Kigogo ccm moshi mjini matatani

Kigogo ccm moshi mjini matatani

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
227
Reaction score
382
WAKATI uchanguzi ndani ya chama cha mapinduzi ccm ukitarajiwa kufanyika wiki ijayo kwa ngazi ya wilaya,katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho manispaa ya moshi,seleman Aman anazongwa na mikasa mbali mbali ikiwamo kudaiwa kuendesha biashara ya vinywaji baridi na kisha kuondoka kwenye nyumba pasipo kulipia kodi ya pango.

Seleman ambaye hata hivyo amepuuza taarifa hizo,amelalamikiwa kushindwa kulipa kodi ya pango ya miezi mitatu kwenye nyumba iliyopo Kata ya mawenzi mjini Moshi .

Mmiliki wa nyumba hiyo aliyejitamnbulisha kwa jina la Charles Mmbaga amedai kuwa pamoja na kumkubusha mara kwa mara juu ya deni hilo lakini kada huyo ameziba masikio .

Mzee Mmbaga anadai kuwa pamoja na kumwandikia barua mei 19 mwaka huu ya kumkusha kulipa kodi hiyo ya pango pamoja na madeni mengine,amekosa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa kiongozi huyo wa chama ngazi ya wilaya.

Kwa mujibu wa mzee Mmbaga,anamdai kada huyo shilingi milioni moja na nusu ikiwa ni malimbikizo ya kodi ya miezi mitatu lakini mpaka sasa ameshindwa kulipa.

"Huwezi ukaondoka kwenye nyumba ya mtu ukashindwa kulipa kodi,nimejaribu bila mafanikio kumkumbusha anilipe fedha zangu mpaka sasa sioni mwafaka",anasema.

Anadai alimwandikia barua akimtaka akabidhi nyumba pamoja na madeni aliyokuwa akidaiwa snjari na nyumba hiyo kuwa katika hali ya usafi wa mazingira lakini hadi leo yapata miezi minne tangu amwandikie barua hiyo ameshindwa kumlipa.

Akijibu tuhuma hizo,kada huyo ambaye pia anatetea nafasi yake kwanza anakiri kumfahamu mzee Mmbaga lakini anakana kudaiwa na mzee huyo na kueleza kuwa alishamalizana naye kitambo na hadaiwi chochote.

Anadai kuwa alifunga biashara kutokana na kuyumba kwa uchumi uliotokana na janga la UVICO19 ambalo lilisababisha kujiendesha kwa hasara hatua ambayo ilimfanya ashindwe kumudu gharama za uendeshaji
 
Mmeshaanza kuchafuana wenyewe kwa wenyewe .

Kama huyo mtu ana madai si aende mahakamani !

Tutoleeni upuuzi wenu humu.
 
Back
Top Bottom