Ras Kisuse
JF-Expert Member
- Sep 25, 2012
- 368
- 31
FANON NA KIGEUGEU CHA WASOMI
KUTOKUWA tayari kwa wasomi na pia kutokuwepo kwa mawasiliano kati yao na wananchi, na hasa uvivu wao, na lazima isemwe, pia woga wao katika kuchukua maamuzi kwenye wakati muafaka wa mapambano, yote hayo katika ujumla wake husababisha majanga ambayo athari zake hazielezeki
Maneno hayo yamo katika kitabu kinachoitwa Viumbe Waliolaniwa (The Wretched of the Earth) cha Frantz Omar Fanon. Alizaliwa Julai 20, 1925 huko Martingue, Visiwa vya Carribean na kufariki dunia Desemba 6, 1961 huko Bethesda, Maryland nchini Marekani. Mbali ya kuandika vitabu kadhaa maarufu duniani, Fanon alikuwa pia mwanaharakati na mpiganiaji mkubwa wa haki za binadamu duniani.