SoC02 Kigoda cha Uzalendo na Utawala Bora

SoC02 Kigoda cha Uzalendo na Utawala Bora

Stories of Change - 2022 Competition

Mr Excel

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2021
Posts
526
Reaction score
1,675
IMG-20220808-WA0004.jpg


Mchezo wa kuhamisha Kigoda kumpatia mwenzako ni rahisi sana wengi wetu tuliucheza utotoni na tuliibuka washindi wa kukaa muda mrefu na kigoda bila ya kutetereka au kukosea na hii ilitupa ujasiri na kukuza ushupavu mbele ya watoto wenzetu.

Je, Kigoda Cha uzalendo kwa mtu na mtu hivi sasa upo imara nchini? Sambamba na Ushupavu ule wa kukaa na Kigoda muda mrefu hapa namaanisha utawala bora je unazingatiwa na kutiliwa mkazo.

Uzalendo Ni Hali ya mtu kuipenda, kuilinda na kuitumikia nchi yake. Uzalendo unaanza na kupenda waasisi viongozi wa nchi, Kupenda lugha ya nchi, kupenda na kulinda rasilimali za nchi, sambamba na kutunza maliasili zote zilizopo kwa dhumuni la kizazi cha sasa na urithi wa kizazi cha baadae.

Utawala ni hali ya kutumia mamlaka ya kisiasa katika kuongoza, kutekeleza na kukamilisha matakwa ya Taifa kwa ujumla.

Utawala bora ni uzalendo wa kutumia mamlaka ya kisiasa, uchumi na maamuzi kwa haki, usawa na uwajibikaji sambamba na uwazi wa hali ya juu katika kutekeleza Sera, mipango ya Taifa na kuleta maendeleo endelevu kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Makala hii ina dira ya kupamua mitazamo juu ya suala zima la uongozi ndani ya nchi yetu.

Ukweli ni kwamba bila ya Uzalendo hakuna Utawala bora, bila ya wazalendo hakuna viongozi bora hapa ndipo tunapata viongozi wenye tamaa ya mamlaka na kuhujumu Mali za Taifa letu.

Tuangaze katika viongozi wetu tunaowapa mamlaka katika Utawala wa kidemokrasia, Kiongozi anayeikebehi nchi yake na kudharau baadhi ya watu kulingana na itikadi za kichama, kidini na kikabila basi kiongozi huyu sio mzalendo na endapo tukimuweka madarakani atashindwa kufuata misingi ya Utawala bora ya ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi, Uhuru wa kuongea, haki sawa, uwazi na uwajibikaji katika kutekeleza matakwa ya wananchi waliompa ridhaa ya kuwa na mamlaka.

Sikio kwa viongozi, Wahenga wanasema Naomba uniazime sikio lako, lakini pia kama haitoshi huwa wanasema Asiyesikia lamkuu huvunjika guu.

Twende sambamba katika kuwakumbusha ndugu viongozi wetu kuhusu nyadhifa wanazopata na hii inatakiwa iendane na mpango kazi au kitengo rasmi serikalini mbali na Bunge au kitakachoteuliwa na Bunge au Mheshimiwa Rais. Ili kiwe na nguvu ya kufuatilia mawajibisho ya viongozi ikiambatana na Kusimamiwa katika kutekeleza ahadi walizoahidi kwa wananchi, hii itasaidia kupunguza wimbi la viongozi wasio bora katika kutawala.

Kwetu wananchi, Kila mtu anawajibu wa kuwa mzalendo maana kuna msemo unasema "mbomoa nchi ndiyo mjenga nchi". Ndugu zangu hususani vijana tuache tabia ya kubeza, kutukana mitandaoni haina maana kabisa, kudhalilisha na kudhoofisha maliasili, utamaduli na rasilimali zote nchini kwa sababu hii inataufanya tusambaze sifa zisizo na haja, nje ya mipaka ya nchi yetu. Pindi viongozi wetu wakikosea tuwape udhuru chanya na tusisambaze ubaya au madhaifu yao maana hakuna mkamilifu isipokuwa Mungu Mwenyezi.
Ari ya uzalendo imepungua kwa watu, hii inapelekea mtafaruko mkubwa wa kimitazo kutoendana baina ya viongozi na wananchi.

Tunawaomba Viongozi mlinde heshima na nyadhifa zenu, pia maadili ya uongozi ni muhimu sana maana mkijiheshimu nasi tutawaheshimu. Masuala ya "kiki" kama vijana wa mjini wanavyoita hayafai kabisa katika ngazi za maamuzi na mamlaka nchini.

Tuangalie mfano hai wa maisha tunayoishi katika kaya zetu baadhi yetu maisha ni magumu katika familia za Kimasikini ila Wazazi na watoto wanakaa pamoja na wanaambiwa kwamba "msijali watoto maisha yatakuwa sawa na mjitahidi hii siri isitoke nje". Hii maana yake ni malezi na kujengewa Uzalendo wa kupenda familia bila kuisaliti hata kama maisha magumu na pia ukipata zaidi usiisahau familia yako na hivi ndivyo tunaishi katika familia zetu.

Malezi hayo yanahusiana na Uzalendo nchini hata kama Viongozi wakubwa wameshindwa kufikia kutekeleza matarajio yetu ya juu, basi wananchi tuwavumilie na kulinda madhaifu yao huku viongozi wakizidi kupambania matakwa ya wananchi na kuwaheshimu.

Muhula wa kidemokrasia ndiyo wakufanya maamuzi sahihi kwa kila Utawala mpya unaoingia hapo ndipo tunatakiwa kupendekeza wazalendo na waadilifu zaidi ya wale waliopita.

Wanaoingia madarakani wajitahidi kutunza amani ya nchi, kuhamasisha uzalendo, kuleta mabadiliko bora, fursa kwa haki na usawa, haki za binadamu kuzingatiwa na Demokrasia bora ya Utawala bora kutekelezwa kwa misingi thabiti.

Ahsanteni.
Wasalaam, Naomba upigie kura makala hii na utoe maoni yako juu ya mtazamo wa uzalendo na Utawala bora.
 
Upvote 6
Vijana na uzalendo ndani ya utawala bora
 
Inabidi Tubadilishe mitazamo ya hasi katika utawala bora na tujenge uzalendo ili tuboreshe utawala bora kwa kuwakosoa vema viongozi.
Bila ya hivyo bado tutabaki kwenye janga hili la kizazi cha kiki na maigizo mpaka kwenye mamlaka.
 
Back
Top Bottom