KERO Kigogo: Kiwanda cha kuyeyesha Plastiki kinazalisha moshi unaosambaa kwenye makazi ya Watu

KERO Kigogo: Kiwanda cha kuyeyesha Plastiki kinazalisha moshi unaosambaa kwenye makazi ya Watu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Snipes

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2013
Posts
9,165
Reaction score
16,791
Niende moja kwa moja kwenye kero yangu, kuna kiwanda cha kuyeyusha chupa za plastiki kipo opposite na Mto Msimbazi (njia panda ya kwenda Kigogo) kile kiwanda hakina mabomba ya kusafirishia moshi kwenda angani, wakianza shughuli zao za uyeyushaji moshi unasambaa barabarani na majumbani kwa watu sasa hii kiafya sio nzuri.

Nimesoma moja ya bango ambalo lipo sehemu husika, kiwanda kinaitwa Deco Manufacturing Limited kipo maeneo ya Mchikichini pembezoni na Mto Msimbazi, (inadaiwa zamani kiwanda hicho kilikuwa kinatumiwa na Twiga cement).

Binafsi mimi sio mkazi wa hilo eneo huwa napita njia kwenda kibaruani, moshi unaosambaa katika eneo lile ukiwa ndani ya gari kwa zile sekunde 30 za kukatisha pale kwa mwendo wa gari ule moshi unaovuta kupitia puani unaona wazi huu sio wa kawaida, je vipi kwa wale Wakazi wanaozunguka eneo lile la kiwanda wanapata athari kiasi gani?

Wahusika kama mpo humu fanyieni kazi hii KERO na sio sehemu moja tu viwanda vingi hapa Tanzania mazingira yao ya kusafirisha takataka hayapo vizuri ni uhuni tu sijui hivyo vibali vinatoka vipi?

Miongoni mwa maeneo ambayo yanaonekana kuathiriwa na hali hiyo, ni Wafanyabiashara kwenye Soko la Sambusa ambalo liko pembezoni mwa kiwanda hicho, wakazi wa kigogo na watumiaji wa njia zinazopita karibu na eneo la kiwanda.
photo_2024-11-04_15-45-57 (6).jpg

photo_2024-11-04_15-45-57 (5).jpg

photo_2024-11-04_15-45-57 (4).jpg

photo_2024-11-04_15-45-57 (3).jpg

photo_2024-11-04_15-45-57 (2).jpg

photo_2024-11-04_15-45-57.jpg
 
Back
Top Bottom