anafahamu vizuri hoja za Wanakigamboni kwa Undani Kabisa na Hata Ikulu ina Nakala za kutosha kuhusu hoja za Wakaazi wa Kigamboni.

Mhe.Waziri amekutana na Kamati ya Wakaazi Wakigamboni Bungeni na pia aliahidi kufanya nayo Kazi katika Mkutano wake uliofanyika Uwanja wa Machava.

Leo hii kutamka maneo kama haya kwanza ni madharau makubwa kwa mtu mwenye akili timamu


Prof Tibaijuka asalimu amri Kigamboni

Akijibu hoja hizo, Profesa Tibaijuka alisema kuanzia sasa atakuwa karibu na Ndungulile na wakazi wa Kigamboni ili waweze kufahamu kila kitu kinachoendelea.

Naomba kumkumbusha Mhe.Waziri kuwa suala hapa si wnanchi kufahamu kinachoendelea issue hapa ni wewe na Wizara yako kuwasikilizwa kwanza Wananchi wa Kigamboni na hoja zao
Naomba kukumbusha kuwa hoja zao tayari unazo mezani au kafungue makabati ya Wizarani kwako .

Wizara yako inafahamu kuwa zoezi hili la Mjimpya wa Kigamboni haijafuata Sheria ila mmeweka pamba masikioni na ndiyo maana muda wote kelele za Mbunge na wananchi imeonekana wimbo wa Mlevi.


Utasema na hili hukulijua ?
Mpaka Gazeti hili imefungwa na inawezekana ilikuwa inaelekea kugusa masilahi mapana ya wanufaikaji watarajiwa wa mradi huu.



Ni vizuri kwa hadhi yako ukafika mahali usidhalilike zaidi kwa usichoweza kukibadilisha ni vizuri ukafanya maamuzi ya Busara!
 
Kuna haja ya kuendesha maisha kiuhalisi kidogo hata kama tunatamani kuishi kama wenzetu huko Ulaya au Dunia ni nyingine.Tukiende taratibu tutafika salama zaidi.

Tamaa zetu au ndoto binafsi zisichukua nafasi kwenye shughuli ya Jamii maana waathirika wa maamuzi yetu watakuwa wengi na itakuwa vigumu kwao kumsamehe atakaye waumiza katika maisha yao na hiyo haitoshi muda mwingine hatua kama hizo huleta vurugu kwenye jamii

Kuna mambo hayako sawa katika utendaji wa Serikali!

Ebu tujikumbushe na hizi kauli mbili ya watendaji wa Serikali.

Waziri Mkuu analiarifu Bunge kusitisha zoezi husika Miezi Mitatu baadaye Waziri husika anaendelea na zoezi lileli .Sasa sijui kama Serikalini ndiyo namna ya utendaji Kazi na uwajibikaji labda wataalamu au wenye uzoefu watasaidia kufafanua.





Kingine la kushutua zaidi hivi ni Makampuni mangapi yaliomba Tenda hii na lini ilitamngwazwa na je wahusika/wadau walishiriki?





Prof Anna Tibaijuka, has stated. "Yono Auction Mart won the tender to allocate the lands to Kigamboni and Kurasini following the announcement by the ministry," she said adding;



Pengine ni muda muafaka sasa kwa serikali kwenda Angola kujionea namna wenzetu walivyofanya na mikwamo waliyopata kwa miradi kama hii.

Lakini huko nako ni mbali tunaweza kutumia NSSF maana imekuwa na miradi mingi ya ujenzi wa Nyumba na ambazo kumekuwa na malalamiko ya Bei na hii ni kiashiria tosha ya kuhofu uhalisia wa miradi kama hizi.





Naamini hatutofautiani sana na Angola kwa vipato,hivyo suala la wenyeji kutokumudu gharama za nyumba hizo bado ni tatizo halisi na mwisho wa siku ni dhuluma tu ndiyo yenye kuchukua Mkondo wake.



Miaka miwili baadaye hali imebadilika,hivyo ni lazima tufike mahali kipaumbele zetu ziendane na hali halisi ya maendeleo yetu kwa wakati tuliopo na hivyo ndivyo tunavyoweza kujiepusha na Mafisadi wa maendeleo.(Wenye pesa kutumia nafasi ya Umaskini wetu wa Kiuwezo na si Umaskini wa Mali,maana ni wazi kuwa tunazo mali nyingi za kutosha na sizizooza.



 
Haya Kigamboni mjionee usanii wa Wajumbe wa Bunge Maalum ya CCM c/o Chenge na mwenzake Sita.


Katiba pendekezwa;

Eti fidia stahiki,masihara gani haya?

Nasikitika kuwaona akina mama wengi wanapiga vigelegele kama vile tuko kwenye kuozesha binti,lakini hawachukui kujisomea maeneo muhimu na ya msingi ndani Katiba pendekezwa.

Hakuna nia njema katika Katiba pendekezwa maeneo mengi yamewekwa kihasara hasara kwa faidaa ya wachache.
Nilitegemea maneno yaliyonyooka yaani;

Fidia kulingana na thamani ya soko ya wakati husika
endapo eneo au sehemu ya ardhi itachukuliwa kwa matumizi ya maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii.

Dr Ndugulile upo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…