DOKEZO Kigogo Benki ya KCBL atuhumiwa kwa ufisadi

DOKEZO Kigogo Benki ya KCBL atuhumiwa kwa ufisadi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
BENKI ya ushirika mkoani Kilimanjaro,imeanziaha uchunguzi wa tuhuma za ufisadi wa mabilioni ya fedha za benki hiyo zinamkabili kigogo mmoja ndani ya benji hiyo .

Taarifa kutoka ndani ya benki hiyo zinadai kuwa uchunguzi huo unafanywa kwa ushirikiano na Benki kuu (BoT) na Benki ya CRDB.

Ikumbukukwe kuwa,BRDB imewekeza zaidi ya Bilioni Saba kwenye benki hiyo ambayo Katika miaka ya hivi karibuni uliwekwa chini ya uangalizi na Benki kuu baada ya mtaji wake kuyumba.

Mtoa taarifa aliyezungumza kwa aharti ya kutotajwa jina lake,amesema kuwa ukaguzi mkubwa wa fedha unafanyika kwa uangalifu wa Hali ya juu ili kubaini kiasi halisi kilichofujwa na ofisa huyo na watu wengine kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa.

Kwa Sasa tunahifadhi jina la kigogo huyo kwa vile hajapatikana kuzungumzia tuhuma hizo hadi hapo tutakapompata .

Kwa wale wanaofuatilia benki hii ni kwamba ipo kwenye mchakato wa kuwa Benki ya Taifa ya Ushirika lakini wataalamu wa masuala ya uchumi wanadia mpango huo unaweza ukakwama kutokana na mwenendo usioridhisha wa uendeshaji wa benki hiyo .

Unataka kujua zaidi juu ya uchunguzi unaoendelea na nani wanahusika?,
Kuwa nasi kwenye page hii

Zaidi pia soma juu ya mkakati wa kuanzishwa kwa benki ya Tiafa ya ushirika Tanzania hapa chini .

Moshi. Tarehe 21 Aprili 2024: Ikiwa imebaki chini ya miezi miwili kabla Rais Samia Suluhu Hassan hajaizindua Benki ya Taifa ya Ushirika Tanzania (CBT), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imebariki mpango huo na kutaka ukamilishwe kwa wakati huku Benki ya CRDB ikiomba iongezewe nafasi ya kuwekeza zaidi katika benki hiyo mpya inayotarajiwa kuwahudumia zaidi wakulima hasa waliopo kwenye vyama vya ushirika.

Baraka za kuanzishwa kwa benki hiyo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mheshimiwa Mariamu Mzuzuri aliyewaongoza wajumbe wa kamati hiyo kupata taarifa za maendeleo ya mchakato ulioanza tangu mwaka 2012 wa kuanzisha Benki ya Taifa ya Ushirika.

Akiwakaribisha wajumbe wa kamati yake kuchangia mjadala wa kuanzishwa kwa benki hiyo mpya baada ya kusikiliza wasilisho la Meneja Mkuu wa Benki ya KCBL, Godfrey Ng’urah, Mheshimiwa Mzuzuri amepongeza maandalizi yaliyofanywa mpaka sasa na akasisistiza kuwa umakini zaidi unahitajika kuhakikisha malengo yanatimia kama yalivyopangwa.


“Kwa jinsi wasilisho hili lilivyojaa hoja za maana kwetu, naamini historia itatukumbuka kwa kuwa sehemu muhimu ya kuanzishwa kwa Benki hii ya taifa ya Ushirika. Tumeelezwa hapa jinsi gani benki za aina hii zilivyo imara katika mataifa mengine ambako wakulima wao wana uwezo mkubwa wa kiuchumi tofauti na wakulima wetu ambao wengi wanafanya kilimo cha kujikimu,” amesema Mheshimiwa Mzuzuri.

Kuhusu ombi la Benki ya CRDB kuongezewa uwekezaji ndani ya benki mpya inayosubiriwa, Mheshimiwa Mzuzuri amesema “kwa jinsi mlivyojitoa kuiwezesha Benki ya KCBL, ombi lenu linajadilika. Tutaona namna ya kufanikisha hilo kwa sababu ni jambo linalozunguzika.”

Alipopewa nafasi ya kuzungumza, Mwenyekiti wa Benki ya CRDB, Dkt Ally Laay alisema kila kitu kinaenda vyema kuiruhusu taasisi hiyo mpya ya fedha ianze kuwahudumia Watanzania lakini akaiomba kamati hiyo ya Bunge kuangalia namna wanavyoweza kuiongezea nafasi y akumiliki hisa nyingi zaidi za benki hiyo mpya.

“Idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za benki ni ndogo sana nchini. Ripoti ya Finscope 2023 inaonyesha ni asilimia 22 tu. Lakini sote tunafahamu hapa kwamba uchumi wa taifa letu kwa kiasi kikubwa unategema kilimo lakini wakulima wengi ndio hawana akaunti kwa sababu wanaishi vijijini. Benki hii ya ushirika itasaidia kwenda kuwawezesha na wakishaimarika watakuja kwenye benki za biashara kuendeleza miradi yao,” amesema Dkt Laay.

Benki ya CRDB ilishatoa shilingi bilioni 7 ili kuinusuru Benki ya KCBL isife baada ya mtaji wake kuyumba na baada ya uwekezaji huo wa kimkakati, tayari zaidi ya shilingi bilioni 16.8 zimekusanywa ili kuanzisha benki mpya ya TCB. Dkt Laay alitumia fursa hiyo akifafanua kwamba huko nyuma KCBL na Tacoba zilikuwa hazifanyi vizuri hivyo serikali ikaiomba Benki ya CRDB iongeze mtaji kuziwezesha benki hizi. Ili kufanikisha hilo, Benki ya CRDB ilikubali kufanya hivyo na ikatoa fedha hizo kwa Benki ya KCBL pamoja na wafanyakazi watano na wajumbe wawili wa bodi.

“Fedha hizi zilitolewa si kama mkopo bali sehemu ya umiliki kwani hisa za benki hii mpya zitakapoanza kuuzwa basi zitaingizwa kwenye ununuzi wa hisa hizo na kuongeza kiasi kingine ili kufikisha asilimia 20 ya hisa zote za benki hiyo. Naomba muiunge mkono Benki ya CRDB ambayo sasa inatoa huduma Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huku ikiwa na mpango wa kujitanu katika mataifa mengine yanayotuzunguka, iweze kununua hata zaidi ya asilimia 20 ndani ya Benki ya Taifa ya Ushirika,” amesema Dkt Laay.

Akiwasilisha mpango wa kuanzishwa kwa benki hiyo, Meneja Mkuu wa Benki ya KCBL, Godfrey Ng’urah amesema inalenga kuongeza njia mbadala za mapato kwa vyama vya ushirika, kutoa huduma zenye gharama shindani kwa kuwafikia watu wengi zaidi, na kutoa bidhaa za fedha zinazokidhi mahitaji wanachama wa ushirika.

Kuhusu manufaa yake, amesema Benki hiyo ya Taifa ya Ushirika itagusa mnyororo mzima wa thamani kuanzia masoko ya bidhaa za wakulima kuanzia wanachama wa vyama vya msingi vya ushirika, wafanyabiashara wadogo, wafugaji, wavuvi na vikundi vya Vicoba pamoja na kufanikisha miradi ya kibiashara, uzalishaji, usafirishaji na ujenzi wa maghala na ununuzi wa pembejeo za kisasa.

“Yapo malengo ya muda mrefu yaani kuanzia mwaka 2024 mpaka mwaka 2030 ya kuongeza mtaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika ufike shilingi bilioni 100. Pamoja na Benki ya CRDB itakayomilki asilimia 20, uongozi wa KCBL unafanya mazungumzo na taasisi za nje kama Rabo Bank, IFC na AFDB na Coop Bank of Kenya kuwekeza CBT,” amesema Ng’urah.

Benki hiyo pia, amesema inakusudia kukusanya mtaji huo kwa kuuza hisa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) zitakazofanikisha kufunguliwa kwa matawi yasiyopungua 10 kutoka matatu itakayoanza nayo pamoja na kuwa na mawakala zaidiya 10,000.

Ingawa mpango wa kuanzisha Benki ya Taifa ya Ushirika ulipendekezwa mwaka 2012, mchakato wake ulichelewa kwa muda mpaka mwaka 2018 bodi ya wakurugenzi wa Benki ya KCBL iliporidhia kufanya mageuzi ya uendeshaji na ukusanyaji mtaji na mwaka 2020 bodi hiyo ikaidhinisha uwekezaji wa kimkakati wa Benki ya CRDB kutekeleza ombi la serikali.

Julai 2021, Benki ya KCBL iliidhinisha mfumo na muundo wa mageuzi kuwa Benki ya Taifa ya Ushirika na Desemba mwaka huo, Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) iliunga mkono kuanzishwa kwa Benki ya Taifa ya Ushirika kupitia KCBL. Mwaka 2022 KCBL ilianza kupokea wanachama na fedha zilizokusanywa TFC kwa ajili ya kuanzisha benki hiyo.

Akieleza matumaini yaliyopo, Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt Benson Ndiege amesema licha ya mchakato huo kuchelewa kutekelezwa tangu pendekezo lilipotolewa mwaka 2012, amesema kasi ya utekelezaji wake kwa sasa inaenda vizuri.

“Tayari Tandahimba Community Bank imebadilishwa na kuwa Tandahimba Cooperetive Bank (TCBL). Uzuri wa benki ya ushirika ni kwamba mteja ndiye mmiliki hivyo inakuwa rahisi kwao kuilinda kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye,” amesema Dkt Ndiege.
RR1A5673.JPG



[IMG alt="Lambardi"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/9/9121.jpg?1207579794[/IMG]
[IMG alt="kawombe"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/281/281013.jpg?1519975216[/IMG]

[IMG alt="GwaB"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/215/215645.jpg?1483890881[/IMG]
 
Habari yako kuanzia paragraph ya kwanza mpaka ya nne inapotosha jamii, Benki ya Ushirika Kilimanjaro, KCBL kwa sasa ipo mikono salama kabisa, na tangia imeanza operation zake upya mwaka 2021 imekuwa ikiingiza faida kila mwaka, na sasa wapo mbioni kuanzisha Benki ya Ushirika ya Tanzania.

Hakuna vigogo waliokula mabilioni ya benki, kuna viongozi tu wanyuma wa benki na baadhi ya board members ambao hawakuwa waadilifu waliisababishia benki hasara miaka ya nyuma ya kiasi cha karibia bilioni 6, na kesi hii imeshafuatiliwa na TAKUKURU na ipo mahakamani kwaajili ya hatua nyingine.

Andika habari yako ukiwa na uhakika au source ya maana,
 
Habari yako kuanzia paragraph ya kwanza mpaka ya nne inapotosha jamii, Benki ya Ushirika Kilimanjaro, KCBL kwa sasa ipo mikono salama kabisa, na tangia imeanza operation zake upya mwaka 2021 imekuwa ikiingiza faida kila mwaka, na sasa wapo mbioni kuanzisha Benki ya Ushirika ya Tanzania.

Hakuna vigogo waliokula mabilioni ya benki, kuna viongozi tu wanyuma wa benki na baadhi ya board members ambao hawakuwa waadilifu waliisababishia benki hasara miaka ya nyuma ya kiasi cha karibia bilioni 6, na kesi hii imeshafuatiliwa na TAKUKURU na ipo mahakamani kwaajili ya hatua nyingine.

Andika habari yako ukiwa na uhakika au source ya maana,
Hao viongozi ni akina nani mkuu?
 
Hao viongozi ni akina nani mkuu?
Sina utaalamu sana wa mambo ya kisheria, so sijajua kama ni sahihi kuwataja, lakini sisi kama wana hisa wa hiyo Benki huwa tunashirikishwa kuhusu habari zao na mchakato wa kesi yao umefikia wapi
 
Mawazo poa makao makuu yatakuwa wapi? Haitakufa kama Amcos na benki zingine Za ushirika?
Makao makuu yatakua Dodoma, uadilifu kwa sasa ni kitu kinachozingatiwa, hivyo bodi ya benki na wanahisa wamekubaliana kuhakikisha hautajitozeza uzembe kama uliojitokeza awali
 
Habari yako kuanzia paragraph ya kwanza mpaka ya nne inapotosha jamii, Benki ya Ushirika Kilimanjaro, KCBL kwa sasa ipo mikono salama kabisa, na tangia imeanza operation zake upya mwaka 2021 imekuwa ikiingiza faida kila mwaka, na sasa wapo mbioni kuanzisha Benki ya Ushirika ya Tanzania.

Hakuna vigogo waliokula mabilioni ya benki, kuna viongozi tu wanyuma wa benki na baadhi ya board members ambao hawakuwa waadilifu waliisababishia benki hasara miaka ya nyuma ya kiasi cha karibia bilioni 6, na kesi hii imeshafuatiliwa na TAKUKURU na ipo mahakamani kwaajili ya hatua nyingine.

Andika habari yako ukiwa na uhakika au source ya maana,
Wewe unahusika na masuala ya uchunguzi au wewe ni mwanahisa ti na hujui chochote kinachoendelea huko ndani ya benki yako?
 
Back
Top Bottom