A
Anonymous
Guest
Mumba ni shule iliyoko Manispaa ya Kigamboni na ikiwa na darasa la awali hadi Darasa la 4 na ikiwa na Walimu wanne na mmoja wa kujitolea ila Mwalimu Mkuu na Mwalimu wa kujitolea ambae ana takriban miaka miwili ndio wanafika shule kila siku, wengine wanakuja Jumatatu na Ijumaa tu, hivyo Watoto wanakosa haki yao ya msingi ya kupata elimu bora maana Mwalimu wa kujitolea anaelemewa na kazi nyingi.
Shukrani za kipekee ziende kwa mwalimu wa kujitolea maana amekuwa msaada sana kwa Wanafunzi wote haswa haswa darasa la 4 waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mock.
Ombi langu ni Manispaa ya Kigamboni iwafikirie Walimu hawa wanaojituma bila kupata kitu wakiamini watapata ajira lakini hamna chochote wanachofaidika nacho.