GE2025 Kigogo wa CHADEMA adaiwa kukamatwa, RPC anafuatilia

GE2025 Kigogo wa CHADEMA adaiwa kukamatwa, RPC anafuatilia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Viktoria kupitia kwa Katibu wake Zacharia Obadi kimedai kuwa Makamu Mwenyekiti wake wa Kanda Khalid S. Hussein amekamatwa na Jeshi la Polisi Oktoba 02.2025

Taarifa za madai ya kukamatwa kwa kiongozi huyo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii hususani kwenye makundi ya Whatsapp kupitia taarifa iliyokuwa imetolewa na Zacharia Obadi, ambapo taarifa hiyo ilidai kuwa kiongozi huo amekamatwa akituhumiwa kutaka kushusha 'mabango ya kampeni' ya mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mapema leo, Ijumaa ya Oktoba 03.2025 baada ya kuona taarifa hiyo, Jambo TV imemtafuta Zacharia Obadi ambaye amethibisha kuwa taarifa iliyopo mitandaoni ni yake na kuongeza kuwa, Makamu Mwenyekiti huyo amekamatiwa wilayani Muleba na baadaye usiku alisafirishwa kuelekea Bukoba, mkoani Kagera,

Jambo TV imezungumza na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Kagera Daniel Damian ambapo ameeleza kuwa usiku walipokea taarifa ya kukamatwa kwa kiongozi huyo na kupitia taarifa hiyo wakaelezwa kuwa mtuhumiwa amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Bukoba, lakini mapema leo asubuhi yeye binafsi (Katibu wa CHADEMA mkoa wa Kagera) amefika kituoni hapo na kuelezwa kuwa mtu huyo hajafikishwa kituoni hapo, hivyo bado wanaendelea kufuatilia kujuwa mahali alipo

Ili kupata uthibitisho wa madai hayo, mapema asubuhi ya leo Jambo TV ilianza jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera kwa njia ya simu, ambapo awali simu yake ilipokelewa na msaidizi wake aliyeeleza kuwa Kamanda alikuwa kwenye kikao wakati huo, hivyo atafutwe baada ya saa kadhaa

1759482206110.png
Chanzo: Jambo Tv

Baadaye tena, tulipopiga simu hiyo, bahati iliyoje alipokea mwenyewe Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera SACP Blasius Chatanda ambapo alipoulizwa kuhusu suala hilo alijibu kuwa kwa wakati huo yuko nje ya ofisini, na kwamba pindi akirejea ofisini na kupata taarifa ataturejea kutupatia

"Niko nje ya ofisi, ngoja nifuatilie nijuwe ofisini kuna nini, na kama lipo limefikia wapi, maana nilikuwa nimetoka kidogo, nikipata taarifa ya kina nitakujulisha, mimi nikishakuwa tayari nitakupigia mwenyewe" -SACP Chatanda.

Pia Soma: GE2025 - Mwenyekiti wa CHADEMA Kibamba, Ernest Mgawe akamatwa kwa tuhuma za kuhamasisha Maandamano na Fujo Vituo vya Mwendokasi
 
Katibu wa chadema Jimbo la kibamba pia anahangaishwa tangu juzi baada ya watu kuimba hatumtaki mama kwenye mwendokasi
 
CCM wanahangaika kupigana na kivuli chao,wataendelea kupoteza muda wakidhani adui yao ni Chadema kumbe wananchi sasahivi wanadai chao,hata vurugu za juzi watajifariji ni chadema hawajui watu wamechoka na maigizo yao
 
Back
Top Bottom