mamakibunju
JF-Expert Member
- Dec 28, 2013
- 1,009
- 221
Watu wengi wakiwemo mashabiki
wa Wema na Diamond walitarajia
kumuona pamoja Wema Sepetu
akimpa kampani mpenzi wake
Diamond Platnumz ambaye
alikuwa anawania tuzo ya BET
Awards 2014 huko Los Angels,
Marekani. Wema alitarajiwa
kuonekana kwenye red carpet ya
BET kama ilivyokuwa kwenye
MTV Africa Music awards
ambapo walikuwa wote S.Afrika
na kina Aunty Ezekiel na team ya
Diamond
Hata hivyo chanzo kimoja kilicho karibu na
Wema na Aunty kimeelezea
kuwa moja ya sababu iliyomfanya Wema
ashindwe kwenda BET Awards licha ya kueleza
kuwa angehudhuria kupitia Instagram siku
kadhaa nyuma ni kufanyika kwa sherehe ya
rafiki yao mmoja maeneo ya Mwananyamala
nyumbani kwa Aunty Ezekiel juzi, ambapo
asingeweza kuwaacha mashosti zake hao peke
yao pasipo sapoti yake katika shughuli hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoomba kutowekwa
wazi jina lake walicheza sana ikiwemo muziki
wenye mahadhi ya kigodoro ambayo ni ngoma/
muziki uliyojipatia umaarufu siku za hivi
karibuni kiasi cha "kuwawehusha" baadhi ya
kinadada wa mjini.
"Wema hajaenda BET Awards alikuwa kwenye
kigodoro Mwananyamala na kina Aunty, kuna
rafiki yao anaitwa Imelda alipata mtoto ndo
wakamfanyia sherehe. watu walikula, kunywa na
kusaza, walichezajee ! kajala na wema
walimaliza mgomgoro wao hapo, ntakutumia na
picha pia ila usinitaje" kilisema chanzo hicho
ingawa kilishindwa kutuma picha hizo kwa
wakati mpaka tunaandika habari hii.
Katika tuzo za BET Awards Diamond hakuwa na
team kubwa kama ilivyokuwa tuzo za MTV
nchini S.Afrika
Wema na kina Kajala katika shughuli hiyo.
Maweeee kigodoro wapi, huyo ali overstay USA last time alipoenda kule sasa wale wana sheria zao kuingia kule wema sio leo wala kesho...Na alivyokuwa na mashauzi na kupenda tension na hivi dada zake wanakaa kule unazani asingeenda kumsapoti diamond, awezi kusema ukweli wema USA no entry for the time Being....